Hivi mteja kama huyu unamjibuje?

[emoji23][emoji23][emoji23]wataje bhana.
Kuna mmoja aliweka oda ya kuchongewa picha mbao sasa kazi yake ishaisha ananiambia niiuze iv sasa nani atanunua picha mbao yenye sura ya mtu mwingine seriously [emoji848][emoji57]
View attachment 2845877
Karipoti kakuibia aje akute MOST WANTED akikuuliza mwambie nimewauzia police
 
Wakati mwingine kuwa tu mpole, yawezekana namna unavyomuhandle huyo mtu akaja akawa mteja wako mzuri tu.

Kuna siku niko sehemu kama mteja, akaingia mama mtu mzima akaulizia kitu ila wakashindwana bei. Akamuuliza muuzaji 'naweza pata wapi tena kama hii'? Muuzaji akamuelekeza vizuri tu, yule mama kwenda kule akakuta tofauti ya bei ni sh elfu tatu tu. Akarudi kwa yule wa kwanza na kumwambia nimekuta tofauti ya bei ni ndogo sana na kwa namna ulivyonitreat vizuri nimeaona ni busara nije nikuungishe tu wewe. Akanunua vitu karibia vya laki 3.
 
Kuna wateja wengine wanauliza kwa ustaarabu hadi watamani umsindikize kwa mpinzani wako lkn wengine pasua kichwa
 
Wee jamaa una roho mbaya, hufai kutumwa kumpelekea mgonjwa uji, uko tayari kunywa uji wa mgonjwa hata akifa hakuna shida.
 
Hivi mteja mpya ameulizia bidhaa ukamtajia bei mkaja mkashindwana bei anakuuliza sehemu nyingine ni wapi?

Wewe kama customer care unamjibuje!
Kama unajuwa sehemu nyingine unamtajia. Kama hujuwi unamwambia kweli.
As a customer care hutakiwi kudanganya hata kidogo. Kuwa mkweli ndipo utapojenga "reputation" ya biashara yako. Usiogope kumtaji hata kama ni washindani wako, kwani hukujipanda kuukabili ushindani?
 
Sio kwa mteja kichefuchefu yaani kashachefukwa kabla ajaja
 
Safi sana,wewe ni mfanyabiashara halisi
 
Roho mbaya tu,kwanza huyo mteja alikuwa mjinga wewe mfamasia unaniandikiaje dawa mm afu nikubali kizembe zembe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…