Hivi mnaokulaga mikate usiku au vyakula vilaini laini vya aina hiyo,huwa mnawezaje kupata usingizi?

Hivi mnaokulaga mikate usiku au vyakula vilaini laini vya aina hiyo,huwa mnawezaje kupata usingizi?

Isenye

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2024
Posts
1,985
Reaction score
5,167
Wakuu habari za usiku?
Aisee jana hali yangu kiuchumi haikua nzuri,nikaona ngoja ninunue mkate nile nilale,mkate nimeula saa 3 usiku,ila hivi sasa ni saa 9 usiku usingizi umekata kabisa nimeamka kukoroga hata uji ninywe maana sio kwa njaa hii ninayoisikia aisee.
Hivi nyie wenzetu hasa wa hapo dar mnaokula mikate na kisha kulala usingizi mnono mpaka asubuhi mnaweza vipi hili jambo?
 
Watakuambia mikate yao wanayokula ni tofauti na ya huko kwenu kibaigwa.
 
Umeuliza swali la maana sana, hivyo vyakula vyepesi huwa havileti usingizi labda uongeze kinywaji kizito. Kula mkate usiku hutokea pale unapokuwa umeshiba ila unaongezea shibe kwa kula chakula chepesi usilale bila kula, utaumwa na njaa usiku wa manane kama hutajazia shibe usiku
 
Wakuu habari za usiku?
Aisee jana hali yangu kiuchumi haikua nzuri,nikaona ngoja ninunue mkate nile nilale,mkate nimeula saa 3 usiku,ila hivi sasa ni saa 9 usiku usingizi umekata kabisa nimeamka kukoroga hata uji ninywe maana sio kwa njaa hii ninayoisikia aisee.
Hivi nyie wenzetu hasa wa hapo dar mnaokula mikate na kisha kulala usingizi mnono mpaka asubuhi mnaweza vipi hili jambo?
Naweza kula mkate usiku endapo utakuwa na vipako vyake kama siagi au n.k. pia usindikizwe na yai au soseji, tunda kama ndizi mbivu na chai nzito.
Kula mkate mkavu na chai ya maji na sukari usiku sifiki saa nne.
 
Kama unaishi uswahili usile mkate usiku maana wachawi wanakuja kukuchukua ukalime
 
Ni kujizoeza kutokuwa mlafi, Fanya hivyo week 1 tumbo lieazoea
 
Ukiwa umeshiba vizuri mchana ukila Mkate usiku hutapata shida sana ya njaa.
 
Hujalizoesha tumbo lako hivyo,usitegemee kama utashiba..
Nina uwezo wa kula chipsi mayai mbili kwa mlo mmoja na Pepsi baridi na kula tena mlo unaofuata kama ni WA usiku,vizuri kabisa bila shida..
Pia ninao uwezo kutokunywa chai asubuhi then mchana nikanywa chai na mkate wa buku usiku nisile chochote hadi kesho mchana tena.
 
Back
Top Bottom