Hivi Malaika huzaa na kufa pia?

 
Hakuna kitu Kama hicho, mkuu Malaika hawazai Hakuna kuzaliana mbinguni sijui kwa imani nyingine
 
aisee kumbe
 
Inawezekana kuitwa mwanamume ni cheo cha uongozi hasa, hivyo hata jina linakuwa likiegemea kiumeni, lakini kwa habari ya jinsia hupatikana mwilini tu. Katika ulimwengu wa kiroho hakuna jinsia sababu roho hauna jinsia ya kike au ya kiume, ni neutral. Ila ikivaa mwili ndiyo hujidhihirisha katika tabia fulani aidha ya kiume au ya kike. Ndiyo maana wakati mwingine unashangaa mwanaume akiwa na tabia za kike na mwanamke tabia za kiume! Natumaini umenielewa.
 
....Kama ni hivyo kwanini tunaitwa "wanawari" wa kristu?
 
Ukitafakari kwa makini utagundua kuwa mume au mke kimaandiko ni zaidi ya jinsia kama wengi wetu tunavyodhania katika hali ya kawaida. Kama Yeye ni mume wa wajane na baba wa yatima hamaanishi kuwa baba au mume kwa namna kama ya kibinadamu laa, anamaanisha faraja yake inaziba pengo la aliyeondoka ikiwa ni mume au baba. Katika roho ni roho na katika mwili ni mwili, usije ukachanganya, ukichanganya tu hautaelewa kamwe!
 
Pia neno bwana linamaana ya mkuu/mkubwa/kiongozi kwa upande wa mwanaume na kwa upande wa kike ni bibi. Ni kama kusema mheshimiwa.
 
Mbona nmewahi kusikia kuwa kuna majini huwa wanazaa na binadamu..?! Fatilia vipindi vya marehem mzee Yahya Hussein
Hii inatokea katika ulimwengu wa kiroho, maana bunadamu naye ni roho anayeishi katika mwili wa damu na nyama wakati hao wengineo ni roho kamili wakiwa na miili yaoya kiroho ndiyo maana unaweza kuwaona vile walivyo katika ulimwengu wa kiroho. Haya mambo ni tata sana wakati mwingine
 
Ahsante, kwa roho zetu zina ukamilifu wa Mwenyezi Mungu! Hukumu itakuwa juu ya nini kwa viumbe? Au huko tutavalishwa miili mingine yenye sense organs ambazo zitatupa amani na furaha ktk pepo na uchungu na maumivu ktk kuzimu?
Kama kulivyo na ulimwengu wa nyama, vivyo hivyo na ulimwengu wa roho ulivyo, roho zinaweza kuwa na utashi wake zenyewe bila kutegemea mwili na bila shaka hata adhabu roho zinaweza zikapeana vilevile
Kwasababu wote tutakuwa ni roho sasa, hata adhabu zitakuwa za kiroho, furaha ya aina ya kiroho, na hata kama kuna moto wa jehanum hautakuw wa namna hii ya kimwili, maana moto wa duniani hauwez kuchoma roho
Note: Wakati wa ndoto za usiku huwa unaweza ukaumizwa kwenye ndoto na ukasikia maumivu kabisa lakin kumbe ni ndoto tu, sasa uchukulie mfano huo kulata picha ya maisha ya kiroho yatavyokuwa

G.Man
 

Hayo maumivu unayapata kwenye roho au kwenye mwili?
Roho ni nini?
Je roho inaweza ku-exist pasipo kuwa na mwili?
 
Hayo maumivu unayapata kwenye roho au kwenye mwili?
Roho ni nini?
Je roho inaweza ku-exist pasipo kuwa na mwili?
Maumivu ya kwenye ndoto huwa hayapatikan kwny mwili mkuu, huo ni mfano tu wa namna roho inaweza ikapitia challenges mbali mbali bila kuwa na mwili.
Roho ni mfano wa nafsi inayojitegemea kimikakati, lakini haiwezi kuonekana kwa namna ya kimwili. Ndo maana mapepo ili kutimiza azma za kimwili huwa inawalazimu kuwa ndani ya mtu kwanz ndo wakamilishe mission
Note: Nafkir maelezo yang yatakuw yana base zaid kwa watu ambao wanaamini kuhus uwepo wa Mungu na roho nyingine ambay msingi wa maelezo yake ni kweny maandiko matakatifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…