Hivi mtu akishateuliwa kiongozi huwa akili zake zinaongezeka mara dufu?

Waziri anaandaliwa cha kuongea na wataalamu, Wizara siyo Waziri pekee kuna wataalamu ambao wanamzidi mara 5 akili ake lakini wao hawaruhusiwi kuongea mbele ya camera
 
Kwa maneno mengine, mawaziri hata wasipokuwepo kila kitu kitaenda kama kinavyotakiwa..!
 
Bunge huwa linavunjwa tarehe 30-June mpaka November mwaka wa uchuguzi kwa muda wa miezi 5 Wizara huwa zinakuwepo bila Waziri na mambo yanaenda vizuri kuliko hata wakiwepo, pale mtendaji Mkuu ni Katibu Mkuu wengine wapo hapo kisiasa na hawana la maana.
 
Huwa sielewe kwa kweli. Hasa nikiangazia teuzi za mawaziri. Unakuta leo waziri yupo wizara hii, kesho kateuliwa kule na keshokutwa kaletwa huku. Na kila unapomwona kwenye wizara mpya anaongea kama alikuwa hapo miaka kumi iliyopita.

Kuna wakati Bashungwa alikuwa waziri wa viwanda. Siku alialikwa pale Sheraton kukutana na wadau. Akaweka mikakati yake wee na kuunda timu ya ufuatiliaji na kuahidi kuona matokeo. Baada ya muda kama wiki 4 hivi akatolewa wizara hiyo, sikumbuki alienda wizara gani. Nilitamani sana kujua ni upi mwendelezo wa alichokianzisha. Najua kiliishia njiani tu japo lilikuwa wazo jema sana.

Tatizo ni hilo kila wizara. Yani mawaziri wamefanywa wanasesere. Aliyebaki na heshima wizarani ni Katibu Mkuu tu.

Sasa kilichonifanya kuandika haya ni kwamba natazama tbc hapa namwona Kijaji akitiririka na masuala ya maxingira utadhani alikuwa wizarrani hapo miaka mitano iliyopita. Wiki moja tu nyuma alikuwa waziri wa viwanda na alikuwa akitiririka kama alianzisha wizara. Wiki hiyohiyo Jery Silaa alikuwa wizara ya ardhi na ghafla akapelekwa Mawasiliano. Yani pale alipokuwa anaanza kuchanganya akatolewa. Hadi wananchi wakachukia. Kesho ukimsikiliza Silaa utadhani alikuwa mawasiliano miaka 7 iliyopita.

Tatizo hapa ni mteuzi kutuona wananchi ni maboya sana. Kwamba anaamka tu na pengine kwa maslahi binafsi anatengua uwaziri wa waziri fulani na kuhamisha huku na kule. Ni kama vile Raisi huwa na akilli za watanzania wote. Sasa nimefikiri nikaona yafuatayo;

1. Mteuzi awe na limit ya kuteua na kutengua. Mara mbili tu!

2. Waziri akae wizara husika angalau miaka mitatu bila kusumbuliwa na hamahama

3. Waziri akishindwa kudeliva hakuna haja ya kumhamisha. Ni kutengua tu

4. Waziri akideliva hakuna sababu ya kumhamisha. Ni kuvuruga malengo na kumharibia utendaji

5. Katibu mkuu wizara asitokane na uteuzi bali ushindani na ajira yake itokane na hekima za bodi
Sababu kubwa ya teuzi ni ulaji. Sasa utakuta kila wizara ina kiwango chake cha ulaji. Kuna wizara zina ulaji mdogo na nyingine zina ulaji mkubwa. Rais anahanisha mawaziri ili kuwabadilishia ulaji. Mtu huwezi kukaa kwenye wizara yenye ulaji mdogo miaka yote ufe njaa. Rais sio mjinga. Anawahamisha mara kwa mara ili kila mmoja aonje aina fulani ya ulaji kwenye wizara mbalimbali.
 
Sababu kubwa ya teuzi ni ulaji. Sasa utakuta kila wizara ina kiwango chake cha ulaji. Kuna wizara zina ulaji mdogona nyingine zina ulaji mkubwa. Rais anahanisha mawaziri ili kuwabadilishia ulaji. Mtu huwezi kukaa kwenye wizara yenye ulaji mdogo miaka yote ufe njaa. Rais sio mjinga. Anawahamisha mara kwa mara ili kila mmoja aine aina fulani ya ulaji.
Una hoja usikilizwe
 
Waziri ni kiongozi, lakini anaweza kuwa mwanasiasa... Ila kiongozi makini hapendi siasa, akifanya ni kwa kulazimisha...
Mtu anayetokana na siasa ni mwanasiasa tu. La sivyo mtu kama huyo angebaki kwenye taasisi zingine za umma zisizo na teuzi na uhusiano na siasa. Kwa kitendo cha waziri atokane na ubunge, tayari mbunge ni mwanasiasa.
 
