Hivi mafao kwa wale vyeti feki bado ayajaanza nakumbuka mama kama alisema tulipwe

Hapana hakusema hivyo watalipwa wasiofoji ambao ni std 7

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Kajaribu kuulizia huko kwenye mifuko yalipokuwa yakipelekwa mafao yako huenda kuna chochote, kawaombe wakupe statement halafu ufuatilie barua kwa mwajiri na nyaraka nyingine za kuwasilisha kwa ajili ya kulipwa hayo mafao yako ambayo kimsingi ni michango uliyokuwa ukichangia, kama ulikuwa unakaribia kustaafu ina maana utapata kiinua mgongo na pensheni za kila mwezi.....​
 
Wapo ambao walishapuuza hilo tukio na wanacheka wakilikumbuka na hata wakiambiwa warudi kazini leo hawatataka sababu walikubaliana na hali wakapambana na sasa wana kipato cha maana.

Mkuu jitahidi uwe mmoja wao, Inawezekana.
Ukiwa mzee hauna ujanja tena wa kupambana kama ukiwa kijana.

Uzee unaambatana na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Wee subiria tu sijui nani alikuambia cheti feki mnapewa mafao. Wee jipelekepeleke kama hujatupwa lupango. Yaani cheti feki mlitakiwa muwe jela halafu wewe unaulizia mafao.
 
Acha kudanganya wenzio...endeleeni kupambana na shughuli za uzalishaji mkuu ujiletee maendeleo
Siyo uwongo. Kuna mmoja aliachishwa hapa kwetu alinitaarifu kuwa wanalipwa. Alihakikishiwa hivyo na CEO.
 
Mpaka utoke waraka wizarani na kwa katibu mkuu kiongozi kwa niaba ya rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…