Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Heshima yako, Rafiki mtoto kula kwa jirani haina maana kuwa kwao hakuna lishe nzuri, watoto hupenda ladha tofauti tofauti, mtapika pilau anakataa halafu anaenda kula ugali na dagaa beche kwa jirani, Hakuna formula katika mambo ya kuchapiana.Naona Mzee Ushachapiwa Mke unajiliwaza Eti unataka kumshauri Mtu!
Mtoto wako ukimlisha akashiba hutasikia anakuabisha kwa kula kula kwa Majirani!
'Mlishe' Mkeo atosheke ndio dawa ya kuchapiwa sio kutafuta vifungu vya Sheria kwenda kufunga Watu
Mathalan mke huyo ameondoka kwa mumewe na anaishi kwao na kwamba hata baada ya suluhu amekataa kurudi. 1. Bado sheria itahesabu kuwepo kwa ndoa?Ndio ni kosa kisheria, hii uitwa ugoni, na hasa wewe mwizi ukikamatwa live, adhabu yake yaweza kua fine au kifungo vile vile, kwa mujibu wa sheria ya ndoa...
Ni kweli mimi ni zero brain na wewe ni genius. Ungeuelewa vizuri ule msemo pengine ungesema vingine.Wewe ndiyo umeonekana mjinga....ukijiona una akili sana basi kuna wengine tunakuona ni zero brain.... Hujalazimishwa kuchangia acha wanaojua tumshauri
Mathalan mke huyo ameondoka kwa mumewe na anaishi kwao na kwamba hata baada ya suluhu amekataa kurudi. 1. Bado sheria itahesabu kuwepo kwa ndoa?
2. Ni hatua zipi zichukuliwe ili mwanandoa aweze kuoa endapo kanisa/msikiti ukikataa kuvunja ndoa hyo hadi mmoja wao apatwe na umauti
3. Je, ni kosa mke kurudi kwao na wazazi wake kumpokea bila kuwepo na mashauriano na mumewe?
Akikujibu nitag [emoji3][emoji3]hivi mwanafunzi ana alama gani? Hivi mwanafunzi anaweza chukuliwa hivi hivi tu kama box Vila kuwa na utashi?
Sheria ipo ya kiserikali ya ugoni,lakini sheria ya kitaani ndio inapendwa zaidi..unafumuliwa marinda huku unarekodiwa..basi kesi imeishaHivi ikitokea umemfumania mke wako akiwa na mtu mwingine unaweza kumshitaki Mahakamani mtuhumiwa kwa kutembea na mke wako wakati mke wako anajijua ni mke wa mtu?
Hivi kesi ikienda Mahakamani hapo ni nani mwenye makosa ambae anaweza kushitakiwa?
Naombeni majibu wana JF maana kuna jamaa hapa nataka kumuelimisha maana yamemkuta anataka kwenda Mahakamani
UMETUDANGANYABelieve me!
More than 90% ya Wanawake wanachepuka kwa mapungufu ya Mwanaume
More than 90% ya Wanaume wanachepuka kwa attraction ya Nje sio mapungufu ya ndani
Huu ni utafiti usio rasmi usije kuanza kuniuliza mambo ya literature review na Conceptual framework
Ushahidi wa mazingira utathibitisha hili,haiwezekani umechepuka na mke wa mtu ambaye mnaishi mtaa mmoja dheni useme hukujua huyu ni mke wa mtuMwenye kosa hapo ni anaechepuka huku anajua anamume .au anamgonga bilakujia kama huyu nimke wamtu.huoni mwanaume anaweza kusema mm sikujua kama nimke wamtu.
Japo post ni ya mda, lakini kuweka kumbukumbu sawa, ulichokieleza ni tofauti na kilichoulizwa. Pili umepotosha kidogo kwa kusema "ndio" kwa Tanzania bara Hamna kosa la "ugoni".Ndio ni kosa kisheria, hii uitwa ugoni, na hasa wewe mwizi ukikamatwa live, adhabu yake yaweza kua fine au kifungo vile vile, kwa mujibu wa sheria ya ndoa... lakini sheria imetilia mkazo sanaa kwenye kumuoa au kuishi na mke wa mtu ambae uenda ametengana tu na mmewe bila talaka au wamekorofishana tu, ambapo Kifungu cha 152 ( 1) cha sheria ya ndoa kinakifanya kitendo cha kufunga ndoa na mwanamke ambaye bado ndoa yake haivunjwa kisheria kuwa ni kosa.
