Hivi mlianzaje biashara zenu, mbona wengine tunakwama?

Hivi mlianzaje biashara zenu, mbona wengine tunakwama?

Biashara hizi zina changamoto nyingi sana ndugu yangu, ukiona watu wanafilisika usidhani ni wapumbavu.Mtu huwezi kufilisika kama stock ipo,unafilisika kwa sababu stock inaisha na pesa haionekani.

Na wala haihusiani na utunzaji wa fedha maana kama mimi pesa ya dukani nilikua hata siitumii kwa matumizi binafsi.

Waulize wafanyabiashara watakuambia,unauza siku nzima ikifika jioni unajikuta una elfu 10 zingine hazipo
Au ulikuwa unaamini kwenye maombi? Kwasababu kwa akili ya kawaida huwezi kufungua biashara bila kamati ya ufundi kuhusika
 
Aisee biashara inahitaji moyo,nakumbuka mwanzo nliteketeza mil 10,nikaokoa laki 4 pekee. Sito sahau. Lakini hatimaye nilianza upya baada ya muda kidogo
Natamani kujua zaidi ilikuwaje mkuu
 
Wakubwa hapa leo najaribu kuelezea madhira tunayopitia vijana tunaojitafuta, tunapata mawazo mengi na kuchora mipango mingi sana ya mafanikio...

Ukifungua notebooks zetu utaona tumeandika mipango mingi ya kutoboa ila tunakosa jinsi ya kuanza.
Binafsi natamani kuwa na biashara flani ila kila nikijaribu kuanza nashindwa, muda ninao ila ninachokosa Ni (1) Rasilimali fedha (2) Rasilimali watu.

Yaani kwenye mitaji tunafeli sana, sometimes tunatamani hata kushikwa mkono na waliotangulia kufanikiwa lakini haiwezekani.

Huwa najiuliza kwanini waliofanikiwa wanakuwa na ugumu wa kumsaidia mtu kuanzisha project zake ila wapo tayari hela zao mkatumie wote kwenye starehe alafu akiachana na wewe baada ya bata hakuachii hata senti 5[emoji23][emoji23] atakununulia kitu ila sio kukupa fedha mkononi. Kuna siri gani hapo?

MASWALI MUHIMU
1. Hivi nyie mlifanikiwa vipi kuanza biashara zenu na zikaenda?
2. Hela(mtaji) mlipata wapi?

3. Siri ya kuwa mfanyabiashara ni ipi?

ASANTENI SANA[emoji120][emoji120]
Mada mbili tofauti kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Corona ilinifanya nipoteze zaidi ya mil 300,baada ya hapo nikayumba sana nusu ya kuwa chizi maana sikuwa na assets yoyote itakayonisaidia ku compasate mpaka sasa naunga unga tu ila kwa mitego niliyotega mwaka huu inshallah nitapiga hatua flan
 
Back
Top Bottom