CHA The GREAT
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 651
- 854
Swali na ufafanuzi kidogo.
Utasikia mke wa rais kachangia hiki kachangia kile, katoa pesa taslim kiasi fulani. Swali langu, je na wake wa marais huwa wanapewa mshahara? Kama ndiyo kwa kazi gani wanazozifanya kwa walipa kodi? Kama hapana, hizo hela wanazotoa huwa wanazipata wapi wakati hawana kazi wala mshahara? Kadhalika, kama analipwa mshahara kwa pesa za walipa kodi, je, katiba inasemaje kuhusu mshahara wa mke wa rais? Kama hiyo haitoshi, je nao hukatwa pesa kwa ajili ya michango kwenda mifuko ya jamii kama vile PPF, NSSF ama LAPF? Je, hukatwa Pay As You Earn?
Ninaamini swali si kosa kwa mujibu wa katiba yetu.