Hivi mtu anaweza kushitakiwa kwa kutembea na Mke wa mtu?

Hivi mtu anaweza kushitakiwa kwa kutembea na Mke wa mtu?

Kifaru86

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2017
Posts
1,734
Reaction score
3,822
Hivi ikitokea umemfumania mke wako akiwa na mtu mwingine unaweza kumshitaki Mahakamani mtuhumiwa kwa kutembea na mke wako wakati mke wako anajijua ni mke wa mtu?

Hivi kesi ikienda Mahakamani hapo ni nani mwenye makosa ambae anaweza kushitakiwa?

Naombeni majibu wana JF maana kuna jamaa hapa nataka kumuelimisha maana yamemkuta anataka kwenda Mahakamani.
 
Umeshasema mke wa mtu. Uliyemfumania nae ni nyani au mti si ni mtu basi na yeye ni mke wake. Maana mke wa mtu ni mtu.

By the way karibu chai
 
Kama hajamkamata live, hakuna kesi hapo. Ila kama alimkamata live na mashahidi wakiwepo, police wetu wajuvi sana. Wanaweza kuibuka na case kama "tresspassing" au "kujimilikisha mali ya mtu kinyume cha sheria" au hata "uchochezi unaolenga kuvunja ndoa halali"🙂
 
Ndio ni kosa kisheria, hii uitwa ugoni, na hasa wewe mwizi ukikamatwa live, adhabu yake yaweza kua fine au kifungo vile vile, kwa mujibu wa sheria ya ndoa... lakini sheria imetilia mkazo sanaa kwenye kumuoa au kuishi na mke wa mtu ambae uenda ametengana tu na mmewe bila talaka au wamekorofishana tu, ambapo Kifungu cha 152 ( 1) cha sheria ya ndoa kinakifanya kitendo cha kufunga ndoa na mwanamke ambaye bado ndoa yake haivunjwa kisheria kuwa ni kosa.

Kifungu kidogo ( 1 ) na ( 2 ) kinasema kuwa mme aliyemuoa mke huyo na mke mwenyewe aliyeolewa wote kwa pamoja wanahesabika kutenda kosa hili. Na kifungu kidogo cha ( 3 ) kinasema kuwa hao wote wawili wakithibitika kutenda kosa hilo basi adhabu yao ni kifungo kisichozidi miaka 3 jela.
 
Naona Mzee Ushachapiwa Mke unajiliwaza Eti unataka kumshauri Mtu!
Mtoto wako ukimlisha akashiba hutasikia anakuabisha kwa kula kula kwa Majirani!

'Mlishe' Mkeo atosheke ndio dawa ya kuchapiwa sio kutafuta vifungu vya Sheria kwenda kufunga Watu
 
Acha kujibu kama unapokea rushwa huko sisiyemu! Unajibujibu tu. Subiri wataalam wa sheria wakupe faida za usomi.
 
Kama hajamkamata live, hakuna kesi hapo. Ila kama alimkamata live na mashahidi wakiwepo, police wetu wajuvi sana. Wanaweza kuibuka na case kama "tresspassing" au "kujimilikisha mali ya mtu kinyume cha sheria" au hata "uchochezi unaolenga kuvunja ndoa halali"🙂
Mwenye kosa hapo ni anaechepuka huku anajua anamume .au anamgonga bilakujia kama huyu nimke wamtu.huoni mwanaume anaweza kusema mm sikujua kama nimke wamtu.
 
Mwenye kosa hapo ni anaechepuka huku anajua anamume .au anamgonga bilakujia kama huyu nimke wamtu.huoni mwanaume anaweza kusema mm sikujua kama nimke wamtu.
Ndo maana nikasema mwanamke anajijuaa kabisa Mimi ni mke wa mtu na Na nimeapa sitokuja kusaliti ndoa yangu.

Halafu mwanamke ukamuua kutoka nje kutembea na mtu mwingineee halafu mwanaume ukatokea umemfumania mke wako na mwanaume mwingineee.

Halafu unamfungulia mashitaka mwanaume mwingine mahakamani sasa hapo mwenye kosa ni naniiiiiii.

Je ikitokea mwanamke wako umemfumania raundi karibia kumi tofauti tofauti na wanaume tofauti INA maana UTAKUWA kila siku wee ni mtu wa kufungulia watu kesi
 
Labda kama ilibadilishwa lakini kisheria ukifumwa na mke wa mtu fine elf 2 tu (2000). Ndomaana watuwalikata tama kufungua mashitaka. That's why case kama hizi sio nyingi makamani
 
Ameuliza jambo zuri. Ila weye unalichukulia poa tu. GIVING OUT A STUPID ANSWER WILL GET YOU A STUPID QUOTATION!
Hivi unaposema kuwa 'umetembea na mke wa mtu' au mtu ametembea na mke wako kuna suala la kuuliza kuhusu kosa hili? Dini, mila,desturi na Sheria zimekwenda wapi hata usijue la kufanya?
 
Hivi unaposema kuwa 'umetembea na mke wa mtu' au mtu ametembea na mke wako kuna suala la kuuliza kuhusu kosa hili? Dini, mila,desturi na Sheria zimekwenda wapi hata usijue la kufanya?
Hayo maswali yako ndiyo yanahitajika kuingizwa kwenye mjadala. Tatizo weye ulitaka kuua mjadala mzuri usiendelee.
 
Back
Top Bottom