Hivi Malaika huzaa na kufa pia?

Hivi Malaika huzaa na kufa pia?

ZNM

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2015
Posts
1,219
Reaction score
1,280
Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya tele wakuu!

Katika tafakari zangu za huku na kule ktk masuala ya imani ya dini, inaonekana ni Mwenyezi Mungu pekee ndiye mkamilifu kwa maana ya kuwa kwetu viumbe hatujui mwanzo na hatujui mwisho wake! Hakuumbwa na hatakufa, na kwamba Mwenyezi Mungu ni wa Milele yote ijayo! Tena hapana kiumbe kingine cha kufananishwa nae!

Sasa, mimi sina tatizo na hilo, ninachotaka kujua leo ni hili la malaika ama mapepo, hivi nao huzaa na kufa? Kama huzaa, huzaa kwa njia gani? Kama hufa, hufa kwa namna gani?

Mbona huyu kiumbe yeye tangu tuanze kusikia habari zake yeye hakuwahi kufa mpaka leo? Wanamuita Shetwani/shetani! Huyu kiumbe ktk vitabu vya dini anapewa mamlaka kubwa sana! Anapewa ushindani mkubwa wa Mwenyezi Mungu na kwamba kwa Mwenyezi Mungu kuwapenda viumbe vyake, basi amekuwa akishusha manabii na mitume yake kulingana na umma wa nyakati zake ili kuwanusuru viumbe vyake na mwovu shetwani/shetani!

Kama malaika na mapepo wana ukomo kama viumbe vingine, mbona huyu kiumbe shetwani/shetani anaishi kwa muda mrefu namna hii? Ni mpango wa Mungu shetwani/shetani kuendelea kuwarubuni/kuwashawishi viumbe wa Mungu kuangamia mwisho wa Dunia katika ile hukumu ya haki?

Kila nikitafakari, nashangaa sana, viumbe vikikoma uhai hapa duniani kumekuwa na msemo, tulikupenda ila Mwenyezi Mungu kakupenda zaidi! Kwa nini Mwenyezi Mungu hajampenda zaidi Shetwani/shetani? Ona sasa mwishowe nafika mbali, samahani imeandikwa, Mwenyezi Mungu hachunguziki kwa akili za kibinadamu ila kwa angalau wenye uelewa naomba mshiriki kunipa elimu kidogo!

Nawasilisha!
 
Kiufupi malaika, mapepo pamoja na shetani wote ni roho, na hawazai wala hawafi. Pamoja na binadamu pia roho zetu hazifi tunakufa mwili tu. Kwenye maandiko Mungu anasema analiheshimu neno lake kuliko kitu chochote na kwenye neno amempa mwanadamu utashi wa kuchagua kufanya ila ameweka matokeo sasa kwamba ukifanya mema mwisho wako utakuwaje na endapo utafanya mabaya utakuwaje vilevile... Sasa hawezi tena kuja kukuingilia kufanya maamuzi japo anao uwezo huo
 
Kiufupi malaika, mapepo pamoja na shetani wote ni roho, na hawazai wala hawafi. Pamoja na binadamu pia roho zetu hazifi tunakufa mwili tu. Kwenye maandiko Mungu anasema analiheshimu neno lake kuliko kitu chochote na kwenye neno amempa mwanadamu utashi wa kuchagua kufanya ila ameweka matokeo sasa kwamba ukifanya mema mwisho wako utakuwaje na endapo utafanya mabaya utakuwaje vilevile
Ahsante, kwa roho zetu zina ukamilifu wa Mwenyezi Mungu! Hukumu itakuwa juu ya nini kwa viumbe? Au huko tutavalishwa miili mingine yenye sense organs ambazo zitatupa amani na furaha ktk pepo na uchungu na maumivu ktk kuzimu?
 
Malaika hawana matamanio hivyo hawawezi kuzaa
Viumbe vyote vitakufa kwani kila nafsi itaonja mauti mpaka majini na malaika pia
Malaika watakufa mwisho kabsa na malaika wa mwisho kufa ni Israel mtoa roho
Shetani yupo mpaka Leo kwa sababu Mara baada ya kufukuzwa mbinguni na kulaaniwa Aliomba awekwe duniani mpaka Siku ya kiama,

Allah akamwambia atakaa duniani mpaka wakati maalum hivi wakati wake ukifka atakufa
Nb:viumbe vyote vitaonja mauti atabaki Allah pekee kisha atamfufua malaika israfilu ili apulize parapanda la ufufuo
Hii ni kwa mujibu wa Quran
 
