Hivi mtu akishateuliwa kiongozi huwa akili zake zinaongezeka mara dufu?

Hivi mtu akishateuliwa kiongozi huwa akili zake zinaongezeka mara dufu?

Huwa sielewe kwa kweli. Hasa nikiangazia teuzi za mawaziri. Unakuta leo waziri yupo wizara hii, kesho kateuliwa kule na keshokutwa kaletwa huku. Na kila unapomwona kwenye wizara mpya anaongea kama alikuwa hapo miaka kumi iliyopita.

Kuna wakati Bashungwa alikuwa waziri wa viwanda. Siku alialikwa pale Sheraton kukutana na wadau. Akaweka mikakati yake wee na kuunda timu ya ufuatiliaji na kuahidi kuona matokeo. Baada ya muda kama wiki 4 hivi akatolewa wizara hiyo, sikumbuki alienda wizara gani. Nilitamani sana kujua ni upi mwendelezo wa alichokianzisha. Najua kiliishia njiani tu japo lilikuwa wazo jema sana.

Tatizo ni hilo kila wizara. Yani mawaziri wamefanywa wanasesere. Aliyebaki na heshima wizarani ni Katibu Mkuu tu.

Sasa kilichonifanya kuandika haya ni kwamba natazama tbc hapa namwona Kijaji akitiririka na masuala ya maxingira utadhani alikuwa wizarrani hapo miaka mitano iliyopita. Wiki moja tu nyuma alikuwa waziri wa viwanda na alikuwa akitiririka kama alianzisha wizara. Wiki hiyohiyo Jery Silaa alikuwa wizara ya ardhi na ghafla akapelekwa Mawasiliano. Yani pale alipokuwa anaanza kuchanganya akatolewa. Hadi wananchi wakachukia. Kesho ukimsikiliza Silaa utadhani alikuwa mawasiliano miaka 7 iliyopita.

Tatizo hapa ni mteuzi kutuona wananchi ni maboya sana. Kwamba anaamka tu na pengine kwa maslahi binafsi anatengua uwaziri wa waziri fulani na kuhamisha huku na kule. Ni kama vile Raisi huwa na akilli za watanzania wote. Sasa nimefikiri nikaona yafuatayo;

1. Mteuzi awe na limit ya kuteua na kutengua. Mara mbili tu!

2. Waziri akae wizara husika angalau miaka mitatu bila kusumbuliwa na hamahama

3. Waziri akishindwa kudeliva hakuna haja ya kumhamisha. Ni kutengua tu

4. Waziri akideliva hakuna sababu ya kumhamisha. Ni kuvuruga malengo na kumharibia utendaji

5. Katibu mkuu wizara asitokane na uteuzi bali ushindani na ajira yake itokane na hekima za bodi
Uko sahihi, Waziri anatakiwa ateuliwe kulingana na uzoefu wake katika sekta husika na pia asihamishwe hamishwe ndani ya muda mfupi, kama amevurunda wizara moja ni bora akaondolewa kabisa kuwa waziri. Tatizo ni kwamba mfumo wa siasa zetu hauzingatii merits bali ukada zaidi.
 
Kumbuka possibility ya kuwa rais 95% ni lazima atokee kwenye baraza la mawaziri. Ili uweze kuwa rais mzuri ni lazima uwe unaijuwa vzr serikali. Kwahyo kuwa badilisha nikuwafanya wa we na uwelewa mpana katika wizara mbalimbali. Au nyie ofisini kwenu hakuna job rotation?
Sio kweli, Rais anaweza kuwa anajua sekta moja tu na ikatosha kumfanya raisa mzuri. Kazi hasa ya Rais ni kusimamia watu watimize majukumu yao na kufanya maamuzi makubwa, sio kwenda kukakugua miradi, majengo na ofisi.
 
Sio kweli, Rais anaweza kuwa anajua sekta moja tu na ikatosha kumfanya raisa mzuri. Kazi hasa ya Rais ni kusimamia watu watimize majukumu yao na kufanya maamuzi makubwa, sio kwenda kukakugua miradi, majengo na ofisi.
Hv unaweza kusimamia kitu ambacho hauna kabisa idea nacho siutalishwa matango poli ?
 
Hv unaweza kusimamia kitu ambacho hauna kabisa idea nacho siutalishwa matango poli ?
Na hao wanaozungushwa kila leo.kwenye wizara wamekuwa na tija gani? Chukilia mfano Makamba na Nape
 
Na hao wanaozungushwa kila leo.kwenye wizara wamekuwa na tija gani? Chukilia mfano Makamba na Nape
Wabongo tunapenda kulalamika mno kama mtu anashindwa kuendesha familia ya watu wa nne itakuwa wizara au nchi?
 
Bunge huwa linavunjwa tarehe 30-June mpaka November mwaka wa uchuguzi kwa muda wa miezi 5 Wizara huwa zinakuwepo bila Waziri na mambo yanaenda vizuri kuliko hata wakiwepo, pale mtendaji Mkuu ni Katibu Mkuu wengine wapo hapo kisiasa na hawana la maana.
Kwahiyo unaweza kukuta hata mama yako chura kiziwi kichwani ni 0 ila anatembelea mawazo ya watu?
 
Ni kwamba ata sisi tunaolalamika kila siku wakati mwingine ata uwezo wakuendesha ofisi zetu wenyewe zenye mfanyakazi mmoja hatuna.
Inawezekana kweli iwe hivyo kwa kuwa rasilimali zinaweza kuwa haba, haswa fedha. Sasa waziri ana bajeti. Ana wasaidizi. Ana mamlaka. Ana media. Ana wataalam. Kwa nini ashindwe?
 
Back
Top Bottom