Hivi Malaika huzaa na kufa pia?

Mbona nmewahi kusikia kuwa kuna majini huwa wanazaa na binadamu..?! Fatilia vipindi vya marehem mzee Yahya Hussein
 
Parapanda itakapolia tutafufuka katika wafu na kupewa miili mipya, kwahiyo km ulipanda dhambi utaelekea kunako hukumu yako na km ulipanda mema basi utaingia ktk mji ule mtakatifu, mji wa yerusalemu
Very imaginary, lakini poa maana kuna mambo yapo kiulimwengu wa roho zaidi ukiyatafakari ktk ulimwengu wa mwili huwezi kupata majibu yake!
 
Mbona nmewahi kusikia kuwa kuna majini huwa wanazaa na binadamu..?! Fatilia vipindi vya marehem mzee Yahya Hussein
Mmmh hapa nisubiri wajuvi!
 
Mkuu hata mm naamini Mungu ni Mume maana kamuumba mwanadamu wa kwanza kwa mfano wake, pia kunasehem kwenye ufunuo wanesema aliona mzee sijui sijakosea..
Mfalme wa Amani.
Na sio Malkia
 
Ukisoma Mwanzo Sita unaweza kuona malaika ni jinsia gani.

Biblia inasema kisha wana wa Mungu wakawaona hao binti za wanadamu ni wazuri. Wakaingia na kuwajua hao binti ya binadamu. Na hapo ndipo walipotokea Wanefili
 
Ukisoma Mwanzo Sita unaweza kuona malaika ni jinsia gani.

Biblia inasema kisha wana wa Mungu wakawaona hao binti za wanadamu ni wazuri. Wakaingia na kuwajua hao binti ya binadamu. Na hapo ndipo walipotokea Wanefili
unajua nini mkuu mie sio msomi wa Bible ila huwa napenda kusoma documentary na hata nikisoma Bible lazima nitakuwa na maswali mengi sana hivyo kuna vitu vingine huwa sipendi sana kuumiza kichwa kwani vitu vya Mungu huwa vina limits ukichunguza sana unaweza jikuta unavuna midhambi tu bila kujua.
 
Mbona nmewahi kusikia kuwa kuna majini huwa wanazaa na binadamu..?! Fatilia vipindi vya marehem mzee Yahya Hussein
katika ulimwengu wa kiroho kuna vitu vingi tusivyojua huenda hata mie nikawa na watoto wengi huko.
 
Dhambi ni Uasi wa Sheria Mkuu.

Hakuna dhambi ya kufanya utafiti.

Soma Biblia hutaogopa kuchunguza mambo.
 
Dhambi ni Uasi wa Sheria Mkuu.

Hakuna dhambi ya kufanya utafiti.

Soma Biblia hutaogopa kuchunguza mambo.
sio kwamba naogopa kusoma ila naogopa akili yangu itanipeleka mbali sana, najua vitabu vyote vya dini vinamuelezea kama mwanaume na kwa upande wingine Mungu anakuambia hafananishwi na kitu kingine chochote.
 
Allaah Anasema:

"Je! Mnamfanya yeye na kizazi chake kuwa marafiki (zenu) badala yangu hali wao ni maadui zenu? Ni mbaya kabisa kwa madhalimu badala (hii)".

Al Kahf - 50


Kauli ya Allaah katika aya hii pale aliposema 'NA KIZAZI CHAKE'. inamaanisha kwamba majini wanazaliana.
 
WAMO MIONGONI MWAO WANAWAKE NA WANAUME
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alisema:

"Anapoingia mmoja wenu chooni, basi aseme:

“Allaah najikinga kwako kutokana na majini wanaume na majini wanawake
 
MAJINI WANAKUFA?
Allaah Anasema:

"Kila kilichopo juu yake (ardhi na mbingu) kitatoweka (kitaondoka)."

Ar-Rahmaan - 26



Na Akasema:

"Hakuna aabudiwaye kwa haki ila Yeye; kila kitu kitakufa isipokuwa Yeye (Allaah basi)."

Al-Qaswas - 88


Inavyojulikana ni kwamba Iblisi yuhai mpaka siku ya Qiyaamah.

Allaah Amesema:

"Akasema (Iblisi); “Mola wangu! basi nipe nafasi (nisife) mpaka siku watakayofufuliwa (viumbe) vyote.”

Akasema (Allaah); “Hakika wewe (nimekwisha kukufanya) katika wale waliopewa nafasi.

Mpaka siku ya wakati uliowekwa (ukifika wakati huo utakufa).”

Al-Hjr - 36 -37-38
 
huyu mtu sijui ni nani ila napendaga sana threads na comments zako haswa yakija katika mambo ya ulimwengu mwingine huwa unakosha. majini ni adui zetu na vile vile majini humuogopa mwanadamu.
 
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam);

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

"Wameumbwa Malaika kwa nuru na Majini kwa ndimi za moto na Adam ameumbwa kwa mliyokwisha elezewa (Udongo)."
 
Hii ni kwa mujibu wa hadith lakin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…