Hivi Msukuma halisi huwa anatokea wapi?

Mkuu walitokea western kuelekea east na huko waliishi kwa kipindi kirefu walikutana na kimbembe kutoka kwa wamasaiv(kutoka ukoo wa wali) hii stori huwa haitoi na ni ngum sana kujua kwa sababu za kuondoa uhasama wa kikabila ndio walianza kurud tena magharibi .
Japo kunasababu tena ya ukame kumbuka siye ni wafugaji asa kwa maeneo kama kishapu,maswa,lalago,meatu,mwamanongo,n.k ni ngum sana kuishi na kund kubwa la mifugo.
Ukienda pande za meatu vijijin ulizia kwa wazee sana ambao ni wazawa wa kule utapata mwanga.
 

Mkuu huo mlima naufaham na nilisha utembele unaanzia maeneo ya kalibia kanegere unaelekea mega,mpaka mwaningi na unaenda kuishia msalala kama sijakosea na kuna sehem wanachimba dhahabu mkanda wa mwakitolyo na yale mawe yakuogea wanayoyauza sehem nyingi wanayatolea kule.

LYANDI LYA BHALOHA(TUTA LA BALOHA) hili ndio jina lake kwa jina letu la kisukuma na lilipatikana kutokana na umbile la mlima huu upo kama LYANDI (TUTA) na jamii walio kua wakiishi maeneo hayo (bhaloha) .

Na kwa upande wa hii Enkamba ni watu ambao walikuwa jini ya utawala Nkamba na hii jamii ilikua ya wahuzi wa vyuma kama majembe (haya yanapatikana kwa sasa kwa waganga wakienyeji kwa wingi) ,shoka ,mapanga,njuga,n.k mpaka saiv jamii ya hawa watu bado wanajihusisha na uhuz wanayusha chuma na kuanda kitu kingine mifano mikuki,njuga,shoka,visu n.k
 
msukuma sio mbaguzi wa kabila . msukuma sio mchoyo wa chakula. msukuma ni mwaminifu mchapa kazi . hata ukioa mwanamke wa kisukuma umeoa kweli hakuna kudanganyana . ukiona msukuma anatofauti na hizo sifa basi sio msukuma ni wazinza. wasumbwa au amechanganya au amekulia usukumani akajiita msukuma
 


Wamekuwa kama Wahaya na makabila ya Kagera. Wote wakiwa Dar wanajiita wahaya, wakirudi makwao wanabaguana.
 



Naona umeenda kwenye rant ya kujifanya life coach!Wewe mwanadamu mwenzangu unanifundishaje jinsi ya kuishi?Who are u?

Na pia huwezi nipangia maswali ya kuuliza!Maswali uulizwe halafu upange uulizwe yepi?Kwanza right questions kwa mujibu wa nani?Wewe?Pleaseee!

Northerners ya wapi?With reference to wapi?Eti Northerners,ya wapi?Ushahidi wako wa jina la Sukuma eti ndio ushahidi mnatoka Ethiopia?Try again!

Bujora is rubbish!Hakuna any research proven...Bujora ni museum with no any scientific evidence kua mnatokea Ethiopia.Kuna andiko lolote proven?Hakuna!


Kujibu kunya hakukusaidii chochote ku-prove Sukuma ina originate from Ethiopia.Tangu lini Bantu people waka-originate from Horn of Africa kama sio ukichaa wenu?
 
Fact
 
Uko vzr....kwenye hizo salamu umenifungua skujua maana yake
 
Rekebisha mada yako Mkonongo,Mzinza,Mrongo si msukuma ni makabila tofauti kabisa wala si jamii za kisukuma labda Wadakama na Wanyantunzu ndo jamii za kisukuma
 
Ni kweli kabisa ameandika asichokijua huyo
 
Msukuma halisi kabisa niwa nnhela, Maeneo ya wilaya ya kwimba, misungwi na nusu ya maswa, magu na kishapu hao ndio wasukuma halisi
Usiisahau na Mza ambapo ndo chimbuko kabisa la msukuma na akaanza kutawanyika kwenda kusini ambayo ni Shinyanga Magharib Sengerema na Geita,Kusini Magharib ni Mnyamwezi
 
Banang'weli ni wasukuma walioko Bunzinza(Sengerema) na Geita wala sio Wasumbwa hili ni kabila tofauti kabisa na wasukuma,ulishawahi kuwasikia wanaongea nusu kama kiha hivi
 
Ni kweli ila hilo la lwimbo lwa Nkwaya ulitokana na mchanganyiko na kabila la wakwaya toka Mara
 
Unachokisema ni kweli kabisa na walikuwa wanasema lwimbo huo ili wasisahau walikotoka ni sawa na Enkwaya hawa ni Wakwaya toka Mara
 
Nilikwenda Bunda sikuamini kukuta jamii ya Wasukuma kubwa sana. Na hata nasikia Esther Bulaya ni Msukuma japo sina uhakika kwa baba au mama.
Bunda Wasukuma ni wengi mno zaidi ya 1/3 ni wao tu ile ni wilaya yao nadhan ilikuwa hivi kwa sababu ya kuwa karibu sana na Lamadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…