Kuna mwanasiasa in nature, mwingine ana act hata ukiangalia matendo yake unaona, either anapitia mgongo wa siasa ili afanikishe mipango yake...
 
Kitendo cha kutaka kufanikisha mipango yake tayari ni siasa, maana ndni ya siasa kuna propaganda na ulaghai
 
Huenda hatuelewani, ila unasema kweli 🤝, eg mimi nijoin na magaidi, lakini lengo langu ni kuvunja ngome ya kigaidi...
 
Huwa sielewe kwa kweli. Hasa nikiangazia teuzi za mawaziri. Unakuta leo waziri yupo wizara hii, kesho kateuliwa kule na keshokutwa kaletwa huku. Na kila unapomwona kwenye wizara mpya anaongea kama alikuwa hapo miaka kumi iliyopita.

Kuna wakati Bashungwa alikuwa waziri wa viwanda. Siku alialikwa pale Sheraton kukutana na wadau. Akaweka mikakati yake wee na kuunda timu ya ufuatiliaji na kuahidi kuona matokeo. Baada ya muda kama wiki 4 hivi akatolewa wizara hiyo, sikumbuki alienda wizara gani. Nilitamani sana kujua ni upi mwendelezo wa alichokianzisha. Najua kiliishia njiani tu japo lilikuwa wazo jema sana.

Tatizo ni hilo kila wizara. Yani mawaziri wamefanywa wanasesere. Aliyebaki na heshima wizarani ni Katibu Mkuu tu.

Sasa kilichonifanya kuandika haya ni kwamba natazama tbc hapa namwona Kijaji akitiririka na masuala ya maxingira utadhani alikuwa wizarrani hapo miaka mitano iliyopita. Wiki moja tu nyuma alikuwa waziri wa viwanda na alikuwa akitiririka kama alianzisha wizara. Wiki hiyohiyo Jery Silaa alikuwa wizara ya ardhi na ghafla akapelekwa Mawasiliano. Yani pale alipokuwa anaanza kuchanganya akatolewa. Hadi wananchi wakachukia. Kesho ukimsikiliza Silaa utadhani alikuwa mawasiliano miaka 7 iliyopita.

Tatizo hapa ni mteuzi kutuona wananchi ni maboya sana. Kwamba anaamka tu na pengine kwa maslahi binafsi anatengua uwaziri wa waziri fulani na kuhamisha huku na kule. Ni kama vile Raisi huwa na akilli za watanzania wote. Sasa nimefikiri nikaona yafuatayo;

1. Mteuzi awe na limit ya kuteua na kutengua. Mara mbili tu!

2. Waziri akae wizara husika angalau miaka mitatu bila kusumbuliwa na hamahama

3. Waziri akishindwa kudeliva hakuna haja ya kumhamisha. Ni kutengua tu

4. Waziri akideliva hakuna sababu ya kumhamisha. Ni kuvuruga malengo na kumharibia utendaji

5. Katibu mkuu wizara asitokane na uteuzi bali ushindani na ajira yake itokane na hekima za bodi
Ndio wenye Nchi hadi wanakufa.
 
Bunge huwa linavunjwa tarehe 30-June mpaka November mwaka wa uchuguzi kwa muda wa miezi 5 Wizara huwa zinakuwepo bila Waziri na mambo yanaenda vizuri kuliko hata wakiwepo, pale mtendaji Mkuu ni Katibu Mkuu wengine wapo hapo kisiasa na hawana la maana.
Umemjibu vzr waziri ni msemaji Kama Ali kamwe au Mangoma Ila utedanji unakuwa na watu efficiency ambo
Ndiyo...wa Serikali ya CCM wote wezi.

Sio kweli mkuu
 
Dadavua elimu ya uraia mkuu
Elimu ya uraia inamuwezesha mtu kutambua namna serikali inavyotenda kazi zake. Ni hapo ambapo mtoa mada angeelewa ni namna gani Waziri anaweza kumudu kuzielewa sera za wizara yake hata kama amedumu kwa muda mfupi.
 
Mfano tuchukulie aliyekuwa waziri wa ardhi, kwa hiyo baada ya kuwasikiliza wananchi hurudi nyuma kupokea nondo toka kwa watendaji kisha anaanza kutoa maamuzi?
Mchukulie Nape. Kwa kauli zile ilimaanisha kuwa jopo lake la washauri hawakufanya kazi yao? Kwa nini ape hakung'oka na watu wake?
No Nape ni case tofauti kwa sababu yeye ni mropokaji na alikuwa anaishi kimazoea yaani kujiona serikali ni yao kwa sababu wameanza kuingia serikalini miaka mingi na walirithi mambo ya uongozi kutoka kwa baba zao kwa hiyo inakuwa ni ngumu kushaurika kama mawaziri wengine.
 
Back
Top Bottom