Kifaru86
JF-Expert Member
- Apr 22, 2017
- 1,734
- 3,822
Kwa wale wadau ambao mshawahi kuishi na kukaa Usukumani mtakuwa mnatambua ndani ya usukuma kuna jamii karibia tano na wote wanajiita Wasukuma.
Lakini ndani ya Usukuma wenyewe kwa wenyewe wamekuwa wakibaguana ya kutokana na asili ya walipotokea kwa mfano zipo jamii ambazo zinasadikika walitokea Zambia, Rwanda, Burundi, Congo, Uganda zilikuja kuishi maeneo ya Tabora, Mwanza, Geita, Shinyanga wanajiita wasukuma lakini inasemekana sio Wasukuma.
Kwa mfano ndani ya Usukuma kuna jamii kama vile Wazinza, Wasubwa, Wadakawa, Wanyatuzu, Wakonondogo, watusiyoo n.k na kila jamiii ina historia yake ni wapi walipotokea ila wengi wakiwa mijini wanajiita wasukuma lakini wakirudi makwao wanabaguana kuwa sisi Wasukuma wale sio Wasukuma.
Hebu tusaidiane hivi msukuma asili au asili ya msukuma inatokea katika jamiii ipi au wenyewe wasukuma original wanatokea sehemu gani

Msukuma halisi kabisa niwa nnhela, Maeneo ya wilaya ya kwimba, misungwi na nusu ya maswa, magu na kishapu hao ndio wasukuma halisi
Mkuu naweza sema kwamba hayo maeneo ndiyo yalikaliwa na wasukuma mwanzon na kwa mda mrefu sana kumbuka walikua wanatoka upande wa maghalibi ng'weri na kuelekea mashariki ambapo walienda kukumbana na wamaasai na kuweza kupata mikikimikik hasa watoto wa kiume (hapa staliweka wazi sana ) lakin ushawahi fatilia kwenye maholelo ya kwetu chanzo cha kuwa wanapandwa na mizim na kuongea Kimasai/ama Kitaturu chanzo nin?
Kwain hifadhi ya maswa kwenye milima kuna nyumba nyingi za kale hata makaburi ya watu maalufu kama vile Nyendwa, Sita (huyu mpaka leo kuna nyumba ake na mabak ya ziz na ng'ombe wake waliobadilika na kuwa mawe na kisima chake na alisafir mpaka Butiama na alitabiri mpaka kuzaliwa kwa nyelele) mtemi wa mwisho wa meadu (ngwesa) .
Lakin pia fatilia story ya Ng'witulo gwa Ng'wawilyamu miaka ya 1950.
Kwa kifupi wasukuma wamegawanyika kuanzia zaman na hasa kufatana na utawala wao na hata maeneo yao na kuweza kuunda makundi yaliyopo mpaka sasa kama nilivyo yataja.
Na ikumbukwe kwamba kikwetu asili aridhi yote ni yawanawake na ndio walikua watawala japo kulingana na wakati walikua wanapinduliwa na waume zao .
Lakin ti kwa hekima mpaka leo tunawaanzi hao watawala wa mwanzo kwa salam japo sku izi watu hawajui ata maana ya hizo hekima za salam (lwimbo) na kwa hawa watawala kunawaliokuwa na maeneo makubwa sana na wanaonekana kuwanaidadi kubwa ya watu kama vile MINZA,( wanatumia EMINZA), Wengine ni akina.
NKWAYA,SEGA,NKWIMBA,SABHE,NG'WASHI,n.k
Na kuna hawa wanasalimiwa NG'WAKADILU walifata kwa huyu mama KADILU hakuwa mtemi na alizaliwa tu kwa kufata jua na asubuhi na alipaya pia wa kumuunzi kwa salam
Msukuma halisi kabisa niwa nnhela, Maeneo ya wilaya ya kwimba, misungwi na nusu ya maswa, magu na kishapu hao ndio wasukuma halisi
Wasukuma original wanapatikana sehemu za mashambani kuanzia biharamulo, teremka hadi Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Igunga, Nzega hadi Bunda....wengine wako kule Ihefu, Kigamboni, Kilosa, Rukwa, Katavi, kibondo na singida. Kuna wasukuma hybrid waliochanganya wazazi....hawa wako miji yote ya Tanzania......
Aba missungwi tumanyhe aha, kwandeja busagara, bukirigulu, mapilonga, ng'wanangwa, misasi, seke, kijima, buhingo, busongo, nyasamba, mbarika, manawa, nyamle, ng'wabaraturu, ne mitindo, ng'wabuke, koromije,
Sehemu yao ya uzawa inaitwa Majebele, far east of sukuma land, hapa ndio pana Malkia anayezaa wasukuma, ndio maana wasukuma wana move kutoka East kwenda west and south of Sukuma land, meaning From Simiyu, to Mwanza, Shinyanga, Geita, Rubondo, Biharamulo, Kahama, etc.