Hivi Malaika huzaa na kufa pia?

Hivi Malaika huzaa na kufa pia?

Kiufupi malaika, mapepo pamoja na shetani wote ni roho, na hawazai wala hawafi. Pamoja na binadamu pia roho zetu hazifi tunakufa mwili tu. Kwenye maandiko Mungu anasema analiheshimu neno lake kuliko kitu chochote na kwenye neno amempa mwanadamu utashi wa kuchagua kufanya ila ameweka matokeo sasa kwamba ukifanya mema mwisho wako utakuwaje na endapo utafanya mabaya utakuwaje vilevile
Mbona nmewahi kusikia kuwa kuna majini huwa wanazaa na binadamu..?! Fatilia vipindi vya marehem mzee Yahya Hussein
 
Parapanda itakapolia tutafufuka katika wafu na kupewa miili mipya, kwahiyo km ulipanda dhambi utaelekea kunako hukumu yako na km ulipanda mema basi utaingia ktk mji ule mtakatifu, mji wa yerusalemu
Very imaginary, lakini poa maana kuna mambo yapo kiulimwengu wa roho zaidi ukiyatafakari ktk ulimwengu wa mwili huwezi kupata majibu yake!
 
Mbona nmewahi kusikia kuwa kuna majini huwa wanazaa na binadamu..?! Fatilia vipindi vya marehem mzee Yahya Hussein
Mmmh hapa nisubiri wajuvi!
 
dah interested question.
ninavyojua na jinsi nilivyo soma kwa upande wa malaika sio immortal creatures hufa pia ila kwa muda maarumu swala la kuwa wao wanazaliana kama sie binaadam hapana hawazaliani kwa kifupi sio wanawake wala wanaume.
Majini huzaliana na kufa pia na wanamatamanio kama binaadam tulivyo.
kama tunavyosoma kwenye hadithi nyingi baada ya shetani kumuasi Mungu aliomba awepo hai mpaka siku maalumu na kama inavyojulika shetani ni miongoni mwa majini. Hivyo nae atakufa tu muda wake ukifika.
Ukisoma Mwanzo Sita unaweza kuona malaika ni jinsia gani.

Biblia inasema kisha wana wa Mungu wakawaona hao binti za wanadamu ni wazuri. Wakaingia na kuwajua hao binti ya binadamu. Na hapo ndipo walipotokea Wanefili
 
unajua nini mkuu mie sio msomi wa Bible ila huwa napenda kusoma documentary na hata nikisoma Bible lazima nitakuwa na maswali mengi sana hivyo kuna vitu vingine huwa sipendi sana kuumiza kichwa kwani vitu vya Mungu huwa vina limits ukichunguza sana unaweza jikuta unavuna midhambi tu bila kujua.
 
Mbona nmewahi kusikia kuwa kuna majini huwa wanazaa na binadamu..?! Fatilia vipindi vya marehem mzee Yahya Hussein
katika ulimwengu wa kiroho kuna vitu vingi tusivyojua huenda hata mie nikawa na watoto wengi huko.
 
unajua nini mkuu mie sio msomi wa Bible ila huwa napenda kusoma documentary na hata nikisoma Bible lazima nitakuwa na maswali mengi sana hivyo kuna vitu vingine huwa sipendi sana kuumiza kichwa kwani vitu vya Mungu huwa vina limits ukichunguza sana unaweza jikuta unavuna midhambi tu bila kujua.
Dhambi ni Uasi wa Sheria Mkuu.

Hakuna dhambi ya kufanya utafiti.

Soma Biblia hutaogopa kuchunguza mambo.
 
Dhambi ni Uasi wa Sheria Mkuu.

Hakuna dhambi ya kufanya utafiti.

Soma Biblia hutaogopa kuchunguza mambo.
sio kwamba naogopa kusoma ila naogopa akili yangu itanipeleka mbali sana, najua vitabu vyote vya dini vinamuelezea kama mwanaume na kwa upande wingine Mungu anakuambia hafananishwi na kitu kingine chochote.
 
Allaah Anasema:

"Je! Mnamfanya yeye na kizazi chake kuwa marafiki (zenu) badala yangu hali wao ni maadui zenu? Ni mbaya kabisa kwa madhalimu badala (hii)".

Al Kahf - 50

Kauli ya Allaah katika aya hii pale aliposema 'NA KIZAZI CHAKE'. inamaanisha kwamba majini wanazaliana.
 
WAMO MIONGONI MWAO WANAWAKE NA WANAUME
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alisema:

"Anapoingia mmoja wenu chooni, basi aseme:

“Allaah najikinga kwako kutokana na majini wanaume na majini wanawake
 
MAJINI WANAKUFA?
Allaah Anasema:

"Kila kilichopo juu yake (ardhi na mbingu) kitatoweka (kitaondoka)."

Ar-Rahmaan - 26

Na Akasema:

"Hakuna aabudiwaye kwa haki ila Yeye; kila kitu kitakufa isipokuwa Yeye (Allaah basi)."

Al-Qaswas - 88

Inavyojulikana ni kwamba Iblisi yuhai mpaka siku ya Qiyaamah.

Allaah Amesema:

"Akasema (Iblisi); “Mola wangu! basi nipe nafasi (nisife) mpaka siku watakayofufuliwa (viumbe) vyote.”

Akasema (Allaah); “Hakika wewe (nimekwisha kukufanya) katika wale waliopewa nafasi.

Mpaka siku ya wakati uliowekwa (ukifika wakati huo utakufa).”

Al-Hjr - 36 -37-38
 
Allaah Anasema:

"Je! Mnamfanya yeye na kizazi chake kuwa marafiki (zenu) badala yangu hali wao ni maadui zenu? Ni mbaya kabisa kwa madhalimu badala (hii)".

Al Kahf - 50

Kauli ya Allaah katika aya hii pale aliposema 'NA KIZAZI CHAKE'. inamaanisha kwamba majini wanazaliana.
huyu mtu sijui ni nani ila napendaga sana threads na comments zako haswa yakija katika mambo ya ulimwengu mwingine huwa unakosha. majini ni adui zetu na vile vile majini humuogopa mwanadamu.
 
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam);

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

"Wameumbwa Malaika kwa nuru na Majini kwa ndimi za moto na Adam ameumbwa kwa mliyokwisha elezewa (Udongo)."
 
Malaika hawana matamanio hivyo hawawezi kuzaa
Viumbe vyote vitakufa kwani kila nafsi itaonja mauti mpaka majini na malaika pia
Malaika watakufa mwisho kabsa na malaika wa mwisho kufa ni Israel mtoa roho
Shetani yupo mpaka Leo kwa sababu Mara baada ya kufukuzwa mbinguni na kulaaniwa Aliomba awekwe duniani mpaka Siku ya kiama,

Allah akamwambia atakaa duniani mpaka wakati maalum hivi wakati wake ukifka atakufa
Nb:viumbe vyote vitaonja mauti atabaki Allah pekee kisha atamfufua malaika israfilu ili apulize parapanda la ufufuo
Hii ni kwa mujibu wa Quran
Hii ni kwa mujibu wa hadith lakin
 
Back
Top Bottom