Hivi maslahi ya Tanganyika kwenye Muungano na Zanzibar yanatetewaga na nani?

Hivi maslahi ya Tanganyika kwenye Muungano na Zanzibar yanatetewaga na nani?

Kwa sasa maslahi ya Tanganyika yanatetewa na Mpina, Lissu na Dr Slaa. Yanahujumiwa na Nape, Machawa na hii CCM na SSH.
Hao uliowataja sii watetezi wa Tanganyika hao wote wamekuwa watetezi wazuri sana wa Zanzibar namkumbuka sana mbunge wa zamani wa Nkasi nadhani ni ndugu Ally Kesi
 
Kwani nimesema uongo ndugu yangu?
Bado najaribu kutafuta angle nzuri ili nikuelewe. Labda ufafanue zaidi maana naona wazanzibari kanchi kadogo hakazidi hata watu million lakini kametoa rais wa nchi yenye watu milioni zaidi ya hamsini mara mbili, sasa hata kama ni mume mjeda sio mume bwege kweli!?

Siku hizi kuna vyama pia vya kutetea haki za wanaume Tanganyika tungeenda huko basi.
 
Unajua mke anaweza kuonekana ana mamlaka na sauti ila ni katika mambo ambayo mume ameruhusu. Mfano, akiwa anatandika kitanda anaweza kutoa maelekezo kwa mume akakae sebuleni na mume akatii.

Kule kwa ndugu zetu, ukileta ujuaji kujaribu kuigusa hii ndoa nini kinatokea? Unatulizwa kwa mamlaka ya jeshi lipi? Tanganyika ipo salama, wala haiburuzwi. Hata mashemeji zetu majirani wanaelewa kuwa Tanganyika ni mwanaume wa aina gani.
 
Wanaosema Zanzibar inapunjwa wachunguzwe akili Zao kidogo, maana kuna vitu vya dhairi Zanzibar wananufaika kuliko Tanganyika, Kwamfano Mzanzibar anaweza kuwa rais wa jamuhuri Ila mtanganyia Kwa Zanzibar haiwezekani, pia tumewaona wazanzibar wengi Tu huku Bara wanamiliki ardhi tena na maeneo makubwa Tu Ila Kwa mtanganyika Kwa Zanzibar haiwezekani .
 
Muungano huu ni wa ovyo sana,ebu jiulize hivi leo hii kama kuna jambo la kujadili baina ya pande mbili za Muungano kupitia viongozi wakuu wa pande zote mbili je Rais wa Zanzibar anakutana na nani kujadili? Au ndiyo anakutana na Mzanzibari mwenzake tunayemuita Rais wa Jamhuri ya Muungano?
 
Kwa wakati ule na mazingira Yale ilikuwa ni sahihi Ila kwa Sasa Tanganyika inabidi isimame Kama nchi huru.

tufahamishe uwo ushihi mkuu, Kushiriki kikamilifu katika machafuko ya nchi jirani pamoja na kutumia ulagahai wa kuunganisha nchi ni usahihi? huhisi kama hayo matatizo tulionayo sasa yanatokana direct na uo ushihi unaousema?
 
Wanaosema Zanzibar inapunjwa wachunguzwe akili Zao kidogo, maana kuna vitu vya dhairi Zanzibar wananufaika kuliko Tanganyika, Kwamfano Mzanzibar anaweza kuwa rais wa jamuhuri Ila mtanganyia Kwa Zanzibar haiwezekani, pia tumewaona wazanzibar wengi Tu huku Bara wanamiliki ardhi tena na maeneo makubwa Tu Ila Kwa mtanganyika Kwa Zanzibar haiwezekani .

Kwa hio kwa upeo wako hizo ndio umeziona faida sahihi za Muungano?
 
Unajua mke anaweza kuonekana ana mamlaka na sauti ila ni katika mambo ambayo mume ameruhusu. Mfano, akiwa anatandika kitanda anaweza kutoa maelekezo kwa mume akakae sebuleni na mume akatii.

