ZNM
JF-Expert Member
- Dec 16, 2015
- 1,219
- 1,280
Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya tele wakuu!
Katika tafakari zangu za huku na kule ktk masuala ya imani ya dini, inaonekana ni Mwenyezi Mungu pekee ndiye mkamilifu kwa maana ya kuwa kwetu viumbe hatujui mwanzo na hatujui mwisho wake! Hakuumbwa na hatakufa, na kwamba Mwenyezi Mungu ni wa Milele yote ijayo! Tena hapana kiumbe kingine cha kufananishwa nae!
Sasa, mimi sina tatizo na hilo, ninachotaka kujua leo ni hili la malaika ama mapepo, hivi nao huzaa na kufa? Kama huzaa, huzaa kwa njia gani? Kama hufa, hufa kwa namna gani?
Mbona huyu kiumbe yeye tangu tuanze kusikia habari zake yeye hakuwahi kufa mpaka leo? Wanamuita Shetwani/shetani! Huyu kiumbe ktk vitabu vya dini anapewa mamlaka kubwa sana! Anapewa ushindani mkubwa wa Mwenyezi Mungu na kwamba kwa Mwenyezi Mungu kuwapenda viumbe vyake, basi amekuwa akishusha manabii na mitume yake kulingana na umma wa nyakati zake ili kuwanusuru viumbe vyake na mwovu shetwani/shetani!
Kama malaika na mapepo wana ukomo kama viumbe vingine, mbona huyu kiumbe shetwani/shetani anaishi kwa muda mrefu namna hii? Ni mpango wa Mungu shetwani/shetani kuendelea kuwarubuni/kuwashawishi viumbe wa Mungu kuangamia mwisho wa Dunia katika ile hukumu ya haki?
Kila nikitafakari, nashangaa sana, viumbe vikikoma uhai hapa duniani kumekuwa na msemo, tulikupenda ila Mwenyezi Mungu kakupenda zaidi! Kwa nini Mwenyezi Mungu hajampenda zaidi Shetwani/shetani? Ona sasa mwishowe nafika mbali, samahani imeandikwa, Mwenyezi Mungu hachunguziki kwa akili za kibinadamu ila kwa angalau wenye uelewa naomba mshiriki kunipa elimu kidogo!
Nawasilisha!