Hivi Mbeya ni Tanzania? Nimekuta Vumbi la kutisha kama Jehanamu. Narudi Iringa

ChoiceVariable na Stuxnet watalia kwa uchungu sana wakiona post yako.
Mbeya haikwepeki ni kama maji tu, usipoyanywa utayaoga. Usipoyaoga utayajengea nyumba na usipoyajengea utayatumia kama njia ya usafiri.

Mbeya ni nchi ndani ya nchi, tunaweza kujitenga dhidi ya Tanzania maana:- Airport tunayo, Barabara kuu tunayo, University ya Serikali na ya Kanisa tunazo. Nchi jirani za kupakana nazo tunazo.

Chakula na mazao ya biashara yapo madini yapo ma watu wa huku wana akili na wachapa kazi
 

Volcanic ash hiyo babuuu...

Mbeya, Chuga na Moshi nadhani ndio maeneo yanaongoza kuwa na vumbi laini sababu ya udongo wa volcano...
 

Juzijuzi nilikuwa hapo mtaa wa maendeleo karibu na Uwanja wa ndege wa zamani.
Aiseeh kuna vumbi Makanya Kwetu pakasome.
Nilikaa Siku tano tuu nikakimbilia Tukuyu
 
Atayesema Mbeya kuna vumbi basi atakua hajafika Dodoma na Manyara.

Vumbi la Mbeya kuna maeneo haulikuti. Ila hiyo mikoa miwili ni ile unatoka nje kwenda dukani ukarudi ndani unarudi na share yako ya vumbi
Dodoma mjini hakuna vumbi la kutisha.
 
Pia Mbeya maeneo yaliyojengeka vizuri hayapo pembezoni mwa barabara, yamejificha ndani
Huku along the road ndio uswazi umejaa left and right kwa hiyo ukikatiza kwenda Zambia hutaona chochote cha maana
Nasikia bado kuna nyumba za matope mjini!
 
Mbeya can't be a city.. it is an affiliated municipal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…