Hivi mtaji wa 30,000/= unaweza kufanyia biashara ipi?

Hivi mtaji wa 30,000/= unaweza kufanyia biashara ipi?

JF ya sasa inachefua sana, sijui kwa nini watu wanaingia kwenye jukwaa serious kama uchumi na biashara halafu wanaanza kudhihaki wenzao! Watu wengine hawafanani kabisa na upmbavu wanaopost!!! Kuna watu wanaanza na mtaji 0, baadaye anatumia nguvu zake anapata elfu5 kuanzia hapo anaizungusha mpaka kutoka, sembuse mtu ana elfu30?!!..thats a lot of money.
 
Kama uko Dar fungua kibanda cha chips mayai na kuku wadada wa Dar wanatafuna sana hii kitu mradi utengeneze vizuri tu.
 
kama uko dar wahi alfajiri maeneo ya ubungo mataa upande wa oil com nunua maziwa fresh........yanahitajika sana zama hizi faida ukipata utukumbuke...!!
mkuu sijaelewa, maziwa huwa yanauzwa hapo oil com au? funguka kidogo
naish ubungo, embu nitupie hiyo fursa!
 
Chungwa mzazi au miwa ila jakikisha kuwa mtaji huo si wakutegemea kwa matumizi ya hom kwa muda kama wiki mbili hivi
 
fanya biashara ya chakula mkuu...na vile uko kampuni ya ulinzi, ukiwa lindo la usiku, basi mchana unawauzia msosi walinzi wenzio, ukiwa lindo la mchana unamuachia mama watoto hiyo kazi.

utatoka tu....hata mbuyu ulianza kama mchicha!
 
Katika wachangiaji wote hamna aliyemsaidia Babu na hii imesababishwa na babu mwenyewe kwa kushindwa kuelezea awali mahali alipo na wachangiaji mmeanza kutiririka tu kwa mbwembwe na kejeli mkizani kuwa kila mwanaJF yupo dar!
Mleta maada yupo korogwe,ningemshauri hiyo 30,000/= aliyonayo aendelee kuongezea kwa kufanya savings kama jinsi alivyozipata. Kwakua pale korogwe kumebarikiwa kuwa na mito isiyokauka basi ajipange ifikapo june aanze kufanya biashara ya mbogamboga kwa kulima mwenyewe hasa ngogwe,mchicha,mchunga,mnavu,chainizi,mwidu,tembele,majani ya kunde,kisamvu na bamia kwa kupeleka Handeni ambapo ni karibu sana ( kwa kipindi hicho handeni kutakuwa kukame) pia anaweza kwenda na kurudi pasipo kuathiri kazi yake kama atapata wasaa wa kuhudhuria lindo lake usiku.
Mpaka januari mwakani atakua ameweka kibindoni mkwanja mrefu usiopungua milioni5 kwa kulima nusu eka tu ya mchanganyiko wa mbogamboga hapo juu.
 
Last edited by a moderator:
Babu rudisha feedback watu wajitolea kwasababu yako lakini sioni respond mzee.
 
ela kubwa sana iyo we angalia location yako then check demand ya watu wat do they want do to their scarcity wengne wavvu wakwenda fer kutake fsh so unaenda unanunua unakuja kuwauzia kwa bei ya faida jus advic!
 
Invisible mtu kupewa ban ya wiki moja kutamfanya awe na nidhamu kidogo au jukwaa hili halina kiongozi, majibu mengine hugeuka karaha kwa wanaohitaji msaada au hata wanaopitia maoni hayo.
 
Last edited by a moderator:
kama uko dar wahi alfajiri maeneo ya ubungo mataa upande wa oil com nunua maziwa fresh........yanahitajika sana zama hizi faida ukipata utukumbuke...!!

Dah hili wazo nilikua nalo nikawa sijui wapi karibu pa kupata maziwa fresh, nmegundua maeneo mengi mjini hakuna maziwa halisi ya ng'ombe. unaweza fahamu ni shilingi ngapi kwa lita hapo ubungo?
 
#nzalendo respect to you.Si kama wengine utani mwingi hata mtu anapokuea anamaanisha.

salute kwako.

kwa kuongezea tu uza kifaa unachotumia kuingia mtandaoni Laptop au simu(bila shaka ni android types) ILI UONGEZE MTAJI na kama ni muumini wa internet cafe acha na uzitumie pia hizo bukubuku na muda unaotumia huko kuestablish mradi wako taraji.
 
