Hivi Mo akitoa Bilioni 20 anatakiwa kuwapa wakina nani?

Hivi Mo akitoa Bilioni 20 anatakiwa kuwapa wakina nani?

Mi naelewa kwamba kama mtu unakampuni, tuseme mtaji wake ni 1,000,000 na wewe ni mmiliki asilimia 100. Ukimuuzia mtu asilimia 50 ya kampuni basi atakupa 500,000 na wewe utazitia mfukoni na kwenda kunywa bia , kuhonga nk.
Sasa Mo anavyonunua hisa na kutoa hizo 20 b anamkabidhi nani ambaye ndiyo miiliki wa Simba?
Anakabidhi bodi ya wadhamini ya simba
 
Mkuu hapo ndo kimbembe maana hisa moja ina cost 40M+,je Mo akiweka mzigo wanachama wapo tayar kuweka the rest %?!,

Ila kuna baadhi yao wanasema eti wao 51% yao Ni majengo na baadhi ya assets za kampuni,

Sasa swali la kujiuliza ni kua je? Hizo assets zao zinafikia thamani ya 51%?.
Ndio brand ya simba inaweza kufika dhamani hiyo
 
Swali langu kwa wale watalaamu wa uhasibu,Hivi simba ikiwa kampuni Assets zinatajumuisha na wachezaji? na kama hapana vipi pale wanapouza wachezaji wanakuwa wanauza nini ki- uhasibu, yaani treatment yake kwenye vitabu inakuwaje.Angalizo hapa panahitaji jibu la kihasibu,kama siyo mhasibu jipe nafasi ujifunze kutokana na majibu.
Wafanyakazi wa taasisi yoyote sio sehemu ya Assets za taasisi hata kama yeye ndio sababu kuu ya taasisi kupata mapato.mfano dr.Mwaka jina lake ndio linaleta mapato kwenye hospitali yake au kuna baadhi ya hospitali au kitengo fulani cha hospitali kinaingiza mapato sababu wagonjwa wanakuja kwasababu ya dr.fulani na siku huyo Dr. anahama na wagonjwa wanahama. Au kuna law firm zinaingiza mapato sababu kuna mmojawapo wa mwanasheria ndio wateja wanamiminika hapo.lakini hao wote hawawezi kuwekwa kama assets za taasisi husika.kwanini? Sasa hapa nitakupa sababu za kiuhasibu
 
Ikumbukwe Simba wanatumia mfumo wa 'board of directors' ilihali club bado haijawa transformed,
Hii Board of Directors ndio inayojulikana katika katiba mpya ya Simba, bila kujali mchakato wa kampuni umekamilika au la. Kwa hiyo usichanganye kampuni na katiba ya Simba. Kwa hiyo hata kama mchakato hautafanyika kabisa, muundo wa uongozi wa Simba umeshabadilishwa kwenye katiba iliyosajiliwa serikalini, na ni lazima iwepo Board of Directors
 
Mi naelewa kwamba kama mtu unakampuni, tuseme mtaji wake ni 1,000,000 na wewe ni mmiliki asilimia 100. Ukimuuzia mtu asilimia 50 ya kampuni basi atakupa 500,000 na wewe utazitia mfukoni na kwenda kunywa bia , kuhonga nk.
Sasa Mo anavyonunua hisa na kutoa hizo 20 b anamkabidhi nani ambaye ndiyo mmiliki wa Simba?
Pesa inaenda Kwa Kampuni Ya Simba, itaingizwa kwenye account za Benk za Kampuni Ya Simba.

Lengo kuu LA Kampuni Kuuza Hisa ni Kukuza Mtaji sio kugawana thamani halisi ya Kampuni.

Mfano Kampuni Real Estate INA miliki maghorofa 30, unapouza Hisa za Hiyo Kampuni Lengo sio kugawana Yale magorofa, lengo ni Kuongeza Mtaji ili Muweze kuongeza Idadi ya Maghorofa, mnunuaji Hisa anaona akiwekeza Mtaji wake hapo atapata faida au atakuwa sehemu ya wanaokula faida ya Biashara hiyo.Kwa maelezo haya pesa hizo hazinywewa bia Bali zitatumika ktk Uwekezaji kulingana na Management itakavyoona uwekezaji huo utaleta faida kwa kampuni kujiendesha na kupata faida ili wanahisa wale faida ya uwekezaji wao
 
