"... Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka. ..."
ISAYA 6:2
"Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko , kuilinda njia ya mti wa uzima." MWANZO 3:24.
"... na juu yake Makerubi ya utukufu, yakikitia kivuli kiti cha rehema; ..."
WAEBRANIA 9:5.
Malaika wako madaraja mbalimbali. Daraja la juu kabisa la malaika ni Maserafi na Makerubi. Hawa ndio wako karibu kabisa na Kiti cha Enzi cha Mungu. Wamekizunguka kiti hichi.
Kuna malaika wengine wengi wasio na idadi wakifanya shughuli mbalimbali za kusujudu na utumishi. Kwa mfano kwenye Kitabu cha Waebrania malaika wameelezwa hivi: "Je, Hao wote si roho watumikao, waitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?" WAEBRANIA 1:14.
Malaika ni viumbe wa kiroho. Hawana umbo maalumu (ambalo halibadiliki) wanaweza wakavaa mwili wowote. Mfano kuna malaika wawili walitumwa kwa ajili ya kuchoma Sodoma na Gomora, hawa walikuwa na umbile la mwanadamu kabisa. Hawakuwa na mabawa. (SOMA KITABU CHA MWANZO 19:1-22.)
Ndugu zangu, mambo ya rohoni hujulikana kwa namna ya rohoni. Akili ya mwanadamu haiwezi kuyajua mambo ya rohoni. Ni lazima tuwe rohoni ili tuyaone na kuyajua ya rohoni. Hatua ya kwanza ya kuishi maisha ya rohoni ni KUMPA YESU MAISHA YAKO, ILI AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO. Huku huitwa kuzaliwa mara ya pili. Hapa ndipo mtu huanza kuongozwa na Roho wa Mungu ambapo huanza kufunuliwa na Roho Mtakatifu mambo ya ndani sana ya Mungu. Hata mafumbo ya Mungu.
"Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu"
1WAKORINTHO 2:10.
hakika YESU NI MWOKOZI.