Mtaji huu unatosha sana kwa mtu anayejituma na asiye na woga wala aibu(soni).
Angalia mambo haya muhimu kwanza.
1. Eneo unaloishi, kama pana mzunguko wa watu wengi.
2. Eneo utakalofanya biashara hii kama mazingira yanaruhusu.
3. Mahali utakaopata bidhaa zako, kwa Dsm Kariakoo, Mabibo (Mahakama ya ndizi) Buguruni sokoni etc.
Baada ya hapo fanya maamuzi kati ya biashara hizi.
1. Matunda maembe, machungwa, mapershen ndizi mbivu n.k.
2. Mboga mboga
3. Mhogo au viazi vitamu vyakuchoma
4. Mahindi mabichi.
Kanuni:
1. Nunua bidhaa za kutosha siku moja au mbili tu hasa kwa zile zinazoweza kuharibika haraka.
2. Panga faida ndogo kiasi ili kukuza mzunguko maana faida haitokani na bei kuwa kubwa bali wingi wa wanaonunua.
3. Fuata bidhaa zako mapema na wahi eneo lako la biashara.
4. Usafi wa bidhaa zako ma mazingira yake.
Mchanganuo:
Biashara ya Matunda.
1. Ndizi mbivu @ Tshs 100 Tshs 5,000/= uza Tshs 150/= unapata Tshs 7,500/=
2. Maembe @ Tshs 200/= - Tshs 5,000/= uza Tshs 300/= hadi 400/= unapata Tshs 7,500 10,000/=
3. Parachichi @ Tshs 200/- Tshs 5,000/= uza Tshs 300/= hadi 400/= unapata Tshs 7,500 10,000/=
4. Machungwa @ Tshs 100/- Tshs 5,000/= uza Tshs 150/= hadi 200/= unapata Tshs 7,500 10,000/=
5. Pasheni @ Tshs 25/- Tshs 5,000/= uza Tshs 50/= unapata Tshs 10,000/=
6. Nauli ya bidhaa zako pamoja na wewe Tshs 5,000/=
Hivyo utaona Faida utakayotengeneza kwa mtaji huu ni Tshs 40,000 30,000 = Tshs 10,000/=