Hivi mtu anakuwa katika hali gani ya akili hadi anakubali kuolewa mke wa tatu, wa nne nk?

Kwa nini umeleta hii mada wakati huu ambao kule jumba kubwa kuna mtu yeye ni wanne?
 
Mimi siyo akili gani, nikipenda mtu nilivyo na wivu siwezi kwa kweli. Yaani najua sasa hivi yuko analala huko, mbona usiku utakuwa mrefu sana.
Baby kwako sina haja yakuongeza mwengine sitaki kukutia stress maana kwanza unajitosheleza au sio baby wangu..??
 
Uzuri wewe sio mwanamke,pili usipingane na dini
 
Bado hujaelewa saikolojia ya Wanawake wewe.
WAliooa ndio Rahisi kuoa kuliko ambaye hajaoa
 
Mwanaume unalalamikaje mwanamke kuolewa mke wa pili ama wa 3?

Yaani wewe unaumia wanawake kuolewa mke wa pili ama wa 3?

Kwa hiyo unaona bora aendelee kua mchepuko kuliko kua na mwanaume wa uhakika wa kumhudumia na kumstiri?
Inafikilisha sana hii
 
Ila wewe unapenda
kuwa mchepuko wa mume wa mwanamke mwenzio siyo?
 
Mwanamke ni kiumbe dhaif Hana maamuzi ni wa kupelekwa tuuuu, na kupangwa
 
Acha gubu bibie
 
Lakini ni vema binti kuzaa na mume wa mtu au kuwekwa kimada na mume wa mtu lakini si sawa binti kuolewa ndoa ya wake wengi, hivi vitu hua vinanifikirisha sana,
Unakuta mtoa mada ana mchepuko wake kampangishia nyumba na kumpa matunzo yote ila anawashangaa wanaooana ndoa za wake wengi.
 
Wewe tena, humu una mababy kibao ndiyo sikuwezi kabisa. πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
Hapana bhana mi sina yoyote nimekuchagua wewe tu!, nilikuwa nakufuatilia toka zamani nikaona huna mambo mengi hivyo leo nakutangaza wewe ndio baby wangu wa humu!, asitokee yoyote kukushika wala kukutaka sawa Bantu wangu.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…