Kifungu kidogo ( 1 ) na ( 2 ) kinasema kuwa mme aliyemuoa mke huyo na mke mwenyewe aliyeolewa wote kwa pamoja wanahesabika kutenda kosa hili. Na kifungu kidogo cha ( 3 ) kinasema kuwa hao wote wawili wakithibitika kutenda kosa hilo basi adhabu yao ni kifungo kisichozidi miaka 3 jela.
Hahahahaha wewe umenichekesha, nikusaidie tu ugoni kisheria unaitwa adultery, na mwezi uliopita nilikua mahakamani kwa kesi hii wilaya ya Tandahimba, Mtwara, Tanzania bara... unapaswa kujua kua sisi tuko ktk mfumo wa common law ambao una turuhusu kukopa sheria au kutumia maamuzi ya mahakama kuu na mahakama ya rufaa kama sheria.Japo post ni ya mda, lakini kuweka kumbukumbu sawa, ulichokieleza ni tofauti na kilichoulizwa. Pili umepotosha kidogo kwa kusema "ndio" kwa Tanzania bara Hamna kosa la "ugoni".
Mkwala mbuzialaaniwe yeyote ajuae kuwa fulani ni mke wa mtu na akamfata kwa kujua udhaifu wake na kumla kwa kutaka sifa kwa wajinga wenzake. wallah atakaejua udhaif wa mke wang akautumia na kumrubuni ili ampate!!
nitamsamehe kabisa ila hawez sahahu jinx atakavyoanza historia mpya ya maisha yake.. huenda hakuna na elim ya kutosha juu ya dini yake na hekma kwa wqke za watu hivyo nitamfunza kwa muda mchache sana. sijaribiwi na usilifanye jambo usilolijua uzito wake baadae
Zipo nyingi tu, hizi ndio kesi za WagogoHivi hakuna mf wa kesi kama hizi zilizohukumiwa?
Well narrated Counsel.1. Hakuna kosa lolote la jinai na polisi hawatausika kwa lolote isipokuwa kusaidia kutendeka kwa makosa ya jinai katika hatua nzima ya fumanizi kama SHAMBULIO, KUJERUHI MAUAJI na mengine
2.Kosa la fumanizi ni kosa la madai ambapo mfumaniaji atadai fidia ama TALAKA kwa kufuata taratibu zilizowekwa na sheria ya ndoa kama ataithibitishia mahakama kuwa kitendo hicho kimemfanya akose uvumilivu wa kuendelea kuishi naye
3. Ndoa ni mkataba kama mkataba mwingine ambapo kila mmoja anatoa ahadi za kutokuvunja ahadi ya tatu kwa kumruhusu mtu wa tatu (third party) kuingilia matunda ya ndoa ikiwemo gegedo sasa kama mmoja wapo atakengeuka na akakamatwa (in flagrante delicto) na muhusika mkuu ama wa karibu anayetambuliwa nasheria ya ndoa basi itakuwa ni kigezo cha kuomba talaka.
4. Kwa kuwa ndoa ni mkataba wa hiari ( kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha sheria ya ndoa) na kwa kuwa sehemu moja wapo ya masharti muhimu ya ndoa ni kutokutoka nje ya ndoa, basi pale mmoja wapo anapofanya hivyo atakuwa amevunja mkataba na kwa kuwa kuanzia sheria za ndani hadi sheria za kimataifa ikiwemo ( International Covenant on Civil and Political Rights)
zinakatazwa mtu kuwekwa mahabusu kwa makosa ya madai, basi polisi hawatamuweka mahabusu kwa kosa hilo labda wanaweza kumtunza tuu kwa usalama wake ile heat of passion ya mfumaniaji ipoe na kuwashauri wafuate taratibu za kimadai kuhusiana na masuala ya ndoa ikiwa ni pamoja na kuanzia kwenye baraza la usuluishi la kata