Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Huwa sielewe kwa kweli. Hasa nikiangazia teuzi za mawaziri. Unakuta leo waziri yupo wizara hii, kesho kateuliwa kule na keshokutwa kaletwa huku. Na kila unapomwona kwenye wizara mpya anaongea kama alikuwa hapo miaka kumi iliyopita.
Kuna wakati Bashungwa alikuwa waziri wa viwanda. Siku alialikwa pale Sheraton kukutana na wadau. Akaweka mikakati yake wee na kuunda timu ya ufuatiliaji na kuahidi kuona matokeo. Baada ya muda kama wiki 4 hivi akatolewa wizara hiyo, sikumbuki alienda wizara gani. Nilitamani sana kujua ni upi mwendelezo wa alichokianzisha. Najua kiliishia njiani tu japo lilikuwa wazo jema sana.
Tatizo ni hilo kila wizara. Yani mawaziri wamefanywa wanasesere. Aliyebaki na heshima wizarani ni Katibu Mkuu tu.
Sasa kilichonifanya kuandika haya ni kwamba natazama tbc hapa namwona Kijaji akitiririka na masuala ya maxingira utadhani alikuwa wizarrani hapo miaka mitano iliyopita. Wiki moja tu nyuma alikuwa waziri wa viwanda na alikuwa akitiririka kama alianzisha wizara. Wiki hiyohiyo Jery Silaa alikuwa wizara ya ardhi na ghafla akapelekwa Mawasiliano. Yani pale alipokuwa anaanza kuchanganya akatolewa. Hadi wananchi wakachukia. Kesho ukimsikiliza Silaa utadhani alikuwa mawasiliano miaka 7 iliyopita.
Tatizo hapa ni mteuzi kutuona wananchi ni maboya sana. Kwamba anaamka tu na pengine kwa maslahi binafsi anatengua uwaziri wa waziri fulani na kuhamisha huku na kule. Ni kama vile Raisi huwa na akilli za watanzania wote. Sasa nimefikiri nikaona yafuatayo;
1. Mteuzi awe na limit ya kuteua na kutengua. Mara mbili tu!
2. Waziri akae wizara husika angalau miaka mitatu bila kusumbuliwa na hamahama
3. Waziri akishindwa kudeliva hakuna haja ya kumhamisha. Ni kutengua tu
4. Waziri akideliva hakuna sababu ya kumhamisha. Ni kuvuruga malengo na kumharibia utendaji
5. Katibu mkuu wizara asitokane na uteuzi bali ushindani na ajira yake itokane na hekima za bodi