Hivi mke wa Rais analipwa mshahara?

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
854
Swali na ufafanuzi kidogo.

Utasikia mke wa rais kachangia hiki kachangia kile, katoa pesa taslim kiasi fulani. Swali langu, je na wake wa marais huwa wanapewa mshahara? Kama ndiyo kwa kazi gani wanazozifanya kwa walipa kodi? Kama hapana, hizo hela wanazotoa huwa wanazipata wapi wakati hawana kazi wala mshahara? Kadhalika, kama analipwa mshahara kwa pesa za walipa kodi, je, katiba inasemaje kuhusu mshahara wa mke wa rais? Kama hiyo haitoshi, je nao hukatwa pesa kwa ajili ya michango kwenda mifuko ya jamii kama vile PPF, NSSF ama LAPF? Je, hukatwa Pay As You Earn?

Ninaamini swali si kosa kwa mujibu wa katiba yetu.
 
Nami HP nasubiri jibu maan wengine walianzisha NGO's
 
Kwa Mujibu wa Sheria zetu...Mke wa Raisi anpata nusu ya Mshahara wa mumewe. Na hii nikutokana na kazi kubwa ya kulinda afya ya Raisi wetu. Kumbuka kuwa ndio mtu pekee anayeweza kuwa faraga na Raisi kwa muda mrefu zaidi. Na mambo mengine mengi tu. Wajuzi wa mambo watakupa uelewa.
 
huwa wanasema wnaenda kwenye sherehe au sehem ya kutoa msaada anamwambia mumewe anapa iyo hela.
 
Mimi naunga mkono yeye kupewa hata posho kumbukeni yeye ni kipunguza pressure cha mkuu wetu anapotindikiwa na majukumu.Kazi ya uraisi ni ngumu sana
 
Msaada please,
Mshahara wa Nini??
Kazi yake ina likizo??
Ofisi yake Iko wapi??
Job Descriptions zake ni zipi??
Boss wake ni nani??
Anaingia Ofisini saa ngapi na kutoka saa ngapi??
 
Mshahara wa Nini??
Kazi yake ina likizo??
Ofisi yake Iko wapi??
Job Descriptions zake ni zipi??
Boss wake ni nani??
Anaingia Ofisini saa ngapi na kutoka saa ngapi??

Shark wewe ni denjarasi, hadi JD yake unaitaka...ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha...
 
Shark wewe ni denjarasi, hadi JD yake unaitaka...ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha...
Nilikua nawaza tu huo mshahara anaupokea wa nini??
Yaani kua first Lady ni Cheo, Majukumu au nini??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…