Hivi Mo akitoa Bilioni 20 anatakiwa kuwapa wakina nani?

Anakabidhi bodi ya wadhamini ya simba
 
Ndio brand ya simba inaweza kufika dhamani hiyo
 
Wafanyakazi wa taasisi yoyote sio sehemu ya Assets za taasisi hata kama yeye ndio sababu kuu ya taasisi kupata mapato.mfano dr.Mwaka jina lake ndio linaleta mapato kwenye hospitali yake au kuna baadhi ya hospitali au kitengo fulani cha hospitali kinaingiza mapato sababu wagonjwa wanakuja kwasababu ya dr.fulani na siku huyo Dr. anahama na wagonjwa wanahama. Au kuna law firm zinaingiza mapato sababu kuna mmojawapo wa mwanasheria ndio wateja wanamiminika hapo.lakini hao wote hawawezi kuwekwa kama assets za taasisi husika.kwanini? Sasa hapa nitakupa sababu za kiuhasibu
 
Ikumbukwe Simba wanatumia mfumo wa 'board of directors' ilihali club bado haijawa transformed,
Hii Board of Directors ndio inayojulikana katika katiba mpya ya Simba, bila kujali mchakato wa kampuni umekamilika au la. Kwa hiyo usichanganye kampuni na katiba ya Simba. Kwa hiyo hata kama mchakato hautafanyika kabisa, muundo wa uongozi wa Simba umeshabadilishwa kwenye katiba iliyosajiliwa serikalini, na ni lazima iwepo Board of Directors
 
Pesa inaenda Kwa Kampuni Ya Simba, itaingizwa kwenye account za Benk za Kampuni Ya Simba.

Lengo kuu LA Kampuni Kuuza Hisa ni Kukuza Mtaji sio kugawana thamani halisi ya Kampuni.

Mfano Kampuni Real Estate INA miliki maghorofa 30, unapouza Hisa za Hiyo Kampuni Lengo sio kugawana Yale magorofa, lengo ni Kuongeza Mtaji ili Muweze kuongeza Idadi ya Maghorofa, mnunuaji Hisa anaona akiwekeza Mtaji wake hapo atapata faida au atakuwa sehemu ya wanaokula faida ya Biashara hiyo.Kwa maelezo haya pesa hizo hazinywewa bia Bali zitatumika ktk Uwekezaji kulingana na Management itakavyoona uwekezaji huo utaleta faida kwa kampuni kujiendesha na kupata faida ili wanahisa wale faida ya uwekezaji wao
 
Ndio maana wale wazee walikua wanalalamika kua katiba ya Simba 'imenajisiwa' na wahuni wa Simba huku ikiwa Mo dewji ndo dereva wa hao 'wahuni' walionajisi' katiba.
 
alafu hizo hela zinaenda kufanya nini?
Lengo kuu LA kuuza Hisa ni Kukuza Mtaji, Hivyo Simba itapata Ongezeko LA Mtaji LA 20Bn zitumike ktk uwekezaji, hapana shaka zitawekezwa ktk eneo ambalo Management itaona litaleta tija na kuzaa faida.Ndio Maana inabidi Simba itoke ktk mfumo wa Club(non profit) kuwa Kampuni(profit making organization)
 
Mpaka sasa hakuna Mmiliki wa Simba Sports Company sababu mchakato wake wa Kuwa Kampuni bado haujakamilika, Wanachama Wa Simba ni wamiliki wa Simba Sports Club, walipata umiliki huo kwa kuwa tu na kadi ya Uanachama na kulipia Ada ya Uanachama which is cheap ukilinganishwa na kuwa Mmiliki au sehemu ya Umiliki wa Kampuni itakayokuwa yaani Simba Sports Club.Hivyo Basi iwe imeelezwa au haijaelezwa kwa ufahamu wangu hiyo 51% iliyobaki itaingizwa sokoni wanahisa wanunue Lakini Wanachama wakipewa kipaumbele
 
Hili linawezekana lakini hutokea pale kampuni huwa na hali mbaya. Hutafuta muwekezaji na kumpa hisa na wao hutumia zile pesa kujikwamua. Kama kampuni inaenda poa na ikauza hisa basi zile pesa hupewa wanahisa/wamiliki.
Kwa Simba bado haijafikia huko, iko ktk Hatua ya awali ya kutaka Kukuza Mtaji, hivyo Kampuni ndio inauza Hisa, hela itaenda kuwa sehemu ya Mtaji, Baadae sasa mfano baada ya Mwaka Mmoja au miwili, Mo anaweza tu anytime akaamua kuuza 29% ya Hisa zake kwa yoyote anayetaka kununua abaki na 20% au akaamua kuuza zoooote, hela atakayouza anachukua Yeye
 
Kulingana na memorandum of understanding, hizo pesa zilitakiwa ziwekwe kwenye escrow account, ndani ya miezi mitatu tu, kwanza wakati mchakato ukiendelea.
 
Kwa mpira huu wa bongo mnataka hizo hela zije kurudi na faida JUU?
Huyo anaenda kutoa SADAKA HELA ZAKE.
hyo club yenyewe ya Simba Haina thamani ya bilioni 20.
 
Simba ni mali yao, wameamua tu kuuza 49 percent kwa twenty Bln. watoe nini tena?

Wao wakina nani hasa speciffically?

Halafu hao wao hao ,waliamua wao au Mo mwenyewe kwa mapenzi yake ya timu ndo alitamka mwenyewe icho kiasi cha B20? Kwani angesema wamuuzie izo hisa labda kwa Bilion 5 wangekataa?

Na ni mfumo upi umetumika ku value izo hisa za 49% ziwe sawa na Bilioni 20?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…