Hivi mtu anaweza kushitakiwa kwa kutembea na Mke wa mtu?

Abunwasi,

Wewe ndiyo umeonekana mjinga....ukijiona una akili sana basi kuna wengine tunakuona ni zero brain.... Hujalazimishwa kuchangia acha wanaojua tumshauri
 
Naona Mzee Ushachapiwa Mke unajiliwaza Eti unataka kumshauri Mtu!
Mtoto wako ukimlisha akashiba hutasikia anakuabisha kwa kula kula kwa Majirani!

'Mlishe' Mkeo atosheke ndio dawa ya kuchapiwa sio kutafuta vifungu vya Sheria kwenda kufunga Watu
Heshima yako, Rafiki mtoto kula kwa jirani haina maana kuwa kwao hakuna lishe nzuri, watoto hupenda ladha tofauti tofauti, mtapika pilau anakataa halafu anaenda kula ugali na dagaa beche kwa jirani, Hakuna formula katika mambo ya kuchapiana.
 
Ndio ni kosa kisheria, hii uitwa ugoni, na hasa wewe mwizi ukikamatwa live, adhabu yake yaweza kua fine au kifungo vile vile, kwa mujibu wa sheria ya ndoa...
Mathalan mke huyo ameondoka kwa mumewe na anaishi kwao na kwamba hata baada ya suluhu amekataa kurudi. 1. Bado sheria itahesabu kuwepo kwa ndoa?

2. Ni hatua zipi zichukuliwe ili mwanandoa aweze kuoa endapo kanisa/msikiti ukikataa kuvunja ndoa hyo hadi mmoja wao apatwe na umauti

3. Je, ni kosa mke kurudi kwao na wazazi wake kumpokea bila kuwepo na mashauriano na mumewe?
 
Hii hushtakiwi ila unahukumiwa direct tena hukumu yake bora ufe[emoji84] [emoji83] [emoji196] [emoji196] [emoji13]
 
1. Hakuna kosa lolote la jinai na polisi hawatausika kwa lolote isipokuwa kusaidia kutendeka kwa makosa ya jinai katika hatua nzima ya fumanizi kama SHAMBULIO, KUJERUHI MAUAJI na mengine

2.Kosa la fumanizi ni kosa la madai ambapo mfumaniaji atadai fidia ama TALAKA kwa kufuata taratibu zilizowekwa na sheria ya ndoa kama ataithibitishia mahakama kuwa kitendo hicho kimemfanya akose uvumilivu wa kuendelea kuishi naye

3. Ndoa ni mkataba kama mkataba mwingine ambapo kila mmoja anatoa ahadi za kutokuvunja ahadi ya tatu kwa kumruhusu mtu wa tatu (third party) kuingilia matunda ya ndoa ikiwemo gegedo sasa kama mmoja wapo atakengeuka na akakamatwa (in flagrante delicto) na muhusika mkuu ama wa karibu anayetambuliwa nasheria ya ndoa basi itakuwa ni kigezo cha kuomba talaka.

4. Kwa kuwa ndoa ni mkataba wa hiari ( kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha sheria ya ndoa) na kwa kuwa sehemu moja wapo ya masharti muhimu ya ndoa ni kutokutoka nje ya ndoa, basi pale mmoja wapo anapofanya hivyo atakuwa amevunja mkataba na kwa kuwa kuanzia sheria za ndani hadi sheria za kimataifa ikiwemo ( International Covenant on Civil and Political Rights)

zinakatazwa mtu kuwekwa mahabusu kwa makosa ya madai, basi polisi hawatamuweka mahabusu kwa kosa hilo labda wanaweza kumtunza tuu kwa usalama wake ile heat of passion ya mfumaniaji ipoe na kuwashauri wafuate taratibu za kimadai kuhusiana na masuala ya ndoa ikiwa ni pamoja na kuanzia kwenye baraza la usuluishi la kata
 
Ni ujinga Mwanaume kuaza kushughulika na Mwanaume mwenzako nje eti kisa amekuchapia Mke wako haliyakuwa huyo Mkeo ameenda kumvulia Pichu mwenyewe huku akijuwa yakuwa yupo kwenye Ndoa.., Malizana na huyo mlieingia kwenye huo Mkataba!!!
 
