Hapo ni kweli kabisa taaluma za nje na nyumbani ni tofauti kwa kujituma kutokana na taaluma zao au hakuna ajira nyingi za wataalamu hao
Ila majuu ni tofauti sana kwani alichosomea anajitahidi kufika mbali kwa alichosomea
Wapo wengi sana wameamua kutengeneza bidhaa kutokana na taaluma zao wakiwa hata nyumbani tu
Mfano mdogo tu juzi juzi walileta habari inayowahusu wahitimu wawili walioanzisha kutengeneza bia wakiwa nyumbani miaka miwili iliyopita na leo bia zao zipo supermarkets zote baada ya kuchukua mkopo na kupata wafadhili
Leo account zao zimetapika
Wapo waliojiendeleza kwa kutengeneza Apps na zikawaingizia hela sana nao ni wasomi pia
Elimu inasaidia sana kwa walioelewa wamesoma nini ila sio kukariri