Hivi mlianzaje biashara zenu, mbona wengine tunakwama?

Ajira zetu zina maslahi madogo, kwahiyo tunadhani kuwa na biashara ya pembeni inaweza kusaidia kujikwamua kumbe tunakosea, hapo una maanisha mtu ashike moja?
Hata kuwa na maslai maslai madogo Nako ni kukosa option kwaiyo itakulazimisha kukaza japo utakata tamaa kwasababu hata ukiacha hela ya kula unayo
 
Shida biashara za vijana wa siku hizi zinachekesha sana, unakuta dogo ana idea, full theory kabisa ukianza kumuuliza maswali hana majibu.

You are selling the product u didnt invent,
The formula u didnt discover,
Yaan idea haina potential yyt zaidi ya story za vijiweni tu, hajui RR iko vp, biashara za hvo walifanikiwa waloanza zamani kabla ya kuwepo kwa ushindani, sasa hivi lazima uwe na kitu unique au special.

Tutakununulia bia na soda tu, lakini kwa ideas uchwara hatukupi hata mia, hapo bora nikununulie bia ntamchangia mmiliki wa bar
 
Hata Hiyo bar sio unique idea
 
Kufeli ni moja ya progress katika kwenye biashara it's not easy that why we have fewer billionaires in the world.
 
Ili ufanikiwe inakupasa ukutane na magumu haswa, asilimia kubwa ya walio fanikiwa walipoteza kwanza kwa ukubwa katika walivyo kuwa wakimiliki. Huwezi kutoboa kirahisi rahisi tu labda utoboe pua.
 
Biashara kwa kweli sio mchezo mchezo lazima uwe na moyo mgumu.Yaani uwe tayari kuanguka na kusimama tena.
Mimi baada ya maisha kunipiga na kukosa ajira hapa mjini niliuza gari na kufungua biashara ya cosmetics...baada ya kama miezi 6 mzigo ukawa unaisha na hela siioni.Ikabidi nianze kutafuta tena mtaji wa kuibust biashara,yaani sio kazi rahisi
 
Binafsi nilianza biashara baada ya kuombewa na mch Mwamposa kawe... Nilkua nashindwa kabisaa yan pesa ipo lkn ata kwa kuanzia sijui naanzajee... now mambo yanaenda nina biashara mkuu.. Thanks God
 
Aisee biashara inahitaji moyo,nakumbuka mwanzo nliteketeza mil 10,nikaokoa laki 4 pekee. Sito sahau. Lakini hatimaye nilianza upya baada ya muda kidogo
Mimi nimepoteza jumla ya milion 300 hadi nikajuatia Bora ningezifanyia ngono nisingeumia.
Bora upoteze Hela kwenye starehe kuliko kwenye biashara,nilichoambulia ni uzoefu wa kutosha kuhusu mapito mbalimbali ya biashara na uwekezaji lakini sijakata tamaa Leo hata nipate billion 800 siwezi zuzuka na Hela.
 
Duu majibu ya maswali yote hayo ninayo labda nianza kwakukuuliza swali, je wazo la biashara unalo km unalo biashara unayotaka kuifanya unaijua? angalizo mtaji mimi nakuambia siyo tatizo. Tutajifunza hatua kwa hatua mradi tuwe na bundle la kutosha na muda
 
"Mzigo unaisha na hela siioni"

Huoni kama hilo lilikuwa ni tatizo la kiuendeshaji badala ya kulaumu ugumu wa biashara? Maana kuuza uliuza ila pesa ndio ulishindwa kuitunza.
 
Ukipata watu ambao tayari wametangulia kwenye hicho ambacho unataka kufanya kisha wakushike mkono kimawazo na ukakubali kujifunza kwao, ni lazima utoboe bila kupoteza kiasi kikubwa cha fedha kama wanavyosema wadau humu.

Usithubutu kuanza biashara bila kuwa na mzoefu yoyote, lakini pia usithubutu kukabidhi pesa zako za mtaji kwa huyo mzoefu, kwake tumia uzoefu wake tu, akili na rasilimali iwe ni juu yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…