Asee movies Ni hobby yangu tokea zamani sana.
Nachopendelea movies za majuu
1.idea ya filamu na wazo kuu mfano angalia movie ya saw kuanzia sehemu ya kwanza
2.wahusika wanavaa uhusika kisawasawa mfano refer Matt Damon wa movies sequel za Jason Bourne , Pamoja na John crammer wa the saw
3.wapiga pichà (cinematographers) wanajua kucheza na angle za kupiga picha,na hisia za mtazamaji yaani wanapiga picha kumshirikisha mtazamaji nawe awe sehemu ya tukio
4.mandhari ya movie na YENYEWE ni kigezo kwanini napenda movie za majuu .ma producer wako tayari kutumia kiasi chochote kile cha pesa katika kutafuta mandhari .
Mfano madmax fury ya 2015 yale mandhari ya jangwani ilikuwa ni jangwa la Kalahari namibia na Australia.unaweza kuvuta picha ni kiasi gani walitumia kutengeneza mandhari.
5.movie za majuu kwanza zipo dynamic Sana kwenye swala la dhamira katika maisha yetu.mfano vita,utumwa ,usaliti, mauaji, madawa ya kulevya na magonjwa
Kwa mfano filamu ya CONTAGION ya 2013 Kama sikosei inazungumzia world pandemic ya Corona virus
6.sound effect na sound track zimekaa poa sana tofauti na za kwetu ,kama ni sehemu ya huzuni lazima sound track itaendana ,kama Ni battle lazima ziendane...
Na mengine kibao.tu
Sasa mtu mwingine anakuja humu ana dis kuhusu kuangalia filamu binafsi ninamuona kama punguani tu .
Kila mmoja hupenda kufanya kile anachotaka as long as havunji kanuni na taratibu za kisheria za kijamii.