Hivi Milioni 25 inatosha kujenga nyumba ya vyumba vitatu kwa Dodoma na wilaya zake?

Hivi Milioni 25 inatosha kujenga nyumba ya vyumba vitatu kwa Dodoma na wilaya zake?

Samahani mkuu, umewahi kujenga? Kama ana kiwanja 25m anapaswa kufika mbali zaidi ya hapo uliposema.

nina nyumba.
Inategemea na ukubwa wa nyumba. Kama anajenga nyumba vyumba vidogo kama Gest sawa. Nayo itaishia kwenye bati.
 
Mkuu hapo utaangalia wewe mwenyewe kama unafamilia kubwa au laa.
Mana hapo kila anachangia anachokiona af na kutokana na mazingira anayoishi
Hizo 25m zinaweza zitoshe au zisitoshe kutegemeana na mazingira.
Cha muhimu tafuta fundi mzuri tu mkae chini mdizain ramani ya nyumba kwamb hapa tufanye hv ili iwe hvi.so hapa kila mtu anatoa ushauri wake.
Kwahiyo hapo ufikire mwenyewe.
Nawasilisha.@min -me instinct desire.
 
Ubarikiwe sana mkuu🙏🏼
Ushauri wako nimeupokea
 
Wale wenye ujuzi/ushuhuda kwenye ujenzi kwa Dodoma naomba mniambie Je! Mil 25 inatosha kumaliza nyumba ya vyumba vitatu?

NB: wale wa kuendelea kushangaa magorofa ya watu endeleeni ss wenzenu ndo tumeanza hivyo.
Kujenga nyumba ya vyumba vitatu kwa material gani? Gharama ni function ya aina ya material unayotumia!
 
Boma sio Nyumba tofautisha Nyumba na Boma ni vitu viwili tofauti kuna watu wanaishi kwenye Boma na kuna watu wanaishi kwenye Nyumba
Tupe tofauti ya Boma na Nyumba.

maana maasai kwa kiswahili chao, wao nyumba huita ni boma.
 
Tupe tofauti ya Boma na Nyumba.

maana maasai kwa kiswahili chao, wao nyumba huita ni boma.
Boma humo humo Mama humo humo Mbuzi humo humo watoto humo humo kuku, hilo ni Boma, nyumba inajitegemea Sebule ya kutosha, ndani humo humo kuna living room, dining, rest room, library, store, studio, nk hio ni nyumba tena sio nyumba ya kawaida ni nyumba ya kisasa, chumba 3 choo nje sebule uchochoro hilo ni Boma sio nyumba
 
Wale wenye ujuzi/ushuhuda kwenye ujenzi kwa Dodoma naomba mniambie Je! Mil 25 inatosha kumaliza nyumba ya vyumba vitatu?

NB: wale wa kuendelea kushangaa magorofa ya watu endeleeni ss wenzenu ndo tumeanza hivyo.
Ukisubiri kupata ushauri humu JF, unawezajikuta umeghairi kujenga, maana humu utaambiwa hiyo milioni 25 yako haitoshi hata kujenga mlango wa choo.

Humu JF, karibia wote tunamiliki majumba ya milioni 100 plus, na mabilioni.

👇🏽
Wewe kama unaanza ujenzi, wewe anza tu (tafuta a proven fundi kupitia watu unafahamiana nao mtaani kwako) kisha wewe na fundi muanze tathmini kwenye vitu na gharama, kuanzia:-
  • Ramani (ukubwa na mpangilio wa nyumba)
  • Tofali (mtafanya tathmini ya tofali ngapi.)
  • Bati ngapi (itategemea na aina ya upauaji)
  • mchanga (fundi mzoefu atakwambia mpaka kiasi cha mchanga)
  • saruji
  • nondo
  • kokoto
  • mbao
  • chokaa (wall putty Gypsum Powder kwa ajili ya skimming)
  • madirisha
  • gharama za ufundi
  • n.k

Mkimaliza tathmini, then mtaanza kucheki ni wapi mnaweza kubana cost ili mbakie kwenye bajeti yenu pasipo ku-compromise project.

👇🏽
@ Fundi mahiri wa Ujenzi | @ Ujenzi nafuu 01 | @ Fundi manyumba | @ aise | @ nyanda madirisha | @ Jamiix

👇🏽
Pia pitia huu uzi
Naombeni mchanganuo wa gharama na idadi ya materials ya kujenga fensi ya ukuta 20m x 20m
 
Gharama za kujenga nyumba inategemra na ukubwa wa nyumba husika.

Kwa nyumba standard (vyumba 3) mara nying upana ni kat 10 m - 12 m na urefu 12 m -15 m.

Kwa hiyo 25 Miln.
Utajenga msing. Unapandisha matofali had juu kwenye lenter na kozi zile 3.
Na Utajaza kifus ndan na kuweka level.
Hela kama kubak itabak kidogo sana nadhan.

Nyumba standard finishing na kila kitu kukamilika hufikia 60-80 miln.
Kuna budget designs ambazo naamini mleta mada anamaanisha kujenga budget house.

Kwa budget designs(hapa nasemea kwa ujumla hasa Dar), milioni 15-20 umamaliza hadi kuezeka. Finishing itategemea unataka kuweka nini, madirisha aina gani, milango aina gani nk.
 
Back
Top Bottom