Hivi mashabiki wa mpira huwa mnashabikia nini haswa?

Apo ndo ujue binadamu ni kama ndondocha mchezaji anahama yeye kabaki pale pale,[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mkuu hicho kitu huwezi kukielezea ni sawa tu na inavyotokea unampenda mwanamke flan haijalishi Leo kavaa nguo gani
Sio kweli ,huwezi kumpenda mwanamke bila sababu, lazima kuna kitu kitakuwa kimekuvutia mfano umbo lake ,makalio,macho,ongea yake, tembea yake , Tania yake nk.
 
Mpira ni mchezo, siyo kitu serious. Ukifuatilia kwa makini unaweza ukaona kama ni uchizi fulani hivi, watu 22 wanakimbiza mpira mmoja wakati kuna mipira mingine iko nje. Kwa kutumia akili kubwa ni uchizi fulani hivi ila imeleta fursa na watu wamejenga investment na ajira ziko kwa wachezaji na wasimamizi wa shughuli yote nzima ya huo mchezo. Basically, sina muda wa kuangalia mpira wote, naangalia magoli tu, nahisi navutiwa na basketball kwasababu kila baada ya muda mfupi kuna goli linaingia so unafurahisha. Mkuu umeongea kitu cha msingi sana, fikirishi.
 
Watu mpaka wanatoana roho kisa mpira.
 
mtoa mada kwani wewe unavyopenda ngono, unapenda nini haswa? 😑😑😑
 
Mwanaume kamili lazima awe mshabiki wa mpira au mcheza mpira
Swali kwako
Nipe faida tano za Ubuyu
 
Kwani mtu anapopenda nyekundu, mwingine bluu, mwingine zambarau anapenda kwa sababu gani? Mwingine anapenda mwanamke mweupe, mwingine mweusi, mwingine "chura" mwingine "ki-portable" unadhani ni kwa nini? Ukishapata jibu ndipo utajua ni kwa nini mimi ni mpenzi wa Man U
 
Ukitoa ule mchezo pendwa wa gizani, mpira ni no 2 duniani kwa kuwa na washabiki wengi, usiniulize kwanini[emoji87]
 
Umeelewa swali lakini?
 
Toa sababu za kupenda mpira ndio hoja iliyopo mezani kwa sasa.
Sababu kama zifuatazo
1:kukutana na marafiki baada ya kazi

2:kupumzisha akili baada ya kazi

3: kujifunza mawili matatu (hapa ina wahusu wacheza mpira
Usisahau swali langu
Nipe faida za Ubuyu kwa mwanaume
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…