Hivi Malaika huzaa na kufa pia?

Hivi Malaika huzaa na kufa pia?

Kiufupi malaika, mapepo pamoja na shetani wote ni roho, na hawazai wala hawafi. Pamoja na binadamu pia roho zetu hazifi tunakufa mwili tu. Kwenye maandiko Mungu anasema analiheshimu neno lake kuliko kitu chochote na kwenye neno amempa mwanadamu utashi wa kuchagua kufanya ila ameweka matokeo sasa kwamba ukifanya mema mwisho wako utakuwaje na endapo utafanya mabaya utakuwaje vilevile... Sasa hawezi tena kuja kukuingilia kufanya maamuzi japo anao uwezo huo
 
Hakuna kitu Kama hicho, mkuu Malaika hawazai Hakuna kuzaliana mbinguni sijui kwa imani nyingine
 
Malaika hawana matamanio hivyo hawawezi kuzaa
Viumbe vyote vitakufa kwani kila nafsi itaonja mauti mpaka majini na malaika pia
Malaika watakufa mwisho kabsa na malaika wa mwisho kufa ni Israel mtoa roho
Shetani yupo mpaka Leo kwa sababu Mara baada ya kufukuzwa mbinguni na kulaaniwa Aliomba awekwe duniani mpaka Siku ya kiama,

Allah akamwambia atakaa duniani mpaka wakati maalum hivi wakati wake ukifka atakufa
Nb:viumbe vyote vitaonja mauti atabaki Allah pekee kisha atamfufua malaika israfilu ili apulize parapanda la ufufuo
Hii ni kwa mujibu wa Quran
aisee kumbe
 
Malaika wote ni wanaume ndio maana majina yao ni ya kiume.
Ref
Gabriel
Michaeli
Jinsia ya kike iliumbwa ktk mwili wa kibinadamu tu ili mtu mume Adamu apate msaidizi.
Kabla ya hapo hakukuwepo na jinsia ya kike.
Hata Shetani Lucifer ni mwanamume.
Mungu Muumba Mbingu na Nchi ni Mwanamume.
Ref
Baba yetu uliye Mbinguni.
Inawezekana kuitwa mwanamume ni cheo cha uongozi hasa, hivyo hata jina linakuwa likiegemea kiumeni, lakini kwa habari ya jinsia hupatikana mwilini tu. Katika ulimwengu wa kiroho hakuna jinsia sababu roho hauna jinsia ya kike au ya kiume, ni neutral. Ila ikivaa mwili ndiyo hujidhihirisha katika tabia fulani aidha ya kiume au ya kike. Ndiyo maana wakati mwingine unashangaa mwanaume akiwa na tabia za kike na mwanamke tabia za kiume! Natumaini umenielewa.
 
Malaika wote ni wanaume ndio maana majina yao ni ya kiume.
Ref
Gabriel
Michaeli
Jinsia ya kike iliumbwa ktk mwili wa kibinadamu tu ili mtu mume Adamu apate msaidizi.
Kabla ya hapo hakukuwepo na jinsia ya kike.
Hata Shetani Lucifer ni mwanamume.
Mungu Muumba Mbingu na Nchi ni Mwanamume.
Ref
Baba yetu uliye Mbinguni.
....Kama ni hivyo kwanini tunaitwa "wanawari" wa kristu?
 
Ninachojua mkuu, Mungu amejitambulisha sehemu nyingi kama, Mungu Mume.

Mfano
Yeremia 3 : 14
" Rudini enyi watoto wenye kuasi, asema Bwana, maana mimi ni mume kwenu "

Isaya 54 : 5
" Kwasababu muumba wako ni mume wako, Bwana wa majeshi ndiye jina lake, na mtakatifu wa Israeli ndiye ukombozi wako, yeye ataitwa Mungu wa dunia yote "

Neno " Bwana " pia linawakilisha jinsia ya kiume.
Kinyume chake ni neno " Bibi "
Ukitafakari kwa makini utagundua kuwa mume au mke kimaandiko ni zaidi ya jinsia kama wengi wetu tunavyodhania katika hali ya kawaida. Kama Yeye ni mume wa wajane na baba wa yatima hamaanishi kuwa baba au mume kwa namna kama ya kibinadamu laa, anamaanisha faraja yake inaziba pengo la aliyeondoka ikiwa ni mume au baba. Katika roho ni roho na katika mwili ni mwili, usije ukachanganya, ukichanganya tu hautaelewa kamwe!
 
