Hivi mtu akiua mtu aliyemfumania na Mke/Mume sheria inasemje?

Hivi mtu akiua mtu aliyemfumania na Mke/Mume sheria inasemje?

Back up! back up!

We've been hit

Man down, I repeat man down.

Do you copy?

Over??
Huwa napenda sana movie za kikomando...

Nafurahiaga sana kile kiingereza wanachoongea wanajeshi wa Marekani....(kwenye movie)

Asante mkuu kwa kunikumbusha mbali
 
Ni kosa Kama kosa lingine lkn defence unaweza sema ni provocation ingawa ina vigezo vyake kosa likawa manslaughter badala ya murder
 
Kama aki proof provocation anaweza kufungwa miaka 2,5au judge atavyoona
 
Unaruhusiwa kuuwa kama utamfumania mke wako, right on time hiyo inaitwa kitaalamu FLAGRANTE DELICTO,,, Na inakuwa right away , yani unauwa hapohapo .

It means that, you have to act on the sport without delay, or hesitate and it could be one of your valuable defence before the court of law.

........................

Screenshot_20210211-155000_Chrome.jpg
 
Mimi nataka kuuliza leo, Haya matukio ya kuuana kwenye mahusiano hasa fumanizi yamekuwa mengi sana siku hizi. Hivi karibuni tu January 04 ya mwaka huu tulisikia jamaa mmoja Huko Chunya Mbeya amemua mtu aliyemfumania na mke wake ndani ya nyumba kwenye chumba anacholala akifanya mapenzi na mke wake.

Nadhani kila mtu anajua maumivu ya kusalitiwa kwa wote mume na mke ikiwa ni kwenye mahusiano au ndoa. Kitendo cha mtu kumkuta anafanya mapenzi na mke wako, ndani kwako, kwenye chumba chako, kwenye kitanda chako ebu imagine ni maumivu makali kiasi gani utakuwa nayo? Na ndipo sasa inatokea hapa mtu anaua bila kukusudia.

Naamini kabisa hapa wengi wanauwa bila kukusudia ni kutokana na stuation anayoipata mtu kwa wakati huo sehemu ya tukio. Ni wachache sana amkute mtu anafanya mapenzi na mkeo/Mumeo amwache tu aondoke bila kashi kashi wala kumgusa mtu huyo aisee.

Na je sheria ya ugoni ikoje hapa mtu ukimpeleka mahakamni ametembea na mkeo na akakana ushaidi huwa unapatikanje? na je ikidhibitika huwa kuna kifungo au faini kwa huyo mtu. Watu wengi wanachukua sheria mkononi pengine sheria ya ugoni haimwajibishi vizuri mtuhumiwa kiasi cha kupunguza maumivu ya mlalamikaji au tatizo nini?.

Pamoja na yote hayo inakuwaje mtu aliyeua katika stuation hiyo ahukumiwe kama muuaji wa kukusudia maana ankuwa amesababishiwa hisira za kuua.

Nawasilisha.

Sheria inasema kuwa ni kosa kusababisha kifo cha mwingine. Sasa ukiua katika fumanizi utashtakiwa kwa Kosa la mauaji kwa kukusudia labda ukiweka utetezi wa 'provocation' unaweza ukakusaidia kidogo na kubadili mashtaka na hatia yako toka 'kuua kwa kukusudia' ambayo adhabu yake ni kifungo cha Miaka 30 hadi 'kuua pasipo kukusudia' ambapo adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka 30.
Sasa hadi hiyo difense yako ya provocation ifanye kazi ni lazma ipitishwe katika kipimo ili kuithibitisha, haitakubaliwa kuwa umfumanie mkeo temeke halafu uende kwa jirani kuchkua panga ndio uje kumchinja hii haitakubalika.
 
Ukijitahidi utatoka murder kwenda manslaughter, hapo miaka 10 itakuhusu jela. Ukirudi uraiani mke ashachakazwa na wajuba na wewe ukilegea jela unatoka hauna marinda
 
Njia rahisi ni kudai fidia ( fungua civil case)
Kama huna uwezo wa kuvumilia fanya maombi ya talaka kwa kuwa ushahidi upo mahakama ikijirizisha u will be awarded
 
Wanasheria uchwara mtatumaliza.

Makanjanja na vishoka mmeshika hatamu kweli kweli.
 
Unaruhusiwa kuuwa kama utamfumania mke wako, right on time
Man, please!

Usifanye mambo ya upotoshaji mitandaoni.

This is a mistake!

Kama hujui jambo ni bora ukanyamaza.

Hii ni hatari. Utawatia watu matatizoni kwa ujuaji wako usio na faida.
 
Sasa hapo kisheria kosa ni lipi? Kutembea na mke wa mtu ama mke wa ndoa kuchepuka?
 
Ngoja nichangie kidogo
Kuua ni kosa na kuna adhabu kisheria kifungu cha 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya 2019.

Sasa inakuwaje umemfumania mkeo/mmeo hasira zimekupanda ukaua!?? Nadhani ndo lengo la mleta hoja.

Basi tujadili pamoja

Moja wapo ya utetezi unaoweza kukupunguzia adhabu au kubadilisha kosa kutoka kuua mpaka kuua bila kukusudia ni utetezi wa PROVOCATION kiswahili chake sijui nisemeje (magu kasema tutumie kiswahili) utetezi huu unaweza kukupunguzia adhabu.
Kesi ya Mwamwindi wengi mnaifahamu mahakama ilitoa vigezo vya utetezi huu kumsaidia mtu.

Mojawapo ni mtu anayeua under provocation lazima awe amechokozeka kweli na ameua kutokana na kukasirishwa kweli.
Mfano: umemfumania mkeo basi palepale unampiga ngumi au na stuli iliyopo chumbani unaua. Basi uko salama

Vinginevyo umemfumania mkeo ukaenda store ukachukua shoka ukarudi ndani na kumkata mkeo na mgoni wako mpaka mauti basi wewe umekusudia.

NB: utetezi huu utakupungizia adhabu tu hauwezi kukuondolea kosa

Kama hatujaelewana karibu tuelimishane
 
Back
Top Bottom