Hivi Mbunge Nassary aliishia wapi? Mrithi wake kwenye kiti cha Ubunge ni nani? Au Jimbo lilibaki wazi?

Hivi Mbunge Nassary aliishia wapi? Mrithi wake kwenye kiti cha Ubunge ni nani? Au Jimbo lilibaki wazi?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Nassary alikuwa kijana machachari Sana kutoka huko Arusha, alikuwa anajenga hoja na kusimamia serikali. Toka nimwone jukwaani akimnadi JPM sijawahi kimwona tena sijui kama yupo nchini au anafanya kazi nje; huyu kijana pamoja na Masele NI watu ambao hakuna siku watamsahau Ndugai. Ndugai alimvua mmoja Ubunge kimabavu na mwingine akafungiwa milango ya uspika huko Afrika Kusini

Baada ya Nassary kupotea kwenye siasa kutokana na usaliti naamini alipatikana mrithi jimboni kwake; Je mrithi wake ni nani? Mbona hakuna sehemu anasikika?

Lakini pia Stephen Masele naye kapotea, sijui Youth league iliwaandaa kuwa viongozi au iliwaandaa kuwa waoongozwa. Umepewa talenti unakubalije mwanaume mmoja akukandamize? Bora wangefuata nyayo za mashujaa waliokimbia nchi kuliko kuambatana na mwanaume ambaye naye anataka sifa kama wao.

Vijana jitokezeni mnunue Uhuru wenu; amkuzaliwa kutawaliwa mlizaliwa kuongoza.
 
Acha ubinafsi , hasadi na chuki, Mwamba huyu hapa akilitumikia taifa:

40F4E302-7E86-4E9A-A32E-8A1223CEC168.jpeg
 
Back
Top Bottom