Hivi mtu akifa na hela zake ziko benki na Mpesa, tukiwa na cheti cha kifo tunaweza fuatilia?

Kuna taratibu za mirathi, kama marehemu kaacha wosia juu ya mgawanyiko wa mali basi itakuwa rahisi kuzipata, lakin zaid ya hapo utazungushwa sana, lakin pesa utazipata kama zilivyo

mkuu kuna uwezekano wa msimamizi wa mirathi kwa mfano kaka wa marehemu kwenda benk kutoa fedha za mirathi za watoto wa marehemu bila uwepo wao
 
mkuu kuna uwezekano wa msimamizi wa mirathi kwa mfano kaka wa marehemu kwenda benk kutoa fedha za mirathi za watoto wa marehemu bila uwepo wao
Kwa nini msimamizi wa mirathi awe kaka wa marehemu wakati mjane yupo na ana akili timamu?
 

mkuu kwanza ningependa kukipata kitabu chako kinacho husu sheria katika mfumo wa soft copy

pili ningependa kuuliza swali, kuna uwezekano wa kufungua faili la mirathi kwa mtu aliye fariki miaka kumi iliyopita licha ya kuwa msimamizi wa mirathi nae alisha kufa miaka kadhaa iliyopita ?
 
Nguvu yote hii sababu jamaa kakosea kuandika herufi moja tu???
Ifike mahali maswala mazito tuyape uzito wake , linalojadiliwa hapa ni kubwa kuliko makosa ya mwandiko
 
Huna hela wewe inawezekana mke wako ndio ana hela
Unawajua wanawake wewe?
 
Kwa nini msimamizi wa mirathi awe kaka wa marehemu wakati mjane yupo na ana akili timamu?

nadhani hii ni kutokana na shinikizi kutoka kwa ndugu wa upande wa marehemu na kutokuwepo kwa usawa au ukandamizajibwa kijinsia kwa upande wa wanawake
 

Hawana huruma ,mtu umefiwa na mpendwa wako bado unamachungu bado wakuzungushe kwenye hela ambayo siyo ya kwao inaboa sana
 
Mme unamficha mkeo kiasi hicho ? Si aibu kwa mkewe aliyebaki duniani na kuonyesha kuwa hakupendwa na mmewe duu [emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]
 
Hapo ni kufiwa na kufiwa na ujane ujane×1000 maumivu kuzidi, watu wanadhambi kubwa sana.
 
Watu wanapenda kuridhi mali za ndugu zao hata kama naye ana mke na watoto, hanaga huruma kabisa.
 
Kudos
 
mkuu kuna uwezekano wa msimamizi wa mirathi kwa mfano kaka wa marehemu kwenda benk kutoa fedha za mirathi za watoto wa marehemu bila uwepo wao

Ndio upo.. maana pesa anaekewa msimamiz wa mirathi.. cheque ikitoka
 
Ndio hivyo Mkuu; huwezi kuwa hakimu wa kesi ambayo una maslahi nayo. Msimamizi wa mirathi anatakiwa kuwa neutral.
dudus I disagree with you. Ndio maana nimekwambia nenda kajiridhishe. Sikutaka kubishana khs hili. Ila naona umenilazimisha niongee kwa urefu.

Nimeona in practice na nina uhakika ninachokisema. Mbona hata ukigoogle kesi za mirathi zipo nyingi tu utaona mke kapewa usimamizi? Hata hili umeshindwa kusearch? Na kama ni mwanafunzi wa sheria mbona precedent ziko nyingi tu ukisoma utaona?

Mke anaweza kuwa msimamizi wa mirathi ya mumewe. Kuwa na interest ktk urithi hakumfanyi yeye kuwa judge in her own case. Kumbuka mahakama ndio inateua sio yeye. Yeye anaomba tu usimamizi. Pili, baada ya kugawa kwa mujibu wa sheria anatakiwa kuifahamisha mahakama khs mgao huo na kufunga mirathi. Kwa hiyo bado yuko subject to mahakama.

Na ndio maana kama muda ukipita bila mirathi kukamilika au kufungwa, mtu au mrithi anaweza kwenda kuomba kutengua uteuzi wake msimamizi wa mirathi kwa ground ya kushindwa kusimamia mirathi vizuri ndani ya muda.
 
Mkuu umeongea points tupu aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msimamizi wa mirathi akiwa na barua/order toka mahakamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…