Uko sahihi kuwa consultation fee ni kubwa, lakini hiyo haileti uhalali wa kuiondoa, labda useme ipunguzwe.
Unachotakiwa kuelewa ni kuwa, consultation fee ni moja ya chanzo muhimu cha mapato kwa hizi hospitals kwani serikali haighalimii kila kitu kwa 100%. Maana yake ni kuwa, ikiondolewa pale hospital itapelekwa sehemu nyingine na lazima wananchi tuilipie tu. Kama ni ugumu wa maisha utaendelea kuwa pale pale. Ni kama vile development Levy ilivyoondolewa ikawekwa kwenye bidhaa ikasababisha bidhaa kupanda bei. Au kodi ya nyumba ilivyowekwa kwenye umeme ikasababisha umeme kupanda bei.
Kiufupi uendeshaji wa hospitals kama zilivyo taasisi nyingine una gharama sana ambazo ukisema serikali izilipe zote kutoka kwenye makusanyo ya kodi moja kwa moja watu watalia zaidi.
Suluhisho hapa ni matumizi sahihi ya rasilimali zetu ili tukuze uchumi wetu. Ndio hapo serikali itaweza kulipa vizuri hizi gharama zote. Lakini kwa mwendo wetu huu, we've a long way to go.