Hivi makomando wa JWTZ wako competent kweli kulinganisha na wenzao wa nchi nyingine?

Lilikua chini ya majeshi ya UN nchi zikiwa Tanzania,S/Africa(Hawa walikua wanatoa air support) na Malawi.M23 walisepa wakaenda Uganda na wengine Rwanda.Na wiki chache zilizopita hao M23 waliingia Congo wakakinukisha kidogo then wakasepa zao.
Brigate iliongozwa na Mwakibolwa kipindi hiko akiwa Brigedia.

Ilikuwa sio sahihi kupambanisha kikosi cha waasi wenye askar pengine wasiozid 500 na Brigate nzima.
 
Kama nitakuwa natowa siri nisamehewe ila kwa taarifa fupi tu huwa wanajeshi wetu watanzania huenda mafunzo mbali mbali ya kimedani katika nchi mbali mbali na huko kote huwa wanafaulu vizuri sana kuliko hao mnaowaogopa.
Askari wetu wanaweza kuhimili mazingira yoyote yale kivita na wako na akili ya kupambana na kukabiliana na mazingira magumu. Hongera JWTZ
 
Hapo kuna siri gani sasa? Kwa hiyo unataka kutuaminisha majeshi mengine yakienda huko huwa hayafanyi vyema? Endeleeni kujazana ujinga kuwa majeshi ya nchi nyingine ni Failure ili hali kwenye ground wako njema zaidi.
 
Dooooh izi rekodi mnatoaga wapi. Unajua ni wanajeshi wangapi wa JW waliuawa Congo ?
Ni kiasi kidogo hawafiki 20 Kwa majeneza yaliyoletwa toka Kongo kuzikwa Tanzania wazi mbele ya Vyombo vya habari na ndugu wakishuhudia
 
JWTZ najivunia Jeshi langu. Bila kujali mapungufu yao ni Jeshi bora kabisa
 
You are not serious. Hapo tu majuzi majeshi ya Kagame yalitoka yalikotoka kuja kuchachafya Msumbuji, sisi kimyaaaaaa!
Sijui kwanini watu wameshikilia huu msimamo kuwa Tanzania haikushiriki suala la Msumbiji. Unajua Makubaliano ya SADC hadi kuamua Rwanda ndiye ashiriki? jirani sio Tz tu, kwanini hajaenda South Afrika, kwanini hajaenda Malawi, kwanini hajaenda Zimbabwe? Tatizo unadhani kupeleka vikosi vya nchi, ni kama wewe unavyokodi masai kuja kukulindia nyumbani kwako. Vita ni mikakati. Na ukumbuke vita ya Ugaidi, si sawa na vita dhidi ya Waasi au wapigania Uhuru.

By the way, Tanzania tumeshiriki sana kijeshi nchi nyingi Afrika toka miaka ya 1960 hadi 1990. Miaka 30 ya kutumia rasilimali zetu kwa ajili ya nchi zingine, kwa sasa imetosha. Tunajenga uchumi. Tutashiriki, sio kupeleka vikosi.
 
Wakiwa wa dada haimaanishi kuwa ni walaini. Tofautisha wanawake wanaoshindania urembo na wanawake wanaohudumu kwenye jeshi. Ni makundi mawili tofauti.
Wote watabaki kuwa wanawake tu......mmoja kuwa kwenye urembo na mwingine kuwa jeshini hakubadili jinsia zao.
 
Hahahahaha yaani mafurushi sijui wametia nini, kwa kweli napata mashaka na wakufunzi wa hawa vijana wetu.
Yale yalikuwa ni maonyesho tu ya ukakamavu/ utayari... isitoshe askari maalumu (commando) kubeba mizigo haishangazi huenda amebeba vyakula,dawa,vifaa vya mawasiliano, vifaa vya matibabu ya dharura, vifaa vya kazi mf darubini, silaha za ziada n.k

Msijifanye wajuaji kupindukia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…