Hivi mteja kama huyu unamjibuje?

Hivi mteja mpya ameulizia bidhaa ukamtajia bei mkaja mkashindwana bei anakuuliza sehemu nyingine ni wapi?

Wewe kama customer care unamjibuje!
Kama mmeshindwana bei si basi!!
Wewe unapata ukakasi Gani kumwelekeza sehemu nyingine?
Kutokumweleza ni wivu huo, tu Kama hutaki kumweleza basi muuzie kwa hiyo bei yake aliyokupa Kama umeona akienda kwingine utapoteza!
 
Unamwambia "AENDELEE KUTAFUTA MWENYEWE".

BIASHARA NI KIPAJI AISEE!

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Hapana mkuu,
Jibu la endelea kutafuta mwenyewe sababu mmeshindwana itaonekana hujaridhika na una hasira.

Mimi nilipata mteja zaidi ya dk20 anashusha nguo after there akaniambia anhaa mbona bei kubwa nikamwambia boss nikishuka zaidi ya hapa nitaumia mimi akasema haya basi poa, nikamwambia karibu sana boss Kama hutojali naomba namba yako uwe unaangalia mzigo naopost.

Akaniachia namba after a week jamaa alirudi, in reality lazima uumie lakini upaswi kumuonyesha mteja, alinunua jinzi, tshirt, na sendo nikampa hesabu alitumia almost 68000.

Akasema bro nimependa sana unavyoongea, mpaka sasa ni mteja wangu sana, anaweza kuchukua nguo ikapelea pesa nikampa na anarudisha ndani ya muda alioahidi.
 
Huyo wako hajakuuliza aende wapi sehem nyingine wanapouza kwa bei nafuu?
 
Kuna siku Niko kwa Pharmacy yangu na Vijana wenzangu wanaoniuzia.

Akaja jamaa analalama kutokua sawa Kiafya.

Ilibidi nmsikilize Mimi , Kisha nikamwambia dawa zipo hapa, Bei yake ni kiasi fulan.


Jamaa akasema daaah Bei kubwa, ni wapi nitaweza zipata ?.

Nikamwambia , Mmhhh Kwa maeneo haya Sidhan ila ngoja nikuandikie .

Nikaandika majina yauongo ya zile dawa .


Alizunguka Kuanzia saa kumi jion mpaka saa 12 kasoro, akarudi tena Kwangu mie nimeshaondoka, jamaa wakanipigia simu, mteja wako karudi.

Nikamwambia mpeni dawa Fulani Fulani.




Kwenye Biashara , USITHUBUTU KAMWE KUMUONYESHA AU KUMUELEKEZA MTEJA KUA NENDA SEHEM FULAN UTAPATA KITU UNACHOTAKA .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…