DOKEZO Hivi Msumi ipo Dar es Salaam kweli?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
We unaishi wp pasipo na changamoto ya usafili?
 
Sa we ulitakaje?
 
Penye ccm dominance lazima pawe hivyo. Refer dodoma, Singida na Pwani.
 
Ni kama kumesahaulika miundombinu ni mibovu mno,mbunge wa huko ana kazi ya kufanya kutetea kiti 2025. Ila watu wanapakimbilia sana sijui kuna nini ?
Mbunge hawezi kuhofia kupoteza jimbo sababu ya kutojengwa barabara, tena hata hatishiki. Anachoweza kuhofia ni suala la kuteuliwa na chama chake, ila kama ana uhakika wa kupitishwa na chama chake basi hata barabara isipitike yeye hajali. Labda atakachohofia ni pale akiona kelele zenu zinaweza kufika kwa Rais na katibu mkuu wa chama chake
 
Hata Mapinga Kerege wengine hulazimisha ionekane wapo Dar, hiyo haibadili jiografia halisi..... Pwani inazidi kupokwa maeneo yake na ipo kimya tu.

Ahaa ila Dar pia ilikuwa ni mkoa wa pwani ila ikamegwa ili kutengeneza jiji ndio maana Dar ndio mkoa uliozungukwa na mkoa. By the way, Dar ishaanza kujaa ndio maana sehemu za pembeni zinaingizwa katika tafsiri za watu kama ni Dar hata kama sio Dar kimipaka
 
Wakazi wa Msumi na Mpiji magoe wanatia huruma sana kama hawako Dar es salaam tena langoni mwa Jiji.
 
Kuna mradi wq DMDP phase two watajenga barabara ya msumi kilometa 9.08 . Ujenzi unaanza mwezi wa saba. Kipindi wanatangaza zabuni ili mkandarasi apatikane. Tembelea page ya mkuu wa mkoa you tube autakuta kafafanua barabara ambazo zitapitiwa lami
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…