Hivi mtu anakuwa katika hali gani ya akili hadi anakubali kuolewa mke wa tatu, wa nne nk?

Wote wanaovuta sigara ni wajinga wasio na taarifa??
Swali hili linakuhusu wewe unayehubiria watu katika maamuzi ya maisha yao binafsi kama ni wajinga wasio na taarifa.
 
Nimesha critique hizi habari kwa kutofautisha polygamist communitues na polygamy as a personal choice kwa mtu.

I am not advocating for everybody to be polygamous.

Huelewi wapi?
Hii ni hatari kisayansi
 
Kwanza kabisa mpaka sasa, baada ya mara tatu kukuelezea, hujaelewa tofauti ya polygamy kama personal choice na polygamy kama a societal thing. Hujaelewa. Sio tu hujaelewa, hujafanya hata jitihada ya kuelewa.

Pili, hujaelewa kuwa, hata baada ya matatizo yooote, mtu bado ana uhuru wa kuchagua maisha yaje yaweje. Na mtu kuchagua kitu unachoona wewe kibaya haina maana hana taarifa. Inawezekana mna priorities tofauti.

Wewe inawezekana ukawa unataka kuishi maisha marefu ya kula mlo mmoja kama Profesa Janabi, mwingine akaona ni ujinga kuishi maisha marefu ambayo huwezi kula unachopenda, hivyo yeye anataka kuishi maisha hata kama mafupi, lakini anakula anachotaka.

Tatizo liko wapi?

Ndiyo maana kuna madaktari wengi wanajua madhara ya pombe na sigara vizuri kuliko wewe. Wanaweza kukuelezea biochemical reactions za ethanol zinazotokana na kunywa pombe, ndani ya mwili wako.

Lakini wanakunywa pombe sana, kwa maamuzi yao. Hiyo ni haki yao. Na wala usijipe ukiranja wa kuwahubiria kama mtu unayeelewa haya mambo kuliko wao. Wanaweza kukupa lecture ya kuvunja aina zote za sukari kuanzia xylitol, erythritol, sorbitol, maltitol, mannitol, isomalt, and lactitol.

Sasa kufikiri kwamba watu wanaokunywa pombe hawajui madhara ya pombe ni kuwa condescending and patronizing tu.
 
Weka research report unayo elezea sio poroja. Pia kuna research inaonyesha wanawake wanao kaa mda mrefu bila mwanaume wananafasi kubwa ya kusumbuliwa na fibroid na saratani ya maziwa. Na mara nyingi hupoteza kabisa hali ya kujiamini. Huwa na msongo wa mawazo mda wote.
 
Ni jambo jema umekubali watu wanaweza kufanya mambo pamoja na kutokuwa na faida yoyote mfano kuvuta sigara, mjadala wa pombe ni mwingine na una debates zake.

Unafikiri ndoa za mitaala zina faida yoyote kisayansi au kijamii kwa binadamu?
 
Ni jambo jema umekubali watu wanaweza kufanya mambo pamoja na kutokuwa na faida yoyote mfano kuvuta sigara, mjadala wa pombe ni mwingine na una debates zake.

Unafikiri ndoa za mitaala zina faida yoyote kisayansi au kijamii kwa binadamu?
But that (faida) is not the point. Huelewi wapi?

Uhuru wa mtu kuamua mambo yake umepita habari za faida.

Ndiyo maana kuna madaktari wanaojua madhara ya sigara na pombe kuliko wewe, na wanavuta sigara na kunywa pombe, na hatuwakatazi wala kuwahubiria kuhusu jambo hili.

Huelewi wapi?
 
Wanawake WA siku hizi mnaendekeza wivu kupitiliza ndo maana mnaongea hivi
Enzi za mababu zetu mbona hayo mambo yalikuwa freshy tu
Sahivi tunauana mkuu,Bora tungekuwa wastaarabu...unakuta mwenzio anakamdomo shuu... kwanini usipige🤨
 
Tatizo lako ni polygamy au Uislam? Naona umetolea mfano nchi ya Uturuki, na hao wanawake wa Uturuki uliowahoji sijui ni wangapi? Mbona hujazungumza mifano ya mababu zako wa kiafrika na jamii zengine nyingi zinazofanya polygamy? Why nchi ya kiislam? Lengo lako nini?


Halafu eti mwanamke msomi unamshangaa kuolewa mke tatu au wa nne ila humshangai akiwa mchepuko akiziniwa na watu, hushangai mwanamke msomi anayefanywa kuwa mchepuko wa kumi au hata wa ishirini! Mwanaume kuoa wake wanne anaowahudumia unashangaa ila hushangai mwanaume mwenye vimada 20, hushangai mwanaume anayewazalisha wanawake wengi watoto kiholela bila kuwaoa! Sio ajabu hushangai ushenzi wa "hit and run"! Si ajabu hushangai ushenzi wa "hookup culture"!

Polygamy inakushangaza ila haikushangazi baadhi ya vijana wa kiume ikiwemo baadhi ya wasomi kukidhi matamanio yao kiholela huku wakiwa hawataki majukumu!

Baadhi yenu wasomi mnapinga mitaala ila mnaunga mkono "open relationships" eti maendeleo na usasa!?

Ajabu sana!
 


"Sayansi" inatumika kupotosha mengi. Ujinga mwingi unasemwa kwa jina la sayansi. Kwangu mimi ukisema "sayansi" sio kwamba ndio ukweli halisi ambao hauwezi kuhojiwa kabisa.

Ukiachana na hivyo, kuna mambo ambayo hata sio katika hiyo "sayansi" (hayakubaliani na vigezo vyake) ila yanasemwa kama "sayansi".
 
Ni heri nisiolewe kabisa kuliko kuwa mke mwenza
 
Wanawake bana akili zenu mnazijua wenyewe unakataa kuwa mke wa pili ila yuko tayari kuwa mchepuko wa mume wa mtu au singo maza.
 
Kuoa na kuolewa ni jambo la hiyari sio la lazima hata dini hailazimishi unaweza kuo au kuolewa na pia unaweza kukataa kuoa au kuolewa mpaka unakufa sio dhambi

Kama wewe hautaki kuolewa mke wa pili au watatu au wa nne wenzanko wanataka
 
Hatuwezi kujua. Angekuwepo mfalme Suleiman angekujibu hasa mke wake wa 700 angetoa jibu zuri.
 
Kama wewe hautaki kuolewa mke wa pili au watatu au wa nne wenzanko wanataka
Hao wanaotaka ndio tunauliza hapa, wana akili ya namna gani? Wewe binti yako au dada yako akisema amapata mchumba, mume wa wengine na yeye ataolewa mke wa tatu utajisikiaje, chereko chereko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…