Hii Board of Directors ndio inayojulikana katika katiba mpya ya Simba, bila kujali mchakato wa kampuni umekamilika au la. Kwa hiyo usichanganye kampuni na katiba ya Simba. Kwa hiyo hata kama mchakato hautafanyika kabisa, muundo wa uongozi wa Simba umeshabadilishwa kwenye katiba iliyosajiliwa serikalini, na ni lazima iwepo Board of Directors
Ndio maana wale wazee walikua wanalalamika kua katiba ya Simba 'imenajisiwa' na wahuni wa Simba huku ikiwa Mo dewji ndo dereva wa hao 'wahuni' walionajisi' katiba.
 
alafu hizo hela zinaenda kufanya nini?
Lengo kuu LA kuuza Hisa ni Kukuza Mtaji, Hivyo Simba itapata Ongezeko LA Mtaji LA 20Bn zitumike ktk uwekezaji, hapana shaka zitawekezwa ktk eneo ambalo Management itaona litaleta tija na kuzaa faida.Ndio Maana inabidi Simba itoke ktk mfumo wa Club(non profit) kuwa Kampuni(profit making organization)
 
Mkuu kwasasa Wanachama si wanamiliki asilimia 100? Sasa wanapata nini na kuuza kwao 49?. Hiyo 51 ni yao toka zamani.
Au Mo si mnunua hisa. Maana ukinunua hisa pesa haziendi kwenye mtaji wa kampuni bali zinaenda kwa wamiliki wa hisa/ kampuni, kwa Simba wanachama.
Mpaka sasa hakuna Mmiliki wa Simba Sports Company sababu mchakato wake wa Kuwa Kampuni bado haujakamilika, Wanachama Wa Simba ni wamiliki wa Simba Sports Club, walipata umiliki huo kwa kuwa tu na kadi ya Uanachama na kulipia Ada ya Uanachama which is cheap ukilinganishwa na kuwa Mmiliki au sehemu ya Umiliki wa Kampuni itakayokuwa yaani Simba Sports Club.Hivyo Basi iwe imeelezwa au haijaelezwa kwa ufahamu wangu hiyo 51% iliyobaki itaingizwa sokoni wanahisa wanunue Lakini Wanachama wakipewa kipaumbele
 
Hili linawezekana lakini hutokea pale kampuni huwa na hali mbaya. Hutafuta muwekezaji na kumpa hisa na wao hutumia zile pesa kujikwamua. Kama kampuni inaenda poa na ikauza hisa basi zile pesa hupewa wanahisa/wamiliki.
Kwa Simba bado haijafikia huko, iko ktk Hatua ya awali ya kutaka Kukuza Mtaji, hivyo Kampuni ndio inauza Hisa, hela itaenda kuwa sehemu ya Mtaji, Baadae sasa mfano baada ya Mwaka Mmoja au miwili, Mo anaweza tu anytime akaamua kuuza 29% ya Hisa zake kwa yoyote anayetaka kununua abaki na 20% au akaamua kuuza zoooote, hela atakayouza anachukua Yeye
 
According to FFC,Simba bado hawajakamilisha mchakato,kwahiyo Simba bado haijawa kampuni,

Mo dewji hauzi shares,ila ana mpango wa kununua shares za 49% ambazo zina gharimu 20B kwa mujibu wake na viongozi wa Simba,

Kwa madai yao mchakato ukikamilika wa ku-transform club from member's tier to shareholders' tier ndo ataweka mzigo,

Ikumbukwe Simba wanatumia mfumo wa 'board of directors' ilihali club bado haijawa transformed,

Karibu.
Kulingana na memorandum of understanding, hizo pesa zilitakiwa ziwekwe kwenye escrow account, ndani ya miezi mitatu tu, kwanza wakati mchakato ukiendelea.
 
Kwa mpira huu wa bongo mnataka hizo hela zije kurudi na faida JUU?
Huyo anaenda kutoa SADAKA HELA ZAKE.
hyo club yenyewe ya Simba Haina thamani ya bilioni 20.
Lengo kuu LA kuuza Hisa ni Kukuza Mtaji, Hivyo Simba itapata Ongezeko LA Mtaji LA 20Bn zitumike ktk uwekezaji, hapana shaka zitawekezwa ktk eneo ambalo Management itaona litaleta tija na kuzaa faida.Ndio Maana inabidi Simba itoke ktk mfumo wa Club(non profit) kuwa Kampuni(profit making organization)
 
Simba ni mali yao, wameamua tu kuuza 49 percent kwa twenty Bln. watoe nini tena?

Wao wakina nani hasa speciffically?

Halafu hao wao hao ,waliamua wao au Mo mwenyewe kwa mapenzi yake ya timu ndo alitamka mwenyewe icho kiasi cha B20? Kwani angesema wamuuzie izo hisa labda kwa Bilion 5 wangekataa?

Na ni mfumo upi umetumika ku value izo hisa za 49% ziwe sawa na Bilioni 20?
 
Back
Top Bottom