Kule kwa ndugu zetu, ukileta ujuaji kujaribu kuigusa hii ndoa nini kinatokea? Unatulizwa kwa mamlaka ya jeshi lipi? Tanganyika ipo salama, wala haiburuzwi. Hata mashemeji zetu majirani wanaelewa kuwa Tanganyika ni mwanaume wa aina gani.
Ila we jamaa una vituko sana na huu mfano wako!!
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Nimekua nikifuatilia mijadala mingi sana ya viongozi wetu, na kugundua kwamba tofauti na watanganyika, wenzetu wazanzibari wote kwa pamoja
wako macho sana kuhusu maslahi yao ndani ya muungano.

Kibaya zaidi ni kwamba kwa huku bara hata wale wa mrengo wa upinzani wanasisitiza tu kwamba eti Zanzibar inanyonywa na Tanganyika kwenye huu muungano.

Hofu yangu ni kwamba huku kulialia kwa wazanzibari kwamba wanapunjwa kwenye muungano kutatufanya watanganyika tunyonywe sana kwa kujifanya tunajibu hoja.
hakuna siku nitafurahi kama muungano ukivunjika.
 
Wanaosema Zanzibar inapunjwa wachunguzwe akili Zao kidogo, maana kuna vitu vya dhairi Zanzibar wananufaika kuliko Tanganyika, Kwamfano Mzanzibar anaweza kuwa rais wa jamuhuri Ila mtanganyia Kwa Zanzibar haiwezekani, pia tumewaona wazanzibar wengi Tu huku Bara wanamiliki ardhi tena na maeneo makubwa Tu Ila Kwa mtanganyika Kwa Zanzibar haiwezekani .
Wewe inaonyesha hata hujui kama kuna mamlaka mbili
 
Kiongozi, kwanza naona unataka kuchepusha mada, hii sio sawa.
Pili, hakuna rekodi rasmi zinazoonesha kwama serikali ya Tanganyika ilihusika kwenye mapinduzi ya 1964. Mapinduzi yale yaliratibiwa na kutekelezwa na wanachama wa ASP.
Tatu, maslahi ya Tanganyika kufanya muungano na Zanzibar yalikuwa ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia...na hapa maslahi yenyewe (ya kufikirika) yalikua juu ya usalama wa Tanganyika, kuendeleza dhana ya umajumui wa Afrika n.k
Sio kweli,nenda kasome nyaraka za shirika la ujasusi la marekani,tafuta pia madokezo ya balozi wa marekani nchini kenya jasusi Frank kaurus,Tanzania hatuna tishio lolote kutoka zanzibar hata kama itajitenga,ila Tanganyika iko pale kulinda mapinduzi ya asp ya mwaka 1964,ueleweke kuwa waliokuwa wanatawala hivyo visiwa ni watu wa pemba wenye asili ya Omani.hata sultan jamshid aliyepinduliwa alikuwa ni mtu wa pemba. Unguja ni watu wa asili ya bara,na ndio waliongoza hayo mapinduzi,makuli na wapagazi kutoka bara wskiongozwa na tito okello kutoka Uganda. Ndio maana kulikuwa na maelekezo yasiyo rasmi ya mtu kutoka pemba asiruhuswe kutawala zanzibar.hivyo,aliyekuwa mtawala wa visiwa vya zanzibar ambaye ni mpemba leo ndio mtawaliwa na watu kutoka unguja,wa bara. Ushahidi ni kwenye suala la muungano,wa pemba hawautaki muungano,lkn unguja wana utaka muungano.siku muungano ukivunjika,unguja na pemba kutawaka moto.
 
Hao uliowataja sii watetezi wa Tanganyika hao wote wamekuwa watetezi wazuri sana wa Zanzibar namkumbuka sana mbunge wa zamani wa Nkasi nadhani ni ndugu Ally Kesi

Kwa sasa hivi, leo hii ndio watetezi wakuu. Wananyoosha maelezo. Ishu muhimu kama Bandari, kuuzwa misitu, kutimulia Wamasai na kuuzwa Ngorongoro, katiba mpya, mfumuko wa bei, ufisadi mkubwa na ubadhirifu kwenye SGR, bwawa ka Nyerere wamepaza sauti na kuwakilisha sauti za Watanganyika milioni 58.
 
Back
Top Bottom