Ninachojua mkuu, Mungu amejitambulisha sehemu nyingi kama, Mungu Mume.

Mfano
Yeremia 3 : 14
" Rudini enyi watoto wenye kuasi, asema Bwana, maana mimi ni mume kwenu "

Isaya 54 : 5
" Kwasababu muumba wako ni mume wako, Bwana wa majeshi ndiye jina lake, na mtakatifu wa Israeli ndiye ukombozi wako, yeye ataitwa Mungu wa dunia yote "

Neno " Bwana " pia linawakilisha jinsia ya kiume.
Kinyume chake ni neno " Bibi "
Pia neno bwana linamaana ya mkuu/mkubwa/kiongozi kwa upande wa mwanaume na kwa upande wa kike ni bibi. Ni kama kusema mheshimiwa.
 
Mbona nmewahi kusikia kuwa kuna majini huwa wanazaa na binadamu..?! Fatilia vipindi vya marehem mzee Yahya Hussein
Hii inatokea katika ulimwengu wa kiroho, maana bunadamu naye ni roho anayeishi katika mwili wa damu na nyama wakati hao wengineo ni roho kamili wakiwa na miili yaoya kiroho ndiyo maana unaweza kuwaona vile walivyo katika ulimwengu wa kiroho. Haya mambo ni tata sana wakati mwingine
 
Ahsante, kwa roho zetu zina ukamilifu wa Mwenyezi Mungu! Hukumu itakuwa juu ya nini kwa viumbe? Au huko tutavalishwa miili mingine yenye sense organs ambazo zitatupa amani na furaha ktk pepo na uchungu na maumivu ktk kuzimu?
Kama kulivyo na ulimwengu wa nyama, vivyo hivyo na ulimwengu wa roho ulivyo, roho zinaweza kuwa na utashi wake zenyewe bila kutegemea mwili na bila shaka hata adhabu roho zinaweza zikapeana vilevile
Kwasababu wote tutakuwa ni roho sasa, hata adhabu zitakuwa za kiroho, furaha ya aina ya kiroho, na hata kama kuna moto wa jehanum hautakuw wa namna hii ya kimwili, maana moto wa duniani hauwez kuchoma roho
Note: Wakati wa ndoto za usiku huwa unaweza ukaumizwa kwenye ndoto na ukasikia maumivu kabisa lakin kumbe ni ndoto tu, sasa uchukulie mfano huo kulata picha ya maisha ya kiroho yatavyokuwa

G.Man
 
Hayo maumivu unayapata kwenye roho au kwenye mwili?
Roho ni nini?
Je roho inaweza ku-exist pasipo kuwa na mwili?
 
Hayo maumivu unayapata kwenye roho au kwenye mwili?
Roho ni nini?
Je roho inaweza ku-exist pasipo kuwa na mwili?
Maumivu ya kwenye ndoto huwa hayapatikan kwny mwili mkuu, huo ni mfano tu wa namna roho inaweza ikapitia challenges mbali mbali bila kuwa na mwili.
Roho ni mfano wa nafsi inayojitegemea kimikakati, lakini haiwezi kuonekana kwa namna ya kimwili. Ndo maana mapepo ili kutimiza azma za kimwili huwa inawalazimu kuwa ndani ya mtu kwanz ndo wakamilishe mission
Note: Nafkir maelezo yang yatakuw yana base zaid kwa watu ambao wanaamini kuhus uwepo wa Mungu na roho nyingine ambay msingi wa maelezo yake ni kweny maandiko matakatifu
 
Back
Top Bottom