Ahsante, kwa roho zetu zina ukamilifu wa Mwenyezi Mungu! Hukumu itakuwa juu ya nini kwa viumbe? Au huko tutavalishwa miili mingine yenye sense organs ambazo zitatupa amani na furaha ktk pepo na uchungu na maumivu ktk kuzimu?
kwa.wakristo tunaamini baada ya huu mwili huu wa nyama uharibikao tutafufuliwa katika mwili usio haribika na hiyo ni katika ulimwengu wa roho na hata hiyo pepo na jehanam viko katika ulimwengu wa roho na ndio maana mpaka kesho hakuna mwanasayansi aliye fanikiwa kufika mbinguni au jeham
 
Inategemea wewe u dini/imani ipi.
Malaika hawana jinsia..
Hawawezi kuzaa.
Malaika wote ni wanaume ndio maana majina yao ni ya kiume.
Ref
Gabriel
Michaeli
Jinsia ya kike iliumbwa ktk mwili wa kibinadamu tu ili mtu mume Adamu apate msaidizi.
Kabla ya hapo hakukuwepo na jinsia ya kike.
Hata Shetani Lucifer ni mwanamume.
Mungu Muumba Mbingu na Nchi ni Mwanamume.
Ref
Baba yetu uliye Mbinguni.
 
Malaika ni roho hivyo roho haizai wala haifi, tulifundishwa hivyo. Labda wewe ujiongeze ni kweli? (pure imagination) jua tu kwa binadamu kuna kuzaliwa na kufa, mwanzo wa vyote hatujui, basi hutajua habari za malaika. Dini zipo tu ili utambue Mungu yupo japo haonekani, ukishakua na hofu inakuzuia kufanya ubaya. Chapa kazi kwa kujua jema na baya Mungu wako unamjua mwenyewe. Jaribu kuuliza Theologians, kama wana jibu kinalofanana na ukweli
 
dah interested question.
ninavyojua na jinsi nilivyo soma kwa upande wa malaika sio immortal creatures hufa pia ila kwa muda maarumu swala la kuwa wao wanazaliana kama sie binaadam hapana hawazaliani kwa kifupi sio wanawake wala wanaume.
Majini huzaliana na kufa pia na wanamatamanio kama binaadam tulivyo.
kama tunavyosoma kwenye hadithi nyingi baada ya shetani kumuasi Mungu aliomba awepo hai mpaka siku maalumu na kama inavyojulika shetani ni miongoni mwa majini. Hivyo nae atakufa tu muda wake ukifika.
 
Ndyo huzaa na kufa mfano mkeo wakati unamtongoza lazima umempe cheo cha umalaika[emoji23]
 
Malaika wote ni wanaume ndio maana majina yao ni ya kiume.
Ref
Gabriel
Michaeli
Jinsia ya kike iliumbwa ktk mwili wa kibinadamu tu ili mtu mume Adamu apate msaidizi.
Kabla ya hapo hakukuwepo na jinsia ya kike.
Hata Shetani Lucifer ni mwanamume.
Mungu Muumba Mbingu na Nchi ni Mwanamume.
Ref
Baba yetu uliye Mbinguni.
U-Mungu hauna Jinsia
 
U-Mungu hauna Jinsia
Ninachojua mkuu, Mungu amejitambulisha sehemu nyingi kama, Mungu Mume.

Mfano
Yeremia 3 : 14
" Rudini enyi watoto wenye kuasi, asema Bwana, maana mimi ni mume kwenu "

Isaya 54 : 5
" Kwasababu muumba wako ni mume wako, Bwana wa majeshi ndiye jina lake, na mtakatifu wa Israeli ndiye ukombozi wako, yeye ataitwa Mungu wa dunia yote "

Neno " Bwana " pia linawakilisha jinsia ya kiume.
Kinyume chake ni neno " Bibi "
 
Hiyo alisema tu,
Lakini Biologically tunajua namna ya kutofautisha ME na KE,
Sasa wewe niambie, Mungu ana sifa zipi za Kibaolojia kuitwa ME
 
Hiyo alisema tu,
Lakini Biologically tunajua namna ya kutofautisha ME na KE,
Sasa wewe niambie, Mungu ana sifa zipi za Kibaolojia kuitwa ME
Mfalme wa Ulimwengu.
Na sio Malkia.
 
Ahsante, kwa roho zetu zina ukamilifu wa Mwenyezi Mungu! Hukumu itakuwa juu ya nini kwa viumbe? Au huko tutavalishwa miili mingine yenye sense organs ambazo zitatupa amani na furaha ktk pepo na uchungu na maumivu ktk kuzimu?
Parapanda itakapolia tutafufuka katika wafu na kupewa miili mipya, kwahiyo km ulipanda dhambi utaelekea kunako hukumu yako na km ulipanda mema basi utaingia ktk mji ule mtakatifu, mji wa yerusalemu
 
Back
Top Bottom