Wewe mbona uko mjini unafanya nini huko?
Lakini sijatelekeza mke kijijini.
Wawe wanaondoka na wake zao basi, maana wengine wanaacha mke na watoto wanataabika kijijini hata matumizi hawatumi.Maisha ya kijijini magumu jamani tusiwalaumu sana,mtu unalima lakini hakuna kwa kuuza mazao yako na hata ukiyauza hakuna faida yoyote,pia huduma muhimu nazo hakuna,ukienda kwenye zahanati dawa hakuna,unadhani mtu bado atakuwa na mawazo ya kuendelea kukaa kijijini?
Hata sisi wa mjini nasi tunatamani kwenda sehemu nyingine zilizoendelea zaidi kwa ajili ya kutafuta maisha bora haijalishi unayapata vipi au unafanya nini.
Mengine ni udhaifu wa mtu binafsi.
Jamani huku vijijini kumekuwa na wimbi kubwa la vijana kukimbia na kwenda mjini kwa kisingizio cha kwenda kutafuta maisha. Lakini sasa imekuwa ni kero kwa baadhi ya vijana wa kiume waliooa kutelekeza wake zao na kwenda kutafuta maisha mjini. Na wengi wao hawarudi kabisa au wakirudi wanakuwa wameoa wake wengine ambao wamewapata mjini. Hii imekuwa ni kero sana maana inasababisha ongezeko la watoto wa mitaani...........
Hao wanasiasa ndio wanatia kichefuchefu kabisa..Mbunge wangu yupo huko yapata miaka minne nilimwona mara ya mwisho Kijijini akiwa kwenye kampeni akijinadi na kutaka Kura yangu!
Amepata Uongozi sasa na Familia kaihamishia huko mjini!
Ile nyumba yake aliyokuwa anaijenga kijijinihaitaki tena anasema amepata kiwanja (Open Space) Pale Masaki hivyo atasimamisha mjengo huko!
Watoto wake tuliokuwa tunasoma nao pale Shule ya msingi Mchungwani wamehamishiwa International school kule kenya!!
Anasema hatarudi mjini na sasa kwani yupo busy na Viongozi wenzie kuangalia namna ya kujenga flying Over hapo Mjini Dsm!!! Bora Nije nikae huko alipo mbunge wangu aliyepata madaraka baada ya kura yangu kumchagua!...... NISIJE MJINI WAKATI KIONGOZI WANGU YUPO HUKO MWAKA WA 4 SASA? HAINIINGII AKILINI NAKUJA HUKO HUKO MJINI!!!
Ahahaah!! Kama maisha yakitulia lazima niwakumbuke wa kijijini.
Niamini.