Hivi Mdude Nyagali ni kiumbe wa namna gani?

Hivi Mdude Nyagali ni kiumbe wa namna gani?

Kwenye hotuba yake ya kwanza akiapishwa Rais Samia mnamo 19/03/2021 alitamka kuwa magazeti yafunguliwe, wananchi waikosoe Serikali kwa mujibu wa sheria. Akasisitiza na kesi za kubambikizwa zifutwe. Akakemea Kodi za DHULUMA zikusanywazo na TRA, na kuikemea TAKUKURU na Polisi kwa kuwanyanyasa watu bila makosa.

Kweli tukaanza kuona nuru mpya baada ya siku chache. Ikawa kama ni kupindua kabisa mambo ya ukatili na uuaji ambayo yalitamalaki wakati wa Magufuli.

Kesi ya Akwilina ikapinduliwa na Mahakama ya Rufaa, yule Mdude CHADEMA wa Mbozi maarufu kwa matusi naye akashinda kesi

Mara tukaanza kusikia kauli za matusi kwenye mikutano ya CHADEMA. Mfano ni ile kauli ya Mdude siku 4 tu baada ya kuachiwa alisikika akiongea Jukwaani Barracuda Tabata kuwa "Mwambieni huyo Mama yenu, nitamnyoa kwa wembe uleule niliotumia kumnyoa mtangulizi wake"

Alitamka maneno mbele ya Mbowe na viongozi wengine wa CDM na hawakumchukulia hatua mpaka leo.

Kwa mtazamo wangu Serikali imeona pengine bado hatuna busara katika kutumia uhuru wa maoni. Tunaleta matusi badala ya kutoa maoni.
Huu ndio ukweli.
 
Ninamlaumu Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA kwa kutomsaidia Mdude kisaikolojia na kumwacha aangamie. Mbona kina Malisa GJ na yule mtoto wa Mbowe hawapati kashkash kama za Mdude?

Jibu ni kuwa wazazi wao ambao pia ni wamiliki wa CHADEMA wanawaongoza vizuri na kuwaonya kuhusu uropokaji. Mdude kwasababu ni mtu baki ni kama wamemtoa kafara.

Anachoambulia ni hashtag ya free mdude. Kina Mnyika wao huwa hawakamatwi kwa sababu wanajua timing ya kuongea.

Mdude kama watoto wengine kutoka familia maskini wanawekwa mstari wa mbele kimakusudi na mmiliki wa CHADEMA Sultan Mbowe.
Ni kweli kabisa.
 
Majitu mnayowaza kuishi kwakupumliwa nyuma huwa hamuwazi kujitegemea zaidi ya kufurahisha mabwana zenu. Achana na Mdude huyo ni mwanaume sio we shoqer.
Na wewe nenda front kama yeye au hautaki kuwa mwanaume? Mnamlisha upepo mwenzenu anajikuta Oliver Tambo kumbe ni Arlus Mabele anapitia matatizo makubwa wewe upo mtaani una enjoy life.
 
Back
Top Bottom