Hivi magereza yetu hayawezi kuboreshwa walau mara 1 kwa wiki wanandoa wakawa wanakutana na wapendwa wao hukohuko gerezani?

Hivi magereza yetu hayawezi kuboreshwa walau mara 1 kwa wiki wanandoa wakawa wanakutana na wapendwa wao hukohuko gerezani?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Nimewahi simuliwa na mtoto wa mama mdogo aliyewahi kufungwa jela.

Aliniambia yote yanayofanyika kule ufirauni na ubabe na kila kadhia aliyokutana nayo tangu day one hadi anatoka kule.

Huenda unajua kabisa kuna baadhi ya jamaa zetu wako kule wamefungwa isivyo halali either kwa kusingiziwa nk
na wengine wamefungwa ki halali kama alivyo fungwa huyu ndg yangu na baada ya muda alitoka na kurejea tena uraiani.

Nimewahi kwenda magereza kadhaa kuwatembelea jamaa kule na kwa nje nu
niliona mazingira ya gerezani.

Mara kdhaa pia nilikuwa naenda pale nanenane dodoma na piga story na wafungwa wa kifungo cha nje
maana walikuwa wanajihusisha na kilimo pia ufugaji(kwa sasa sijui kama bado wapo)

Nao pia niliyasikia ya kwao kwa kifupi tu gerezani sio kuzuri wote walisema hivyo.Siwezi kuyasema hapa niliyoambiwa hadi waseme gerezani sio kuzuri........

Kulingana na maendeleo ya sasa yalivyo kwanini magereza yasiboreshwe na wafungwa walio acha wapendwa wao wakawa wanakutana na wapendwa wao wanaongea kuhusu familia yao na hata kushiriki tendo kuondoa upwiru na kurejesha upendo.

Ni mara chache sana mwanaume akifungwa na hata kama ni miaka3 tu kumkuta mwanamke wake bado yupo ana msubiria binafisi sijawahi kuona.Wengi wao hukuta wake zao wameolewa ama kuzalishwa na wanaume wengine hata kama huyo mama aliachiwa mali bado utakuta mali zimetapanywa ama kama sio kuisha kabisa.

Yote haya ni kwa sababu mtu akifungwa hakuna mazingira mazuri tena ya kuonana na wapendwa wake.Ni ndg wachache sana huenda kuwaona wapendwa wao walio fungwa.

Ni wazi kuwa mwanaume anapo enda jera basi familia husambaratika na mama kuolewa haijarishi mwanaume ka fungwa kwa kosa gani.Na mama akishaolewa wanaoteseka ni watoto na hatimae watoto hukatisha masomo na kwenda mtaani.Hii nina mifani zaidi ya mitano.

Ni pale tu watoto wamfungwa hukutwa wakiwa wakubwa tiyari na wanajiweza ndipo familia ile husimama na wale watoto wawe wa kiume.

Najua kuna wafungwa wenye kesi kubwa na wanahitaji ulinzi mkali hao sasa wasipewe hii nafasi ya kuonana na wapendwa wao kulingana na ukubwa wamakosa yao.

Je! serikali haioni sasa ni muda wa kurekebisha magereza na kuyafanya kuwa ya kisasa na kuepukana na magereza ya kikoloni.Maana kuna baadhi ya vitu kwa ulimwegu huu wa sasa sio sawa kuendelea kuwepo magerezani.

Mfano watu kujisaidia kwenye ndoo na kuwa bebesha(mtondoro) hii sio sawa hata kwa maaskari magereza wenyewe kuona uchafu wa bindamu wenzio daily sio sawa kabisa.

Kinyesi cha binadamu sio kizuri kuonekana kwa macho hasa kilicho changanyika na mkojo na makamasi ya watu sio sawa hata kidogo.Fanyeni maboresho sasa.Kuna nchi kama canada magereza yao ni mazuri na wameweka utaratibu mzuri wa watu kuonana na wapendwa wao kwa uzuri kabisa,.....kama sio canada mni sahihishe.

INAWEZEKANA.
 
Gereza ni sehemu ya kuteseka ili ujutie na ubadilike
Yaani wafungwa wapewe nyapu huko gereza Sasa hilo ni gereza au shughuli za kanga moko
 
Mfungwa atajifunza Nini sasa? Au ilimradi tu asionekane mtaani?

Na je, mfungwa wa kike akipewa mimba inakuwaje?

Halafu watakutana wapi kwenye kunyanduana?

Je, mtu akifikisha umri wa kutamani kuwa na mwenza ataruhusiwa kutafuta? Na muda wa kutafuta atapata wapi?
 
Mbona wakike wanaenda na mimba wengi tu,sembuse kupatia mimba uko uko.
Kukutana wanaweka vyumba special.kumbuka hiyo inakua kwa wanandoa tu,mke akienda kumuona mume wake anaenda na cheti Cha ndoa,wanapewa dakika zao 20 ,za kuchapana.
 
Kukutana wanaweka vyumba special.kumbuka hiyo inakua kwa wanandoa tu,mke akienda kumuona mume wake anaenda na cheti Cha ndoa,wanapewa dakika zao 20 ,za kuchapana
 
Mbona wakike wanaenda na mimba wengi tu,sembuse kupatia mimba uko uko.
Kukutana wanaweka vyumba special.kumbuka hiyo inakua kwa wanandoa tu,mke akienda kumuona mume wake anaenda na cheti Cha ndoa,wanapewa dakika zao 20 ,za kuchapana.
Magonjwa yatakuwa mengi sana huko
 
Gereza ni sehemu ya kuteseka ili ujutie na ubadilike
Yaani wafungwa wapewe nyapu huko gereza Sasa hilo ni gereza au shughuli za kanga moko
 
Back
Top Bottom