Mkuu raisi ni mwanasiasa, anaweza toa tamko la kisiasa hivyo ni lazima akishatamka arasimishe kwa kutoa maagizo rasmi kwa watendaji nje ya jukwaa.....
Achana na mawazo ya hizo pesa zikija sawa ila usizifikirie. Watendaji hawana maagizo rasmi zaidi ya kauli ya jukwaani.
Umenikumbusha issue very genuine!
Kuna sehemu moja, Shirika la umma.
Alitembelea Bosi kubwa mmoja. Akakuta Wateja kadhaa sehemu ya kazi wamekaa juani wakisubiri Huduma. Bosi kubwa akafoka kwelikweli!! Mbele ya Wateja: "Hey! Manager, yaani wewe huna huruma hata kidogo kwa wateja wetu ambao ndio wanaotuletea mapato? Haya, nataka pajegwe nyumba yao ya mpumziko haraka iwezekanavyo!"
Manager kwa kimbelembele mbio kwa wazabuni na kujenga nyumba chapchap akitumia fedha za fuel & lubricants!
Wakaguzi walipoenda mambo yalikuwa kama hivi:
Wakaguzi: "Daa tunaona kuna jengo zuri sana hapa, ni la nini?"
Manager: (Kwa kujitutumua) "Mapumnziko kwa Wateja wakisubiri Huduma".
Wakaguzi: " Aaaa. Sasa ulipata wapi fedha kwa ajili ya ujenzi huu?"
Manager: "Kwa kuwa Bosi kubwa alisema linahitajika haraka sana libidi tutumie fedha za fuel & lubricants"
Wakaguzi:"Hee!!"(mkagizi mmoja anachukua simu na kuanza kubofyabofya)...Eee! Bosi kubwa, wakaguzi hapa. Eti uliruhusu pesa ya fuel & lubricants itumike kujengea nyumba ya kupumzikia Wateja?"
Bosi kubwa: "Nani, Mimi?
Mkaguzi:" Ndiyo wewe!"
Bosi kubwa: "Nani kasema?"
Mkaguzi:"Manager wako"
Bosi kubwa: "Hana akili huyo,kwani hajui financial regulations? Tafadhali naomba nisisumbuliwe na mambo ya kipuuzi"