Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kujiamini kwa kupitiliza kwa Marekani na Israel ndiko kunakokaribisha chuki kutoka kila upande duniani.Huwa wanafanya kile kisichopendeza kwa wenzao na wakifanyiwa wao inakuwa ni nongwa kubwa.
Raisi Biden tangu siku ya mwanzo bila kupata picha kamili ya vita vilipoanza akasema Israel inastahiki kujilinda full stop.
Baada ya hapo wamepeleka meli za kubeba ndege za kivita kwenye bahari ya Mediterranean.Ndege za mizigo tangu siku ya mwanzo zimekuwa zikipeleka shehena za silaha Israel.
Leo tena Antony Blinken ameizuru Israel na kufanya mazungumzo na Netanyahu na baadae kutoka kwenye press conference kutoa matamko.
Katika tamko lake Blinken ameeleza masikitiko yake makubwa na kutoa hisroria ya wazazi wake aliosema wametokea eneo hilo na katikati ya hotuba yake akatokwa na machozi.
Waislamu watatafsiri vipi machozi yake hayo wakati wapalestina wameshauliwa kwa malaki huko nyuma na hayo hayakumuuma.Wakati akitoa hotuba yake mauwaji yalikuwa yakiendelea Gaza ya hao hao wanawake na watoto wasio na silaha.
Kwa upande mwengine watu wenye kuwaonea huruma Hamas na wapalestina kwa ujumla wamekuwa ni watu wengi maarufu mmoja momoja na viongozi wachache nchi.Hakuna miongoni mwa majirani za Palestina na ndugu zao waislamu walioonekana kuwa na moyo wa huruma kama ule wa Marekani.Wanaacha waluliwe bila kuhoji na bila matamko.
Kwa ujumla naona kujiamini kwao na kibri cha kumiliki silaha kunawasahaulisha kwamba wanacheza na binadamu wenzao.Kilichompata kule Afghanistan na kule Ukraine inaonekana hawajapata fundisho la kutosha.