Kwanza poleni kwa msiba mkuu.
Fateni taratibu zifuatazo: Kwanza wanafamilia wakae kikao na kuandaa muhtasari wa kikao ambao pamoja na mambo mengine; utampendekeza msimamizi wa mirathi ya marehemu (endapo marehemu hakuacha wosia).
Baada ya hatua hiyo hapo juu, msimamizi wa mirathi ya marehemu aliyependekezwa atapaswa akathibitishwe na Mahakama (endapo hakuna pingamizi), ambapo atapewa 'hati ya usimamizi wa mirathi ya marehemu'. Kama marehemu alikuwa muislamu, mtaenda Mahakama ya mwanzo, kama marehemu alikuwa mkristo basi mtaenda Mahakama ya Wilaya/Mahakama ya hakimu mkazi, lakini kwa Mahakama ya Wilaya/Mahakama ya hakimu mkazi basi kuna maombi maalumu ambayo yanapaswa kuandaliwa na wakili na ndiyo yanapelekwa mahakamani, isipokuwa mkienda Mahakama ya mwanzo ambapo mtajaza tu fomu maalumu.
Viambatanisho muhimu ambavyo msimamizi wa mirathi aliyependekezwa kwenye kikao anatakiwa kuwa navyo ni cheti cha kifo cha marehemu na orodha ya mali za marehemu.
Bilashaka umenielewa mkuu. Karibu ununue Kitabu changu chenye jina; DONDOO MUHIMU ZA NAMNA YA KUKABILIANA NA KESI ZA ARDHI, JINAI, MADAI, MIRATHI NA NDOA HASA KWA WASOMAJI WASIO WANASHERIA NA WANASHERIA WACHANGA:SOMO FUPI LA SHERIA KWA VITENDO. Bei ni TZS 10,000 tu. Nipo Dodoma ila mikoani natuma pia. Au naweza kukutumia softcopy ukipenda. Aksante.