Wewe ndiyo umeonekana mjinga....ukijiona una akili sana basi kuna wengine tunakuona ni zero brain.... Hujalazimishwa kuchangia acha wanaojua tumshauri
Ni kweli mimi ni zero brain na wewe ni genius. Ungeuelewa vizuri ule msemo pengine ungesema vingine.
 

Well, Mkuu ndoa ni zao la sheria, ata mwisho wa ndoa ni lazima uvunjwe kisheria, ndoa itakoma tu pale mmoja wapo atakapo kufa au mwingine akapotea muda usiojulikana then ikafanyika pressumption of death na kubwa kabisa ni hii ya sheria mahakamani.

Kama bibie atakua karudi kwao still ndoa iko pale pale, na kosa litakuwepo pale pale endapo akiolewa na ndoa kwa mtu mwingine bila kuivunja ile ya awali, hakutakua ukwepaji bado ata kama akifanya maksudi kupitisha miaka iende watu wasahau.

Kama ndoa itakatalika kuvunjika msikitini au kanisani au popote pale, basi wanandoa itawalazimu wafuate njia za kimahakama, ambapo watatakiwa waende kwenye baraza la ndoa la kata wakipeleka maombi yao hayo ya kutaka kuvunja ndoa, na kwa pamoja wakiridhiana basi baraza litawapa go on to mahakama ya mwanzo,

ambako uko ikionekana kua ndoa hio iko ktk wakati ambao haiwezi kutengemaa au parties kuishi pamoja tena yaani imekufa, basi mahakama itaivunja ndoa hio rasmi na kugawanya mali na namna ya utunzaji watoto... ikumbukwe mahakama haitavunja ndoa yoyote ile ambayo itakua chini ya miaka mitatu toka ifungwe.
 
Sheria ipo ya kiserikali ya ugoni,lakini sheria ya kitaani ndio inapendwa zaidi..unafumuliwa marinda huku unarekodiwa..basi kesi imeisha
 
Ni kosa.

Wengi wetu hudharau adhabu za kisheria kwa sababu huonekana kutoendana na uzito wa kosa (ugoni).

Wengi huwa wanajipimia mkononi adhabu stahiki dhidi ya wagoni wao.
 
UMETUDANGANYA
 
Mwenye kosa hapo ni anaechepuka huku anajua anamume .au anamgonga bilakujia kama huyu nimke wamtu.huoni mwanaume anaweza kusema mm sikujua kama nimke wamtu.
Ushahidi wa mazingira utathibitisha hili,haiwezekani umechepuka na mke wa mtu ambaye mnaishi mtaa mmoja dheni useme hukujua huyu ni mke wa mtu
 
Japo post ni ya mda, lakini kuweka kumbukumbu sawa, ulichokieleza ni tofauti na kilichoulizwa. Pili umepotosha kidogo kwa kusema "ndio" kwa Tanzania bara Hamna kosa la "ugoni".
 
Japo post ni ya mda, lakini kuweka kumbukumbu sawa, ulichokieleza ni tofauti na kilichoulizwa. Pili umepotosha kidogo kwa kusema "ndio" kwa Tanzania bara Hamna kosa la "ugoni".
Hahahahaha wewe umenichekesha, nikusaidie tu ugoni kisheria unaitwa adultery, na mwezi uliopita nilikua mahakamani kwa kesi hii wilaya ya Tandahimba, Mtwara, Tanzania bara... unapaswa kujua kua sisi tuko ktk mfumo wa common law ambao una turuhusu kukopa sheria au kutumia maamuzi ya mahakama kuu na mahakama ya rufaa kama sheria.
 
Mkwala mbuzi
 
Well narrated Counsel.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…