Hivi Mkuu wa Wilaya Ubungo atathibitishaje ukahaba wa hawa watu?

Bilioni 36 zitatokea wapi. ???
Tusubiri muda utaongea !
 
madada poa (makahaba) walikuwepo toka enzi za kwenye biblia. Tafuta habari ya Kahaba Rahabu kwenye biblia, au habari ya mwanamke aliyetaka kuuliwa kwa kupigwa mawe sababu ya uzinzi lakini akaokolewa na Yesu.
Wengine wakaambiwa yule anayejiona hana dhambi aanze kurusha jiwe kumpiga yule mwanamke mzinzi 😳
 
Muache akafie mbele kwa stroke mbele ya wasomi wakali! Ameshaanza kudaiwa 36b/-
Halafu anashitakiwa binafsi! hakuna state attorneys
 
Utakuta hata yeye kapitia wengi tu au katemwa
Haki za binadamu zina mambo mengi sana, uhuru wa mtu huwezi kuuingilia kwa kukamata

Kama ni street crawlers sawa wakamatwe kwa sababu za kiusalama na maadili
Lakini kama wanajistiri huko ni kumnyima mtu haki zake za msingi
Sitetei bali ni haki ya mtu kufanya anachotaka ili mradi havunji sheria
 
Tatizo lilinzia pale alipoita na Waandishi wa habari wakiwa na makamera yao huku Polisi wakitumia nguvu kuwatoa watu vyumban hapa ndipo alipokosea sana kavamia faragha za watu
Cross Examination Day;

Wakili:
Mhe. Mkuu wa Wilaya ijuze mahakama kiwango chako cha elimu.

Mkuu wa Wilaya:
Shahada

Wakili:
Ieleze mahakama majukumu yako kwa kifupi

Mkuu wa Wilaya:
Mwakilishi wa Mhe. Rais Wilaya ya Ubungo na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Wilaya

Wakili:
Je! Unawafahamu madada 36 walioko hapa mahakamani

Mkuu wa Wilaya:
Siwafahamu

Wakili:
Ilikuwaje ukaamuru Polisi wawakamate na kuwashikilia mahabusu?

Mkuu wa Wilaya:
Ni 'madada Poa'

Wakili:
Mhe. Mkuu wa Wilaya ieleze mahakama unamaanisha nini unaposema hawa ni 'Madada Poa?'

Mkuu wa Wilaya:
'Madada Poa' ni wanawake wanaojishughulisha na biashara haramu ya kuuza miili yao.

Wakili:
Je! Ulijuaje madada hawa wanafanya hiyo biashara uliyoisema?

Mkuu wa Wilaya:
Niliwakuta wamesimama usiku Sinza

Wakili:
Je! Ulipowakuta walikuuzia wewe miili yao

Mkuu wa Wilaya:
Hapana

Wakili:
Je! Unaweza ukataja majina ya wateja (wanaume) waliokuwa wananunua miili ya hawa madada?

Mkuu wa Wilaya:
Sikuwaona.

Wakili:
Unafahamu maana ya biashara

Mkuu wa Wilaya:
Biashara ni shughuli ya kuuza na kununua bidhaa au huduma

Wakili:
Je! kusimama Sinza usiku ni kufanya biashara

Mkuu wa Wilaya:
Hapana

Wakili:
Je! Kusimama Sinza usiku ni kosa la Jinai?

Mkuu wa Wilaya:
Hapana

Wakili:
Je! Unafahamu kuwaita madada hawa jina ulilowaita na kuwaweka kwenye Vyombo vya Habari ni kuwadhalilisha na kutweza utu wao mbele ya waume zao, familia zao na umma kwa ujumla (Defamation)?

Mkuu wa Wilaya:
Ndio

Wakili:
Je! Unafahamu kuwakamata watu na kuwashikilia rumande Polisi kwa muda wa ziadi ya siku tano pasipo kuwapeleka mahakamani ni kinyume cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura 20?

Mkuu wa Wilaya:
Najua

Wakili:
Kwa hiyo umefanya makusudi kuvunja Sheria za nchi?

Mkuu wa Wilaya:
Hapana. Nilikuwa nasafisha Wilaya yangu ya Ubungo

Wakili:
Je! Unamaanisha hawa madada ni takataka?

Mkuu wa Wilaya:
Hapana

Wakili:
Mhe. Hakimu sina maswali zaidi.
 
Labda wakikubali kupata mikopo Kwa maana watakuwa wamekubali kufanya ukahaba pia inaweza Ikawa njia rahisi ya kukwepa mtego wa maswali yako, japo hakuna asiyependa pesa, Swali fikirishi je hiyo mikopo Wana biashara za kuwezesha kulipa marejesho, (kulipa mkopo)
 
Huyo DC hakupaswa kuendelea kuwa katika ofisi ya umma mpaka sasa hivi, ni kwa vile tu nchi hii individual freedom rights sio kitu cha kutiliwa maanani sana.
 
Vijana kwa wazee, wote wanasimama na dada poa, hadi raha.....

#freedadapoa #freezeutamu
Wakimaliza kuwadhalilisha wanaodaiwa dada poa watahamia kwa michepuko, madanga na watu wanaoishi kama mume na mke bila ndo mwisho mnashangaa mmegeuka kama Iran au Afghanistan hakuna hata kuingia chumbani wawili kama hamna cheti cha ndoa.
 
Wilaya ya ubungo inaongoza kwa baraka mbovu DSM angeshughulikia hilo kwanza tungemshukuru sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…