Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 12,658
- 16,205
Hadithi ni masimulizi ya kubuni au ya kutunga. Sio masomulizi ya ukweli, ni ya sanaa ya kubuni.Hata biblia ni kitabu cha hadithi pia, Kwa maana Ulimwengu ndio uliyoanza kuwepo kwanza na watu walikuwa wakiishi kama kawaida ndipo baadae zikafuatia hizi simulizi (vitabu vya kidini) Kutoka kwenye kuumbwa kwa ulimwengu hadi kuandikwa kwa biblia kuna miaka mingapi imepita?
Mfano.
Hadithi za Abuniwasi
Au Hadithi za Alfu Lela U Lela.
Shigongo ni mtumzi mzuri wa hadithi hapa Tanzania.
Hadithi yake moja inasema
" Raisi Anapenda Mke Wangu"
Tofautisha vitabu vya hadithi na vya historia.
Historia, ni masimulizi ya ukweli yaliyotokea Zamani.
Kwa mfano
Tanzania na Uganda walipigana vita mwaka Sabini na nane 1978.
Tanzania ilishinda vita hivyo na Raisi wa Uganda Iddi Amini alikimbilia uhamoshoni.
Biblia haijaandika Hadithi labda kama inatumika kama mfano wa kufundishia.
Biblia imeandika historia ya ukweli ya Uumbaji wa Ulimwengu na vyoote vilivyomo.
Biblia pia inaandika Historia ya Binadamu kuanzi Adamu hadi kizazi cha sasa.
Hivyo basi Biblia sio kitabu cha hadithi bali ni cha Historia ya ukweli ya chanzo cha kila kitu kilichopo leo.