Mtaji wa Tshs 30,000/=​
Mtaji huu unatosha sana kwa mtu anayejituma na asiye na woga wala aibu(soni).

Angalia mambo haya muhimu kwanza.
1. Eneo unaloishi, kama pana mzunguko wa watu wengi.
2. Eneo utakalofanya biashara hii kama mazingira yanaruhusu.
3. Mahali utakaopata bidhaa zako, kwa Dsm – Kariakoo, Mabibo (Mahakama ya ndizi) Buguruni sokoni etc.
Baada ya hapo fanya maamuzi kati ya biashara hizi.
1. Matunda – maembe, machungwa, mapershen ndizi mbivu n.k.
2. Mboga mboga

3. Mhogo au viazi vitamu vyakuchoma
4. Mahindi mabichi.
Kanuni:
1. Nunua bidhaa za kutosha siku moja au mbili tu – hasa kwa zile zinazoweza kuharibika haraka.
2. Panga faida ndogo kiasi ili kukuza mzunguko – maana faida haitokani na bei kuwa kubwa bali wingi wa wanaonunua.
3. Fuata bidhaa zako mapema na wahi eneo lako la biashara.
4. Usafi wa bidhaa zako ma mazingira yake.
Mchanganuo:
Biashara ya Matunda.
1. Ndizi mbivu @ Tshs 100 – Tshs 5,000/= uza Tshs 150/= unapata Tshs 7,500/=
2. Maembe @ Tshs 200/= - Tshs 5,000/= uza Tshs 300/= hadi 400/= unapata Tshs 7,500 – 10,000/=
3. Parachichi @ Tshs 200/- Tshs 5,000/= uza Tshs 300/= hadi 400/= unapata Tshs 7,500 – 10,000/=
4. Machungwa @ Tshs 100/- Tshs 5,000/= uza Tshs 150/= hadi 200/= unapata Tshs 7,500 – 10,000/=
5. Pasheni @ Tshs 25/- Tshs 5,000/= uza Tshs 50/= unapata Tshs 10,000/=
6. Nauli ya bidhaa zako pamoja na wewe Tshs 5,000/=
Hivyo utaona Faida utakayotengeneza kwa mtaji huu ni Tshs 40,000 – 30,000 = Tshs 10,000/=
 
Iangalie jamii yako, ondoa uoga na utengeneze fursa kwa matatizo yaliyoko kwenye jamii yako.
 
katika wachangiaji wote hamna aliyemsaidia babu na hii imesababishwa na babu mwenyewe kwa kushindwa kuelezea awali mahali alipo na wachangiaji mmeanza kutiririka tu kwa mbwembwe na kejeli mkizani kuwa kila mwanajf yupo dar!
Mleta maada yupo korogwe,ningemshauri hiyo 30,000/= aliyonayo aendelee kuongezea kwa kufanya savings kama jinsi alivyozipata. Kwakua pale korogwe kumebarikiwa kuwa na mito isiyokauka basi ajipange ifikapo june aanze kufanya biashara ya mbogamboga kwa kulima mwenyewe hasa ngogwe,mchicha,mchunga,mnavu,chainizi,mwidu,tembele,majani ya kunde,kisamvu na bamia kwa kupeleka handeni ambapo ni karibu sana ( kwa kipindi hicho handeni kutakuwa kukame) pia anaweza kwenda na kurudi pasipo kuathiri kazi yake kama atapata wasaa wa kuhudhuria lindo lake usiku.
Mpaka januari mwakani atakua ameweka kibindoni mkwanja mrefu usiopungua milioni5 kwa kulima nusu eka tu ya mchanganyiko wa mbogamboga hapo juu.
kilimo si rahisi kama unavyodhani
 
dah hili wazo nilikua nalo nikawa sijui wapi karibu pa kupata maziwa fresh, nmegundua maeneo mengi mjini hakuna maziwa halisi ya ng'ombe. Unaweza fahamu ni shilingi ngapi kwa lita hapo ubungo?

kwa kipindi hiki sina uhakika na bei,ila ni vizuri uwepo eneo la tukio utapata details za kutosha.
 
Back
Top Bottom