Hivi Msukuma halisi huwa anatokea wapi?

Kifaru86

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2017
Posts
1,734
Reaction score
3,822
Kwa wale wadau ambao mshawahi kuishi na kukaa Usukumani mtakuwa mnatambua ndani ya usukuma kuna jamii karibia tano na wote wanajiita Wasukuma.

Lakini ndani ya Usukuma wenyewe kwa wenyewe wamekuwa wakibaguana ya kutokana na asili ya walipotokea kwa mfano zipo jamii ambazo zinasadikika walitokea Zambia, Rwanda, Burundi, Congo, Uganda zilikuja kuishi maeneo ya Tabora, Mwanza, Geita, Shinyanga wanajiita wasukuma lakini inasemekana sio Wasukuma.

Kwa mfano ndani ya Usukuma kuna jamii kama vile Wazinza, Wasubwa, Wadakawa, Wanyatuzu, Wakonondogo, watusiyoo n.k na kila jamiii ina historia yake ni wapi walipotokea ila wengi wakiwa mijini wanajiita wasukuma lakini wakirudi makwao wanabaguana kuwa sisi Wasukuma wale sio Wasukuma.

Hebu tusaidiane hivi msukuma asili au asili ya msukuma inatokea katika jamiii ipi au wenyewe wasukuma original wanatokea sehemu gani

Msukuma halisi kabisa niwa nnhela, Maeneo ya wilaya ya kwimba, misungwi na nusu ya maswa, magu na kishapu hao ndio wasukuma halisi



Msukuma halisi kabisa niwa nnhela, Maeneo ya wilaya ya kwimba, misungwi na nusu ya maswa, magu na kishapu hao ndio wasukuma halisi


Aba missungwi tumanyhe aha, kwandeja busagara, bukirigulu, mapilonga, ng'wanangwa, misasi, seke, kijima, buhingo, busongo, nyasamba, mbarika, manawa, nyamle, ng'wabaraturu, ne mitindo, ng'wabuke, koromije,

 
Nani kakwambia wazinza,wasumbwa,wakonongo ni Wassukuma? Kwa huku kwetu tuna Bhanantunzu,bhadakama(wanyamwezi), Bhanang'wagala, Bhasumabhu na Bhanabhulima ndio hao wanaform kabila la WASUKUMA ambapo kuna wengine huwagawa kwa pande kuu nne za dunia.

Na kwa nyongeza tu hatujawahi kubaguana hata siku moja siye tukikutana na kujuana tunaanza na kubonga kikwetu iwe ndan ama nje ya mikoa tunayopatikana kwa wingi .
 

Sielew sana histry ya Wasukuma !ila ulicosema ni kweli 100%ngumu sana msukuma kum-bagua msukuma mwenzake!
 
SWADAKTA.
 
Msukuma halisi kabisa niwa nnhela, Maeneo ya wilaya ya Kwimba, Misungwi na nusu ya Maswa, Magu na Kishapu - hao ndio Wasukuma halisi
Huyo Msukuma halisi anaitwaje, maana jamii zote hizo zipo eneo moja.
 
Kiuhalisia kabisa Sukuma walihamia kutoka nchi ya Ethiopia huko ndio hasiri yao ila inawezekana napo huko kuna sehemu walitoka kabla kwan jamii za zamani zilikuwa zinahama kutokana na sababu mbalimbali mfano kushindwa vita na himaya kuchukuliwa, majanga, kujitenga kutoka kwenye utawala fulani au kufukuzwa na jamii husika.
 
Basukuma= Wakaskazini
Banang'weli= Wamagharibi
Badakama= Wakusini (mnawaita wanyamwezi kwa kweli hakuna wanyamwezi)
Banakiya= Wamashariki

Hawa wote ni lugha moja watofautiana lafidhi tu
Wasukuma (bhasukuma) ni Mwanza na Shinyanga
Banang'weli(bhanang'weli) hawa ni wasumbwa wanakaa zaidi sehemu za Geita na Kahama
Badakama (bhadakàma) au wanyamwezi mkoa wapo eneo karibu lote la Tabora
Banakiya(bhanakiya) ni wanyantuzu ni wasukuma maeneo yao ni Bariadi, Maswa tuseme mkoa wote wa Simiyu kwa akina Cheyo,Shibuda na Vijisenti
Nimeishia hapo kama anayejua zaidi karibu
SUKUMA ni kaskazini
DAKAMA ni kusini
KIYA ni mashariki
NG'WELI ni magharibi
Watu hawa lugha moja ni mtawanyiko wao ulivyo
 
Msukuma halisi kabisa niwa nnhela, Maeneo ya wilaya ya kwimba, misungwi na nusu ya maswa, magu na kishapu hao ndio wasukuma halisi

Mkuu naweza sema kwamba hayo maeneo ndiyo yalikaliwa na wasukuma mwanzon na kwa mda mrefu sana kumbuka walikua wanatoka upande wa maghalibi ng'weri na kuelekea mashariki ambapo walienda kukumbana na Wamaasai na kuweza kupata mikikimikik hasa watoto wa kiume (hapa staliweka wazi sana ) lakin ushawahi fatilia kwenye maholelo ya kwetu chanzo cha kuwa wanapandwa na mizim na kuongea Kimasai/ama kitaturu chanzo nin?

Kwain hifadhi ya maswa kwenye milima kuna nyumba nyingi za kale hata makaburi ya watu maalufu kama vile Nyendwa, Sita (huyu mpaka leo kuna nyumba ake na mabak ya ziz na ng'ombe wake waliobadilika na kuwa mawe na kisima chake na alisafir mpaka Butiama na alitabiri mpaka kuzaliwa kwa nyelele) mtemi wa mwisho wa meadu (ngwesa) .

Lakin pia fatilia story ya Ng'witulo gwa Ng'wawilyamu miaka ya 1950.
Kwa kifupi wasukuma wamegawanyika kuanzia zaman na hasa kufatana na utawala wao na hata maeneo yao na kuweza kuunda makundi yaliyopo mpaka sasa kama nilivyo yataja.

Na ikumbukwe kwamba kikwetu asili aridhi yote ni yawanawake na ndio walikua watawala japo kulingana na wakati walikua wanapinduliwa na waume zao .

Lakin ti kwa hekima mpaka leo tunawaanzi hao watawala wa mwanzo kwa salam japo sku izi watu hawajui ata maana ya hizo hekima za salam (lwimbo) na kwa hawa watawala kunawaliokuwa na maeneo makubwa sana na wanaonekana kuwanaidadi kubwa ya watu kama vile MINZA,( wanatumia EMINZA), Wengine ni akina.

NKWAYA, SEGA, NKWIMBA, SABHE, NG'WASHI, n.k

Na kuna hawa wanasalimiwa NG'WAKADILU walifata kwa huyu mama KADILU hakuwa mtemi na alizaliwa tu kwa kufata jua na asubuhi na alipaya pia wa kumuunzi kwa salam.
 
Fact! Na safari ya mababu zetu ilianza karne ya 6
 
Huyo msukuma halisi anaitwaje maana jamii zote hizo zipo eneo moja
Mkuu kwa kawaida tu head state ya Wasukuma wote ipo USUKUMA Mwanza na hata zile shelehe na bhulabho zilikua zinafanyikia mara nyingi maeneo yale na huko ndiko mtemi wa kabila lote aliteuliwa japo anaweza kutoka sehem yeyote wasasa sijajua ametokea eneo gan japo wamwisho mie kumfahamu alikua Majebhele toka Busia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…